Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Naandika kama mdau na mzoefu kwenye kada husika
Kuna wengi wetu hapa hawana ufahamu wa ulimwengu wa magari na biashara yake inavyofanyika... Hii sio kesi wala huwezi kuwabeza kwakuwa si kila mmoja wetu hapa ni mjuzi wa kila kitu.. Hivyo basi kwa wale wenye ufahamu zaidi kuhusu jambo fulani kutuzidi si mbaya kutoa elimu
Nimekuwa mfuatiliaji wa karibu wa wadau wanaouza magari yao hapa JF kwasababu zozote zile na wale ambao Mungu anewajaalia wamepata chochote kitu na wanataka nao kutembelea makalio na si miguu tena
Kwa wauzaji
Wengi hawana ufahamu kamili na biashara ya magari hivyo kujikuta anauza bei kubwa kwa sababu mbili au tatu hivi
. Hofu ya kudhani anauza bei poa
. Tamaa ya kutaka faida kubwa
.Kutojua uhalisia wa bei sokoni
. Fikra za kulipa thamani kubwa gari lake tofauti na uhalisia
Wengi wamejikuta wanashindwa kuuza gari zao na kuishia kupata maudhi toka wadau wasio na simile..! Yaani badala ya kukuelimisha wanaishia kukuchamba na kukukebehi
Ushauri wangu kwao ni huu njia sahihi ya kuuza gari yako kwa muktadha wa kupata bei elekezi au bei kikomo weka tangazo la kutaka kununua gari lenye vigezo sawa na lako unalotaka kuuza
Vilevile tembelea site mbalimbali zinazouza magari Tanzania.. Baada ya kujua hali halisi ya bei sokoni sasa unaweza kuweka tangazo la kuuza gari yako
NB: Zingatia sana hili kamwe usibandike tangazo la kuuza gari kwenye gari husika..hiyo gari haitauzika
Kwa wanunuaji magari JF
Wengi wanakwama kwenye swala la bajeti na hili pengine kama sio ubahili basi ni ufahamu finyu
Mtu anatangaza hitaji la kutaka kununua gari na anaweka na offer kabisa kumrahisishia muuzaji! Hili si tatizo ni jambo zuri ILA shida inakuja kwenye vigezo vya gari analohitaji..ukija kufananisha kwenye uhalisia, vigezo na bei vinaachana mbali sana
Gari za bei poa ni za kwenda nazo kwa makini sana nyingi zina matatizo yaliyojificha ambayo muuzaji hayuko tayari kukueleza. . Na ni kati ya hizo gari zenye vigezo vingi kwa bei poa ndio matapeli hupata nafasi ya kukupiga
Natambua kuna baadhi huuza magari genuine kabisa yasiyo na tatizo lolote na yaliyotunzwa vizuri kwa bei poa sana..Hawa wapo na wengine huuza kutokana na dharura za kimaisha ..lakini kwa bahati mbaya sana hizi gari za namna hii hudakwa juu kwa ju na walengaji
Ushauri wangu
Unapotaka kununua gari ya bei poa kwa bajeti yako usiwe na haraka wala kutwezwa na lugha tamu za wauzaji na wawakilishi wao...Chukua muda kuzikagua kupitia wajuzi waaminifu... Hakikisha nyaraka ni halisi na hazina shida kuanzia mamlaka ya mapato, mikopo kwenye taasisi za fedha, umiliki/ jina/ mirathi nknk..