Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Kwa hulka na haiba yake ni mtu wa vituko na vibweka, hili si tatizo kwakuwa ndivyo alivyo ni hulka, ni mtu anayependa kuwa spotlight kwenye kila anachofanya (hili kuna wakati lina madhara yake)
Eric huyo wa wakati huo si huyu wa sasa! Wiki hii kapost picha akiwa kaangikwa msalabani kama Kristo Yesu na juu yake akaandika MWIZI ASAMEHEWA
Eric pamoja na kipaji chake lakini anategemea watu ili kazi zake ziweze kuonekana, ni kati ya watu hao kati yao ni wa imani anayoidhihaki
Ukiwa msanii unakuwa na wafuasi wengi, unachotakiwa kufanya ni kuishi Kwa weledi, heshima na busara na makundi yote katika jamii...utafika mbali
Wasanii wengi wameangushwa na ugomvi ulevi bifu, madawa lakini pia dharau kwenye imani za wengine