CCM wanatumia kila njia kuwatongoza ACT na CHADEMA ili waingie kwenye serikali na ubunge, kwa kinachoendelea bado kwa upande wa Zanzibar hali imekuwa ngumu zaidi na zaidi kila kunapokucha haswa kunapotokea vifo vinavyoendelea vya wahanga wa ulioitwa uchaguzi Mkuu.
Upande wa Tanganyika au tuseme Tanzania bara kumetokea sintofahamu ambayo itahitaji wakuu wa CHADEMA kutoa kaulimbiu ya kilichotokea kama kina baraka au hakina baraka kuhusiana na wabunge wanawake wa kuteuliwa kuingia bungeni.
Zanzibar kila kijiwe hakipo tayari kuona ACT inaingia kwenye serikali ya Rais Hussein Mwinyi,wananchi walio wengi wanasema kila mtu abebe mzigo wake kwa maana hawataki kuona wala kusikia ACT inaingia kwani hakuna faida na zaidi wanadai hakukuwa na uchaguzi wa aina yeyote kilichotokea ni kuwaharibia watu muda wao.
Kuna habari kuna kundi kubwa la walioteswa huko Pemba ambao hali zao zimekuwa tete na zinazoashiria kupoteza maisha wamehamishiwa hospitali za Dar es Salaam ili lifanyike la kufanyika kuokoa hali zao baada ya Hospitali za Pemba kuelekea kushindwa kuwatibu kwa majeraha waliyopewa na vikosi vya SMZ.
Haiwezekani kwa ACT kujiunga na serikali ya Rais Hussein Mwinyi hata dakika moja utakuwa ni usaliti kwa wanachama wa ACT na wapiga kura.
Wanachokitafuta CCM ni kwa vyama hivi kuingia katika serikali zao haramu ili waitangazie dunia kuwa uchaguzi umekuwa ni wahalali na walioshindwa wameshindwa kihalali,zilikuwa ni peresha za kushindwa tu ,sasa wametulia na wameshaingia kwenye serikali kama haitoshi wataandika mabarua makubwa makubwa kupeleka kwa mabeberu kuwa kila kitu shwari na hakuna tena mvutano watanzania wote ni wamoja huku wakionyesha picha za kideo wabunge wa upinzani kushiriki serikalini.
Chadema fukuza chama wabunge wote waliopokea hela na kununuliwa kwa bei mbaya na hata maalim akienda kuingia kwenye serikali atafukuzwa chama.
CCM moja ya faida watakayoipata kama hawa ni kuingiza fitina ndani ya vyama na kusababisha viongozi na wanachama kufarikiana.