Ushauri wenye mantiki na staha: Dreamliner iuzwe, pesa itakayopatikana itumike kujenga shule na madarasa yanayohitajika

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Nchi yetu ina upungufu mkubwa sana wa vyumba vya madarasa na shule. Maana wanafunzi wengi huwa wanakosa masomo sababu ya kukosa madarasa ya kusomea au shule kuwa mbali na maeneo wanayoishi.

Kuliko serikali kukopa pesa World Bank na kuzitumia kujenga madarasa na shule. Bora Dreamliner tulilonunua kwa bilioni 520 za kitanzania liuzwe na pesa itakayopatikana itumike kujenge madarasa na shule.
 
Mimi naona tungegawana tu hizo hela baada ya kuuza hilo dreamliner lao!! 😇 Au mnaonaje ndugu zangu!!!

Maana mtaani kwenyewe huku hata hakusomeki!!
 
Umenena vizuri.
 
Hoja mujarabu kabisa hatuwezi kuwa na Madege yaliyopaki huku hatuna shule bora za kutosha

Naunga mkono hoja.
 
Yaani maamuzi ya ununuzi wa Dreamliner yalikuwa ya kukurupuka..ndege limepaki hasara juu ya hasara!!

Afu ukisemwa unalalamik kwamba ni vita ya kiuchumi vya mabeberu na mawakala wao.
 
Tokea yanunuliwe ni hasara na muda unakwenda, ngoja tusikie gharama za matengenezo
 
Kisha mtaacha kuzaa ili sasa pesa itayopatika ifanya mambo mengine?
 
Hau Hauna akili wewe utauza hata makochi ya ndani mwako ukiishiwa. Baada ya kushauri hela zitafutwe unashauri vitu viuzwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…