Escrowseal1
JF-Expert Member
- Dec 17, 2014
- 4,618
- 4,605
Hakuna shaka ubovu wa vyombo vya usafiri una mchango mkubwa katika ajali zinazotokea nchini ikiwemo iliyochukua uhai wa watoto wa shule hapo majuzi.
Nashauri wizara husika ipeleke mswaada bungeni ili itungwe sheria ya ukaguzi wa magari , kama usivyoweza kuendesha gari bila bima , basi kuwe na cheti cha ukaguzi wa magari kila mwaka. Kuna nchi zinafanya hivyo na kuendesha wakati gari haina ukaguzi ni kuvunja sheria. Kuna vitu vidogo vidogo huwa tunavidharau kama ,taa, wiper ,exhaust vyuma kuchakaa nk. Mamlaka huwa zinaweka standard za kila kipimo kitakachoifanya gari ama I pass au I fail. Kwa mfano tread za tairi kwa nchi ya uingereza si chini ya 1.6 mm , kwetu mpaka askari barabarani akusimamishe otherwise mpaka taili liwe kama yai la mbuni.
Kwetu vitu kama tali vipara, kutu ya vyuma, breaks , wiper , na taa , vinachangia ajali sana sana, mfano nilishawahi kusafiri na basi mvua inanyesha sana na wiper zinasiliba uso mzima wa gari na dereva wanajiamini balaa .
Kwa uingereza ukaguzi huu unaitwa MOT na kila mwaka lazima ufanyike, ukaguzi unategemea centre gharana yake ni kuanzia Tsh 60,000 kwenda juu lakini unasaidia sana sana kugundua matatizo ambayo yangeweza kuchangia ajali za barabarani.
Basi pamoja na mengine ningeomba mamlaka ziliangalie na hili suala labukaguzi wa magari kwa kuanzisha centre za ukaguzi kila wilaya maana zile swaga za wakaguzi za kujiviringisha na vi troli wakati wa wiki ya usalama barabarani havina maana na hawana vifaa vya ukaguzi na ni muhimu kuwe na agency ya ukaguzi .