Ushauri wangu kwa Diamond Platinum kabla ya kuumbuka!

Ushauri wangu kwa Diamond Platinum kabla ya kuumbuka!

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,277
Reaction score
8,860
Nimefuatilia kwa karibu tamasha la fiesta jana kuna jambo kubwa nimejifunza na sii vibaya nikamshauri huyu bwana mdogo Diamond kuwa marafiki wanakuwa karibu pindi mziki wako unapokuwa juu, wakijua watapata msaada flani kutoka kwako au faida flani.

Wanapogundua unashuka au una dallili za kuchokwa wanakukimbia mmojammoja au kuwa sehemu ya kukumaliza kabisa.
Nakuasa wee...kijana kipindi hiki ukiwa juu ukiwa na vimafanikio vya magari na vijumba utazungukwa na marafiki lakini baadhi yao ni wanafiki."sijadharau hizo mali zako ila kwa mimi naona ndio kwanza maisha unayaanza una safari ndefu kuitwa tajiri wa uhakika.

Kumbuka hawa clouds ni manyoka tena hatari na wenye sumu mbaya,wataonyesha unyenyekevu lakini baada ya kuanza kuonyesha dadili za kufanikiwa binafsi bila kuwategemea wao wameanza kukumaliza kisanii na sidhani kama hilo umeshaligundua muda sio mwingi hawa jamaa utashangaa hawaonekani tena kwenye mzunguko wako wa kifedha.
Jambo la msingi kwako na wasanii wengine mnatakiwa wanapokaribia kupoteza mvuto wa kisanii kama wewe mjiandae kuwa wajasiriamali.

Tatizo hufahamu kwamba kuna muda wa kupoteza mvuto kimziki kama ilivyokuwa kwa wasanii wenzako wa Tanzania na kimataifa jiandaa kwa hilo mdogo wangu kwa kuanza kuwa wajasiriamali,fungua hata kiwanda kidogo cha kubangua korosho kama biashara ya nguo ilikushinda.

Kinachofanyika sasa hivi na hao unaowaona marafiki zako"clouds"ni kumtengeneza All kiba afanane na saizi yako then wanakutupa na kukuzika wewe na mziki wako
Kwahiyo jiandae mapema baada ya dhamira yao hiyo kutimia uje uishi maisha ya raha na starehe, kama Sugu na wengine wengi...yaliyokukuta jana kwenye tamasha la fiesta iwe funzo kwako na kwa wengine wote.

Ni mimi mpenda maendeleo ya watu Kibo10
 
Kweli kabisa mazingira ya jana inaonesha kabisa yalikuwa kwa ali kiba
 
Kweli kabisa mazingira ya jana inaonesha kabisa yalikuwa kwa ali kiba

Na kama huyu bwana mdogo akiwaendekeza tu...atajikuta anamrudisha ally kwenye chati na yeye kushuka kabisa na wasimamizi wakuu wa tukio hilo watakuwa clouds wenyewe
 
Na kama huyu bwana mdogo akiwaendekeza tu...atajikuta anamrudisha ally kwenye chati na yeye kushuka kabisa na wasimamizi wakuu wa tukio hilo watakuwa clouds wenyewe
Clouds ni nyoka
 
Mie naomba nikuulize ina maana clouds iliwaambia watu kuwa akipanda diamond muanze kumzomea?Kama ni ushauri labda umshauri aache dharau na apunguze sifa.Nadhani hilo ndo tatizo kubwa kwa huyu kijana na pia mkumbushe asisahau alipotoka
Kabisa
Kuna kitu bahati na Kujua
Alafu kuna kupanda ngazi na kushuka
 
Hivi akikimbia ule mkoko atarudisha?

Ngoja achoke ndio atajuwa hii dunia ni tambara bovu
Maana maisha yatakuwa magumu kuliko enzi akiwa watu hawamjui zaidi zaidi watu kama hao wanaishia kuvuta unga au hata kujimaliza!!
 
Kibo10 "A perfect moment for a perfect Message"
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom