Ushauri wangu kwa ACT Wazalendo na Maalim Seif

Ushauri wangu kwa ACT Wazalendo na Maalim Seif

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Ndugu Maalim Seif,

Tumekusikia ukikiri kupokea barua toka Serikali ya Zanzibar( Rais wa Zanzibar) juu ya kushiriki kwenu ACT Wazalendo kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Ushauri wangu kwenu ACT Wazalendo na Maalim Seif

Kamwe msiingie kwenye huu mtego. Kwa sababu kwenye miaka yote ya mapambano ya ukombozi ni mwaka huu ndo tumeona tunaenda kupata suluhisho la uhakika juu ya udhalimu wa CCM na watu wake.

Ni mwaka huu ambapo Jumuiya ya kimataifa imepata ushahidi mzito na mzuri juu ya CCM na ubaya wao hivyo wamedhamiria kweli kuchukua hatua dhidi ya CCM na vibaraka wake.

Maridhiano yoyote watakayofanya ACT na CCM kwenye hatua hii yatawafanya hata Jumuiya ya kimataifa kutuona hatunazo na tunachojali ni matumbo yetu tu.

Imefika muda ni lazima waliofanya ufedhuli wawajibishwe kwa matendo yao na wanaotaka kuwawajibisha hawawezi kupata nguvu ya kuwawajibisha kama na sie tukionesha hatujielewi na tunajali matumbo yetu!!!

Kama ni kukubaliana na CCM sharti kuu ni kuwa wale wote waliohusika na mauaji ya watu pamoja na kuiba Uchaguzi wakashtakiwe tena ICC , sio hapa Tanzania na sharti na pili liwe Uchaguzi urudiwe chini ya Tume mpya ilivyo huru na haki.

Nawaonya ACT, lolote watakalokubaliana na CCM litarudisha mafanikio tuliyoyapata mara milioni moja nyuma na hakuna hapa duniani atakaewaelewa.

Kama wao wanaangalia ruzuku ya kuendesha Chama , hawatakiwi kuhofu kwa sababu hata kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la EU limejadili Jana juu ya kuvisaidia vyama vinavyotetea demokrasia na haki za binadamu kwa Tanzania. Hivyo kama ni hela watapata zaidi ya hiyo ruzuku.

Tumefika sehemu lazima tuchore mstari kuwa kuna vitendo havitakiwi kufanyika Tanzania na vikifanywa na yeyote lazima awajibishwe iwe ndani au nje ya Tanzania.

Watanzania tumeumia sana kwa yaliyofanywa na CCM kwenye uchaguzi huu, uzuri Mungu ametuona ameleta wakombozi watusaidie kweli. Na kweli wanatusaidia, kamwe tusiwaangushe watanzania na hawa watu waliojitolea kutusaidia.

Cc.@Zitto kabwe , Ado Shaibu,@ Juma Duni Haji,@ Nassoro Mazrui, ismail Jussa
 
Hivi unadhani atakataa? Hapo ni staki nataka nipo hapa, hivi unawajua wanasiasa vizuri? Subiri utaona utabaki kinywa wazi
 
Nimeona kuna dalili kuwa atakubali. Lakini nitashangazwa sana akifanya hivyo.
Inasikitisha sana, ikitokea hilo basi wakae wakijua huo ndio utakuwa mwisho wa upinzani nchini. Yatasalia magenge ya akina Shibuda na wachumia tumbo wengine tu.
 
Wanasiasa hawatabiriki, tungoje mpaka mwakani (inshaallah) tuone kama wataendelea na msimamo wao.
 
Hakutakuwa na tofauti yoyote kubwa kama alivyopatana na Amani Karume na kuunda SUK baada ya mgogoro mkubwa wa uchaguzi wa 2000 na yaliyotokea Januari 2001.

Wakati mwingine kusamehe na kuanza upya pamoja ni busara kuliko kususiana wakati wote. Ila asifuate cheo bali kujenga umoja.
 
Ushauri Muflisi!

Mtoa hoja atambue kuwa Zanzibar na Rais Hussein mwinyi hana cha kupoteza iwapo ACT Wazalendo, haitataka kushirikiana na nayo kwenye serikali ya maridhiano ya kitaifa kwa mujibu wa katiba.

Yeye ataendelea kupiga kazi katika kutatua kero za wananchi, wakati wao wakibaki vijiweni kupiga umbea na majungu baina yao na kupeleka umbea kwa mabeberu wao, huku Maalim Seif akiendelea kunufaika na mafao ya pensheni yake, kutokana na wadhifa aliokuwa nao wa kuwa Waziri Kiongozi wa SMZ, na Makamo wa Kwanza wa Rais wa SMZ.

Wasipupmbazwe na hoja za Zitto, ambaye bila ya kutarajia, ndoto zake zimepeperushwa, na sasa anatapatapa! ataendeleaje na msala wa maisha bila ya kuwa na pahala madhubuti pa kujishikia!.
 
Akubali asikubali, au mkubali msikubali mwisho wenu umewadia hakika. Vyama venu vinakwenda kufa kifo cha mende.
 
Back
Top Bottom