USHAURI: Watumishi wakopeshwe pensheni yao kwa riba ndogo au bila riba badala ya kutegemea mikopo ya mabenki yenye riba kubwa

USHAURI: Watumishi wakopeshwe pensheni yao kwa riba ndogo au bila riba badala ya kutegemea mikopo ya mabenki yenye riba kubwa

x - mas

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
931
Reaction score
612
Ukifikiria kiundani utagundua mtumishi anufaiki sana na mkopo anaokopa, wanufaika wakubwa wa mikopo kwa wafanyakazi ni mabenki/taasisi zinazohusika na ukopeshaji kupitia faida inayotokana na riba, mikopo inapelekea chanzo cha Maisha magumu kwa watumishi waliowengi huku ikiwaacha wakopeshaji wa kiwa na ukwasi mkubwa.

Mtumishi anakopa bank wakati kwenye mfuko wake wa mafao ana mamilioni.

Ushauri wangu kwa wahusika wa mambo ya wafanyakazi Tanzania wengeanzisha utaratibu wa kukopesha watumishi pesa kotokana na mafao yake mwenyewe mfanyakazi na utaratibu wa kulipa deni hilo uwe kama ulivyo sasa kupitia mshahara wake hadi deni litakipoisha.

Kwanini ukope bank wakati una mamilioni kwenye mfuko wa mafao? Kupitia mkopo wa mafao naamini mtumishi ataweza kukopa bila riba na kama riba itakuwepo basi itakuwa ni kiasi kidogo ambacho mwisho wasiku bado kitaendelea kutunisha mfuko wa mafao wa mtumishi hivyo kufanya anapostaafu kuwa na pesa nyingi Zaidi kupitia mkopo ambao kajikopesha mwenyewe.

Kwa utaribu huu kwa asilimia Zaidi ya mia mkopo utamnufaisha mtumishi na siyo hii mikopo ya sasa ambayo inanufaisha zaidi Mabank.

Kukopa bank kuwepo lakini kama chaguzi/option.
 
Wazo lako zuri lakini pesa zenyewe sijui kama zipo maana wastaafu wasingehangaika kupata mafao yao.
 
Fao la kujitoa ni suluhisho la kukuza uchumi na kupunguza tatizo la ajira. Mtu mkataba wake wa kazi ukiisha apewe mafao yake akawekeze kwenye biashara au kilimo nk. kwa kufanya hivyo ataweza hata kuajili watu wengine.

Kuliko hivi sasa kwamba mkataba wake wa kazi ukiisha aingie tena kwenye soko la ajira kucompete na watu ambao kila mwaka wanagraduate na kua mzigo kwa serikali.
 
Back
Top Bottom