sanshinda
Member
- Sep 25, 2017
- 79
- 33
1. UTEUZI WA WACHEZAJI
Haukuzingatia uhalisia kwa kuwa wachezaji waliofanya vizuri kwenye ligi ya ndani hawakujumuishwa, mfano Mkude kwenye kiungo cha kukaba, Ajibu kwenye pasi za mwisho alipngoza Tanzania nzima kwenye eneo hilo, Ayee kwenye kufunga na wengineo.
2. BODI YA LIGI
Kutokuwepo kwa bodi ya ligi inayoaminika kumechangia sana kubadilisha ratiba ya ligi mara kwa mara kwa misingi ya utashi au kutokuwa na weledi, hali hiyo imesababisha kuwepo kwa msimamo wa ligi usiokuwa na uhalisia ma pia kuwafanya wachezaji kutokuwa na utimamu wa mwili endelevu
3.LIGI KUKOSA WADHAMINI
Hii imesababisha kutokuwepo mazingira sawa miongoni mwa washindani ambao ni vilabu, matokeo yake msimamo wa ligi hauakisi hali halisi ya ubora wa timu
4.WAAMUZI WA LIGI KUU
Kumeonekana wazi baadhi ya waamuzi kuzibeba baadhi ya timu na kuziangamiza baadhi ya timu huku bodi ya ligi ikifumba macho na masikio ya wadau wake wakuu wanapolalamika na kujikita zaidi kwenye kupangua ratiba bila ulazima na bila kuangalia athari za kiuchumi na kisaikolojia kwa timu.
5. WAANDISHI WA HABARI
Waandishi walitumia kalamu zao kuipamba Taifa stars kwa sifa ambazo hawana au tuseme hawajafikia.
6. UONGOZI WA TIMU YA TAIFA
Uongozi huu uwe na mchanganyiko ambao unabeba taswira ya Taifa badala ya uliopo sasa ambao unaonesha taswira ya wasanii na viongozi wachache tena waliopo Dar es salaam
7.SULUHISHO
Kwa maoni yangu ni vyema TFF ikaweka nguvu kubwa kwa vijana U23, U20, U17, na kurejeshwa kwa mashindano ya mikoa ambako kutaleta hamasa kubwa na kupata wachezaji wenye vipaji kwa njia rahisi mno n.k huku serikali nayo ikiimarisha mashindano ya shule za msingi na sekondari.