Mkandara Heshima mbele
Mimi nikiwa muumini mzuri wa mageuzi na niliyekubaliana na Zito katika harakati zake siwezi tetea kuhusu uhusika wa mtu yeyote yule kwenye tuhuma za Rushwa. Wote waliopata tuhumiwa watu wao waliwatetewa kwa nguvu zao zote. Hii ilileta madhara pale ilipothibitishwa vinginevyo.
Ninaweza nikawa siamini kweli Zito kala rushwa, ila kinachonipa tabu kwanini atajwe, ahisiwe kwanini hata mtu afikiri anaweza kula Rushwa, nilivyomwamini Zito pamoja kwamba kunamambo mengi huwa hatukubaliani naye sijawahi kufikiri anaweza kula Rushwa wala kutoa. Ila kwa sababu rushwa ni matokeo ya madaraka, tamaa, na uchu wa utajiri lolote linawezekana.
Kazi ya chadema ni kuweka wazi kuwa Rushwa haikubaliki ndani ya chama kipimo kile kile tunachokitumia kwa watawala na viongozi wa serikali ndicho kitumike kwa watuhumiwa wa CDM kama wapo. Huanza na tetesi, shutuma then udhibitisho.
Rushwa imeharibu wengi sana Nyerere alimwamini sana Mkapa hata akaitwa Mr Clean leo unaweza kutumia hilo jina. Kinachoniudhi sana ni kubadilika kwa viongozi wetu kitabia na utendaji.
Zitto hasemwi ovyo ovyo isipokuwa wanajua Zitto ndiye kiungo kikubwa cha pande mbili za mtazamo kitikadi ndani ya Chadema. Navyoamini mimi, ktk swala la Uchaguzi mkuu na utawala -chama cha CCM huchukulia hili kama wako vitani na ndio maana wanasema - Ushindi wa Uchaguzi mkuu utapatikana kwa njia yoyote ile..Na siku zote CCM hutafuta sehemu inayoweza kukiyumbisha chama mbadala cha Upinzani kwa kutafuta their weakest point of entry..Hivyo wakaona mahala ambapo wanaweza penyeza ngome ya Chadema ni Zitto. Ndio maana Zitto alipewa wenyekiti wa kamati ya JK kuhusu madini wakati uleee, Mnyika akaja juu sana kupinga uteuzi ule kinyume cha matakwa ya chama, lakini kwa furaha kubwa Zitto akaingia mzima mzima. Toka pale CCM wakamkamata na kuhakikisha anaambukizwa gonjwa la upinzani wowote ndani ya Chadema dhidi yake ni kwa sababu yeye Muislaam..
I know all these things toka vijiwe vya mujini, tena walimpa Zitto hadi mafaili ya kina Mbowe na viongozi wengine waliopokea rushwa ama kuwa upande wa kina RA na EL kumpitisha JK uchaguzi wa 2005. Vitu vingine vilitungwa kuhakikisha Zitto anaweka mashaka ktk dhamira ya viongozi wake. Na wala sii kosa lake tu, uongozi wa Chadema pia kwa kuelewa hivyo walianza kumtenga, kutomwamini maana mtu yeyote anayefanya kazi na serikali wakati hakuna makubaliano ya Bipartisan ina maana yuko upande wa pili..
Sijui kama unakumbuka Senator Joe Lieberman wa Marekani, huyu alikuwa Presidential material alipokuwa Democratic lakini kutokana na msimamo wake wa ndumila kuwili, alianza kutengwa akajikuta pekee na kila siku hakosekani CCN kwa kashfa na misimamo yake, mwisho ilifikia kuhama chama na leo hii kabakia senator tu ambaye hana mbele wala nyuma..Hivi ndivyo siasa inavyoweza kukujenga ama kukubomoa.
Mambo yote hyanayohusiana na Zitto yametengenezwa na CCM ili wanaCHadema mzidi kukosa matumaini naye na kwa kufanya hivyo mtagawanyika. Zitto ana watu wanaomwamini sana na ambao wanajua fika kwamba ndani ya Chadema kuna mtandao vile vile.. Na tumeyaona mengi hapa JF jinsi Zitto anavyosakamwa na WanaChadema wenyewe. Kuna makundi ndani ya chama na pengine naweza kusema kwamba tunaweka sana matumaini kwa Dr.Slaa wakati ikifika 2015, sidhani kama kiafya na Umri, atakuwa na nguvu kama za jana na leo - simwombei mabaya lakini nasema what if?.....
Let's say kwa hali ambayo haikutegemewa Dr.Slaa hatagombea Urais - Je, tuna chaguo gani jingine -Ni Tundu Lissu? Mbowe? Mnyika? au Prof. Safari?....Na kwa nini jina la Zitto lisiwepo?
Zitto anapakazwa sana kwa malengo na hasa wabunge ambao wanapokea posho ilihali Zitto ndiye sababu ya kukatwa ongezeko..Zitto na Makamba wana maadui wengi tu muhimu ni wao kufahamu makosa yao kama vijana mnaowategemea kesho.