Ushauri wangu kwa Wakuu wapya wa Wilaya

Ushauri wangu kwa Wakuu wapya wa Wilaya

Ndugu zangu watanzania,

Kwanza niwapongeze Sana kwa dhati ya moyo wangu wakuu wote wa wilaya walioteuliwa na mh Rais wetu mpendwa mzalendo wa kweli Jasiri shupavu na madhubuti Mama Samia Suluhu Hassan,Ni heshima kubwa Sana na Imani kubwa Sana mliyopewa na mh Rais, mmepata heshima hiyo Kati ya mamillioni ya watanzania wenye uwezo pia wa kushika nafasi hiyo,Tambueni kuwa mmepata uongozi kwa Neema za Mwenyezi Mungu ambapo siku zote tunasema uongozi unatoka kwa Mungu

Tambueni kuwa mmepata nafasi hizo ili mkawatumikie watu na siyo kutumikiwa, mkawasikilize watu kero zao na changamoto zao na kuzitafutia majibu, mmepewa nafasi hizo ili mkamsaidie mh Rais katika wilaya zenu,Hivyo Nendeni mkachape kazi,mkawafute machozi wenye kulia,mkawape matumaini wenye kukata Tamaa,mkarudishe Tabasamu kwa wenye maumivu na shida,mkawashe Taa ya maendeleo katika wilaya zenu , mkawasaidie wenye kuonewa na mkawe sauti kwa wasio na sauti

Nendeni mkatatue kero na siyo kuwa walalamikaji,msiende kumuonea mtu Wala Kutumia vyeo vyenu kwa manufaa yenu binafsi, nendeni mkajenge ushirikiano wenye tija katika kuwatumikia watanzania na siyo kushirikiana na yeyote kuihujumu serikali na kuiibia serikali,Nendeni mkawe wasuruhishi wa migogoro na siyo chanzo Cha migogoro,Nendeni mkawe chanzo Cha amani na siyo chanzo Cha uvunjifu wa amani.

Katangulizeni busara hekima na upendo katika maamuzi yenu,msifanye maamuzi kwa jazba Wala hasira,kuweni wauungwa na wenye subira, msimvumilie yeyote mwenye kuwa kikwazo katika kuwahudumia wananchi,Tendeni haki kwa haki kwa kila mwenye kustahili haki, kasimamieni vizuri na kufuatilia kwa ukaribu fedha zote za serikali zinazopelekwa katika miradi iliyo katika maeneo yenu kwa kushirikiana na wakurugenzi wenu.

Ni aibu na fedheha mbio za mwenge zinazopita Mara moja kwa mwaka kuja kugundua ufisadi katika fedha za umma katika maeneo yenu huku nanyi mpo Tena mkiwa kimya,fuatilieni na kuhakikisha mnasoma vizuri ripoti za CAG ili kujuwa Ni wapi katika wilaya zenu panastahili kuchukuliwa hatua za kiuchunguzi na kuwajibishana kwa kuwabana wahusika, hakikisheni kuwa kila mtu Ni lazima aiogope kuichezea fedha ya umma Kama ukoma,Ni lazima miradi ya serikali ifanyike kwa ufanisi na kwa Kiwango kinachostahili.

Msiende kukaa maofsini tu Bali tokeni maofisini na kwenda kwa wananchi kujionea Hali halisi ya maisha Yao ,namna wanavyohudumiwa ,kusikilizwa na pia kuwasikiliza kero zao na kuwapatia majibu,msisubili kila kitu kuletewa mezani pasipo kujiridhisha,nendeni kila eneo la wilaya zenu mkajionee uhalisia maana magari mnayo ambayo Ni kwa ajili ya kazi hizo.

Hongera Sana mh Rais wetu kwa Kuendelea kuweka Timu madhubuti na shupavu ambayo italeta ushindi dhidi ya maadui wetu wa Ujinga, maradhi na umasikini japo adui mwingine wa Rushwa na ufisadi anatakiwa apigwe Sana ili kufanya jitihada zote unazozifanya za kutafuta fedha huku na kule zinazaa matunda kwa pesa za umma kuwa salama na kutumika Kama ilivyotarajiwa na kuleta matokeo chanya badala ya kupotelea katika mifuko ya watu wachache wasio na uchungu na maisha ya watanzania wanyonge.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
Na kujipendekeza kote kule huchaguliwi hata ukatibu kata, shame on you
 
Wandugu aliyependa ushauri wa mwenzetu pia,sio vibaya kumtumia hata pesa ya Pongezi...M-Pesa ihusike basi ..
 
Na kujipendekeza kote kule huchaguliwi hata ukatibu kata, shame on you
Kilimo ndio ajira yangu na ni heshima kwangu kwa kuwa ninashiriki katika kulinda usalama wa Taifa letu kwa kuhakikisha kuwa chakula kinakuwepo cha kutosha hapa nchini,maana huwezi ukamuongoza wala kusikilizwa na mtu mweye njaa ya chakula na Wala hakuwezi kukawa na utulivu nchini ikiwa watu wananjaa
 
Unalimia mtandaoni
 
Najua hujapenda kuandika ujumbe huu bali ni hasira za kutoswa
Niwe na hasira ya Nini ndugu yangu,kwani Kuna siku nimeandika hapa kuwa Nina subiri uteuzi,Mimi huwa Nina andika hapa kwa hiyari yangu na uzalendo wangu na kutokana na namna ninavyoridhishwa na utendaji kazi madhubuti na wakutukuka wa serikali ya mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani kipenzi Cha watanzania
 
Mwashambwa pole ndugu yetu kwa kukosa teuzi kwa mara ya kumi, chama lenu uchawa peke yake hautakutoa, muhimu ni connections kama huna utaendelea kuchakaza soli za viatu
 
Mwashambwa pole ndugu yetu kwa kukosa teuzi kwa mara ya kumi, chama lenu uchawa peke yake hautakutoa, muhimu ni connections kama huna utaendelea kuchakaza soli za viatu
Mimi naandika hapa jukwaani kwa hiyari na uzalendo kwa Taifa langu na kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa mama Samia kwa kazi nzuri na yakutukuka anayoifanya katika kuwatumikia watanzania
 
Acha kujisumbua ndg [emoji23][emoji23] mama sio Magu zile zama za ukisifia sifia unateuliwa zimepita ingekuwa ukisifia unateuliwa basi Steve Nyetere ambaye ni chawa no 1 wa mama angeshateuliwa
So acha kusumbua akili yako kama unamsifia mama sifia kawaida sio mpk uandike no ya sm [emoji23][emoji23]
Unaandika no ya sm ya nn?[emoji23][emoji23] unadhan mama ni Magu kuwa atakukumbuka?[emoji23][emoji23] utakufa maskin na nakala zako
Andika nakala sifia then kimya sio unaandika andika no za sm kujipendekeza [emoji23][emoji23][emoji23] hiloooooooooo [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ninayoyaandika hapa siyo barua za maombi ya uteuzi Bali Ni maoni yangu binafsi
 
Back
Top Bottom