Ushauri wenu unahitajika: Boss wangu anataka kunidhulumu mshahara wangu

Ushauri wenu unahitajika: Boss wangu anataka kunidhulumu mshahara wangu

mwmbeki

Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
91
Reaction score
124
Ndugu wapendwa mimi ni mwalimu wa shule moja ya secondary hapa arusha, yapata mwaka mmoja sasa tangu niajiliwe shuleni hapo January 2017 baada ya kumaliza shaada yangu ya elimu august 2016.

Kulingana na ugumu wa ajira nilikubali anilipe mshaara mdogo tu Tsh 200000tu, tulifanya kazi vizuri nikiwà kama Mtaaluma wake cheo alichonipatia mapema baada ya kuanza kazi, lakin hakuwai kunipa mkataba wala barua ya maangalizi(probation letter). hii ni kwa wafanyakazi wake wote.

Mishahara yake kwa watumishi imekuwa ni ya kusuasua sana..ilipofika mwezi wa saba 2017 ikakwama kabisa..kwa hiyo watumishi wake wameishi bila mishahara tangu mwezi wa saba mwaka jana 2017.

Mimi wa mwezi wa saba nilibahatika kupata na ndo ulikuwa wa mwisho hadi namaliza mwaka lkn alihaid atatoa pesa zote January 2018 baada ya wanafunzi kufungua na kusema amekwama japo sababu za kukwama zilikuwa hazijulikani.

Mimi nimemwambia sitaendelea na kazi hivyo anipatie pesa yangu yote naona anataka kuleta chenga

kibaya zaidi ana chuo cha kitapeli hapo hapo shuleni kwake,anaajili walimu waliofeli form four ndo wafundishe secondary na chuo,yeye mwenyewe hana taaluma yoyote lkn ndo director na ndo mkuu wa shule yaan anaendesha tasisi kitapeli tapeli na ana mapungufu mengi sana,na shule yake haistahili kuwa hata kituo cha tuition

Pamoja na kutokuwepo kwa mkataba lkn nilikuwa nasain kwenye daftar LA maadhulio ya walim kila siku,nilikuwa nasain kwenye class journal kila baada ya kufundisha.

Nimfanyeje ??
 
cha kukushauri kama hizo details ni za ukweli na unauhakikika nazo nenda halmashauri umlipue aweze kupata stahiki za kudanganya ww japokua ulikua unashida ulikosea kuanza kazi pasipo mkatabaa wwte ww na boss wako anauwezekano wa kukukana cuz hamna ushaidi wa mkataba wa kisheeria ila usikate tamaa jaribu kufatilia kwanza ili upate muafaka wa swala lako

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
hili ni tatizo kubwa, chukua hatua kwa kupeleka mashtaka, wala sio malalamiko, ngazi husika ili kuokoa jahazi. Utajiokoa mwenyewe, utaokoa walimu wako na utaokoa wanafunzi wanaosoma hiyo shule bubu.
 
Kimsingi na kisheria, unastahili kupata stahiki zako licha ya kutokuwa na mkataba wa ajira lakini kwao hicho ulichokieleza wewe ni mwajiriwa kama ilivyo kwa wengine.
 
Duuh! Hivyo vyuo vimekuwa vingi vya kimagumashi cha kushangaza vimesajiliwa na VETA
 
pole sana ndugu kwa tatizo lako hilo. Nakushauri muone afisa elimu wa mkoa wako kwa ufumbuzi wa haraka juu ya tatizo lako au Katibu tawala wa mkoa. Hao wana mamlaka ya juu ktk suala lako kulipatia maamuzi,
 
Kwa mujibu wa sheria ya "the sale of goods Act "CAP 214 R. E 2002......formalities of contract...
Section 5(1) subject to the provision of this Act and of any other written law in that behalf, a contract of sale may be made in writting (either with or without sale) or by word of mouth, or partly in writing and partly by word of mouth or may be implied from the conduct of the parties.........

Sasa hapo kwenye may be implied inamana hata bila kuandikishina lkn kuna huduma ulikuwa unamsaidia kutoa tayari kuna mkataba hivyo basi anatakiwa kukilipa
 
Sasa hii sheria inafungamana na masuala y kuuza na ununuzi wa bidhaa tu, huyu tatizo lake lina tatuliwa na ELRA
 
cha kukushauri kama hizo details ni za ukweli na unauhakikika nazo nenda halmashauri umlipue aweze kupata stahiki za kudanganya ww japokua ulikua unashida ulikosea kuanza kazi pasipo mkatabaa wwte ww na boss wako anauwezekano wa kukukana cuz hamna ushaidi wa mkataba wa kisheeria ila usikate tamaa jaribu kufatilia kwanza ili upate muafaka wa swala lako

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
Hawezi kutumia class journal aliyokuwa akisaini kila kipindi anachofundisha kama ushahidi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom