Mama, waliokushauri umkamate Tundu Lissu na kumfungulia mashtaka makubwa makubwa hayo hawana nia nzuri na wewe. Yaani, wamekupoteza/ wamekudanganya.
Nionavyo mimi ni kwamba, badala ya kudhani unatatua tatizo hapo kwa akili yangu umeongeza tatizo mara 50 zaidi. Faida ya kumfungulia mashtaka Lissu kwako ni ndogo zaidi kuliko Hasara yake.
Ipo hivi, saa hizi CHADEMA wanapitisha zile Form za Petition ambazo anasaini kila mtu bila kujali chama chake cha siasa.
Wanaosaini zile Form ni wengi sana ikiwa ni pamoja na watu wa chama chako wasiokuunga mkono.
Zile Form zikikamilika, CHADEMA watachukua hizo fomu pamoja na Kauli za Mnawie za kuiba kura na Kauli ya yule aliyekiri kwamba huwa wanawafanyia mbaya watu misituni nyakati za Uchaguzi. Lakini pia wakiunganisha na report za Waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa kwa chaguzi zilizopita(ambazo ni mbovu), wakiunganisha na hii issue ya kumkamata Lissu na kumfungulia mashtaka ya uhaini anapodai uchaguzi huru na haki, kuna kupona mtu hapo?
Matokeo yake ni pamoja na:-
1. Uchaguzi kuahirishwa.
2. Tanzania kupigwa vikwazo vya kiuchumi nk.
Yakitokea hayo mikononi mwako, wewe ndo mwenye kubeba dhambi hii yote kwa sababu Watanzania wengi watapata shida kutokana na maamuzi mabovu ya watu wako. Lakini pia kimataifa Haiba ya Tanzania itashuka sana.
Rais Jakaya Kikwete aliruhusu wapinzani kuongea hata kumtukana yeye mwenyewe, lakini pia angalau aliruhusu Demokrasia kuchukua nafasi yake ndipo wapinzani waliweza kupata wabunge, madiwani na viongozi wa serikali za mitaa/vijiji wengi sana. Je, kwa kufanya hivyo, Kikwete alishindwa kuwa Rais? Alishindwa kuunda serikali? Alipata hsara gani?
Ushauri wangu ni kwamba:-
1. Mwachie Lissu bila mashariti yoyote.
2. Kaa na CHADEMA mkubaliano baadhi ya masuala ya uchaguzi na uwashawishi CHADEMA kushiriki uchaguzi wa mwaka huu 2025.
Kwa kufanya hivyo, utakuwa kwenye mikono salama zaidi.
Mwenye masikio na asikie.