Ushauri wangu kwa wauza magari na wanunuzi ndani ya JF

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Naandika kama mdau na mzoefu kwenye kada husika
Kuna wengi wetu hapa hawana ufahamu wa ulimwengu wa magari na biashara yake inavyofanyika... Hii sio kesi wala huwezi kuwabeza kwakuwa si kila mmoja wetu hapa ni mjuzi wa kila kitu.. Hivyo basi kwa wale wenye ufahamu zaidi kuhusu jambo fulani kutuzidi si mbaya kutoa elimu

Nimekuwa mfuatiliaji wa karibu wa wadau wanaouza magari yao hapa JF kwasababu zozote zile na wale ambao Mungu anewajaalia wamepata chochote kitu na wanataka nao kutembelea makalio na si miguu tena

Kwa wauzaji
Wengi hawana ufahamu kamili na biashara ya magari hivyo kujikuta anauza bei kubwa kwa sababu mbili au tatu hivi
. Hofu ya kudhani anauza bei poa
. Tamaa ya kutaka faida kubwa
.Kutojua uhalisia wa bei sokoni
. Fikra za kulipa thamani kubwa gari lake tofauti na uhalisia

Wengi wamejikuta wanashindwa kuuza gari zao na kuishia kupata maudhi toka wadau wasio na simile..! Yaani badala ya kukuelimisha wanaishia kukuchamba na kukukebehi
Ushauri wangu kwao ni huu njia sahihi ya kuuza gari yako kwa muktadha wa kupata bei elekezi au bei kikomo weka tangazo la kutaka kununua gari lenye vigezo sawa na lako unalotaka kuuza
Vilevile tembelea site mbalimbali zinazouza magari Tanzania.. Baada ya kujua hali halisi ya bei sokoni sasa unaweza kuweka tangazo la kuuza gari yako
NB: Zingatia sana hili kamwe usibandike tangazo la kuuza gari kwenye gari husika..hiyo gari haitauzika

Kwa wanunuaji magari JF
Wengi wanakwama kwenye swala la bajeti na hili pengine kama sio ubahili basi ni ufahamu finyu
Mtu anatangaza hitaji la kutaka kununua gari na anaweka na offer kabisa kumrahisishia muuzaji! Hili si tatizo ni jambo zuri ILA shida inakuja kwenye vigezo vya gari analohitaji..ukija kufananisha kwenye uhalisia, vigezo na bei vinaachana mbali sana
Gari za bei poa ni za kwenda nazo kwa makini sana nyingi zina matatizo yaliyojificha ambayo muuzaji hayuko tayari kukueleza. . Na ni kati ya hizo gari zenye vigezo vingi kwa bei poa ndio matapeli hupata nafasi ya kukupiga

Natambua kuna baadhi huuza magari genuine kabisa yasiyo na tatizo lolote na yaliyotunzwa vizuri kwa bei poa sana..Hawa wapo na wengine huuza kutokana na dharura za kimaisha ..lakini kwa bahati mbaya sana hizi gari za namna hii hudakwa juu kwa ju na walengaji

Ushauri wangu
Unapotaka kununua gari ya bei poa kwa bajeti yako usiwe na haraka wala kutwezwa na lugha tamu za wauzaji na wawakilishi wao...Chukua muda kuzikagua kupitia wajuzi waaminifu... Hakikisha nyaraka ni halisi na hazina shida kuanzia mamlaka ya mapato, mikopo kwenye taasisi za fedha, umiliki/ jina/ mirathi nknk..
 
Kabisa,hao wauzaji wakitaka kupata bei halisi kulingana na gari analouza bei elekezi ni hii:-

1.Aangalie bei ya gari kwa japan yaani CIF eg labda 3000USD basi hapo hadi Bongo aongeze 90% ya CIF = 5700 USD hadi analitoa bandarini.

2.Kitu cha Pili aangalie gari limetumika kwa miaka mingapi bongo ,gari lina depreciate kwa 20% ya Price kila mwaka ,hii inaamanisha kama price ilivyotua bongo ilikuwa USD 5700 means baada ya mwaka inatakiwa bei akitaka kuuza iwe 5700USD-(20% ya 5700) = usd 4560

3.Hapo inategemea pia na condition ya gari kama kaifilimba bei inazidi kushuka.
 
Naandika kama mdau na mzoefu kwenye kada husika
Kuna wengi wetu hapa hawana ufahamu wa ulimwengu wa magari na biashara yake inavyofanyika... Hii sio kesi wala huwezi kuwabeza kwakuwa si kila mmoja wetu hapa ni mjuzi wa kila kitu.. Hivyo basi kwa wale wenye ufahamu zaidi kuhusu jambo fulani kutuzidi si mbaya kutoa elimu

Nimekuwa mfuatiliaji wa karibu wa wadau wanaouza magari yao hapa JF kwasababu zozote zile na wale ambao Mungu anewajaalia wamepata chochote kitu na wanataka nao kutembelea makalio na si miguu tena

Kwa wauzaji
Wengi hawana ufahamu kamili na biashara ya magari hivyo kujikuta anauza bei kubwa kwa sababu mbili au tatu hivi
. Hofu ya kudhani anauza bei poa
. Tamaa ya kutaka faida kubwa
.Kutojua uhalisia wa bei sokoni
. Fikra za kulipa thamani kubwa gari lake tofauti na uhalisia

Wengi wamejikuta wanashindwa kuuza gari zao na kuishia kupata maudhi toka wadau wasio na simile..! Yaani badala ya kukuelimisha wanaishia kukuchamba na kukukebehi
Ushauri wangu kwao ni huu njia sahihi ya kuuza gari yako kwa muktadha wa kupata bei elekezi au bei kikomo weka tangazo la kutaka kununua gari lenye vigezo sawa na lako unalotaka kuuza
Vilevile tembelea site mbalimbali zinazouza magari Tanzania.. Baada ya kujua hali halisi ya bei sokoni sasa unaweza kuweka tangazo la kuuza gari yako
NB: Zingatia sana hili kamwe usibandike tangazo la kuuza gari kwenye gari husika..hiyo gari haitauzika

Kwa wanunuaji magari JF
Wengi wanakwama kwenye swala la bajeti na hili pengine kama sio ubahili basi ni ufahamu finyu
Mtu anatangaza hitaji la kutaka kununua gari na anaweka na offer kabisa kumrahisishia muuzaji! Hili si tatizo ni jambo zuri ILA shida inakuja kwenye vigezo vya gari analohitaji..ukija kufananisha kwenye uhalisia, vigezo na bei vinaachana mbali sana
Gari za bei poa ni za kwenda nazo kwa makini sana nyingi zina matatizo yaliyojificha ambayo muuzaji hayuko tayari kukueleza. . Na ni kati ya hizo gari zenye vigezo vingi kwa bei poa ndio matapeli hupata nafasi ya kukupiga

Natambua kuna baadhi huuza magari genuine kabisa yasiyo na tatizo lolote na yaliyotunzwa vizuri kwa bei poa sana..Hawa wapo na wengine huuza kutokana na dharura za kimaisha ..lakini kwa bahati mbaya sana hizi gari za namna hii hudakwa juu kwa ju na walengaji

Ushauri wangu
Unapotaka kununua gari ya bei poa kwa bajeti yako usiwe na haraka wala kutwezwa na lugha tamu za wauzaji na wawakilishi wao...Chukua muda kuzikagua kupitia wajuzi waaminifu... Hakikisha nyaraka ni halisi na hazina shida kuanzia mamlaka ya mapato, mikopo kwenye taasisi za fedha, umiliki/ jina/ mirathi nknk..
Asante sana. Sasa sijui huu ugonjwa wa kupenda vya chee (kwa wanunuzi) na kutotaka kujifunza kwa baadhi ya Watz kutaisha lini. Si magari tu, tunateseka maeneo mengi tu.
 
Shortcut is the longest way you were not going... Vya chee vina gharama kubwa
 
Gari hii kuna mtu alikuwa anauza alitangaza hapa jf na alieleza kabisa tatizo, bei yake ilikuwa hata 5mil anapokea. Nashukuru alikuwa muadilifu.

2867570_IMG_20210321_104131_952.jpg

2867573_IMG_20210624_171123_000.jpg
 
Eti mkuu, hivi hii X Trail jamaa alifanikiwa kuiuza? Maana nilikuwa naivizia. Au unaweza kuurudisha ule uzi wake jukwaani ili nijaribu kumuuliza!
Habari wakuu,

Nauza gari yangu Nissan x-trail tatizo nimetembelea bila oil injini ikaanza kugonga na kwasasa sina hela ya kununua injini mpya nipe offer yako nikuachie gari ufunge injini mpya, haina tatizo lolote zaidi yahilo.
Usajili. No DBX
Injini mpya inauzwa milioni moja tuuh.
Gari... Car4Sale - Nauza Nissan x-trail
 
Back
Top Bottom