Ushauri: Wilaya za Kibaha na Bagamoyo zihamishiwe Dar es Salaam, Mbagala na Kigamboni zipelekwe mkoa wa Pwani

Ushauri: Wilaya za Kibaha na Bagamoyo zihamishiwe Dar es Salaam, Mbagala na Kigamboni zipelekwe mkoa wa Pwani

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Kipindi nakua mji ulikuwa mwisho ubungo, pale lilipo jengo la Tanesco ndio ulikuwa mzani wa kupima malori ambao sasa uko mkoa wa Pwani, Dar inakuwa kuelekea kaskazini,npaka wa Dar na kibaha unafutika, mpaka wa Dar, Bagamoyo unafutika kwa kasi sababu ya ujenzi unaokuwa kwa kasi ya ajabu.

Jiografia ya mkoa wa Pwani inashangaza sana, mtu wa Bagamoyo akitaka kwenda Rufijii au mafia lazima apitie Dar au apande chombo cha baharini. Ushauri wangu

Hizi wilaya mbili Kibaha na Bagamoyo zije Dar, ili kubalance mapato na uchumi wa mkoa wa Pwani Kigamboni na Mbagala yote iende Pwani,waungane na Mkuranga,Kisarawe, Mafia Kibiti na Rufiji.

Faida zake:

Jiji la Dar eS Salaam litapumua kwa kupata ardhi ya kutosha na kukua kwa kasi ya ajabu kibaha itakuwa kama urusi kwa technology na viwanda na Bagamoyo zitakuwa kama ukraine kwa utalii, pata picha chalinze iwe ni sehemu ya Dar es Salaam.

Tuje Pwani sasa.

Pwani kwa kupewa Kigamboni na Mbagala itachangamka sana, tatizo la Pwani ni kukosa amsha amsha. Mbagala itakuwa Dubai mpya kwa biashara mpaka sasa Mbagala inazidi baadhi ya mikoa kwa idadi ya watu na amsha amsha ya kibiashara njoo Mbagala kuanzia saa kumi jioni mpaka saa nne usiku hutaamini macho yako kila aina ya biashara utaikuta .pata picha Mbagala iko Pwani na na sehemu ya Kigamboni itakuwa Paris au Spain sehemu za kula bata kwenye fukwe.

Bandari ibaki Dar.Wakazi wengi wa Mbagala wana asili ya Pwani au Kusini mwa Tanzania, watafurahi kurudi nyumbani kwa style nyingine.
Chawa wa mama mfikishieni hii
 
😆😆😆 mkuu geographia yako bado haijakaa sawa

Unapoepeleka Kigamboni Pwani ni makosaa
Iyo kigamboni unayoisema iende pwani ni kigambon hii hii au ipo nyingine ?

Kigamboni hihii ya ferry mpaka kibada pale kuna short cut ya kutokea Kijichi mtoni, ambako ni DSM

Suluhisho hapa ni kuanzisha mkoa mpyaaa utakaojumuisha wilaya za rufiji, mkuranga , kibiti, mafia hapo ndipo binafsi naona ni solution ila sio.kuichukua kigamboni kuipeleka pwani
 
[emoji38][emoji38][emoji38] mkuu geographia yako bado haijakaa sawa

Unapoepeleka kigamboni Pwani ni makosaa
Iyo kigamboni unayoisema iende pwani ni kigambon hii hii au ipo nyingine ?

Kigamboni hihii ya ferry mpaka kibada pale kuna short cut ya kutokea Kijichi mtoni, ambako ni DSM

Suluhisho hapa ni kuanzisha mkoa mpyaaa utakaojumuisha wilaya za rufiji, mkuranga , kibiti, mafia hapo ndipo binafsi naona ni solution ila sio.kuichukua kigamboni kuipeleka pwani
Mwache mdukuzi ajikoroge mkuranga iwe na bandari yake alaf aone kama kariakoo haijagawana matumizi na mbagala
 
Mimi ningekua na uwezo ningehamisha mkoa mzima wa pwani na morogoro na kuuleta Dar ili kutengeneza mkoa mmoja, service delivery ingekua ndio msingi sio utitiri wa hii kitu,nchi nzima mikoa 12 tu.
😂😂😂 Ukubwa ulionao Morogoro kwa sasa hujatosheka nao unataka uiongezee na pwani pamoja na Dar boss😅 fikiria kwanza
 
Kama nakupata vile ,alafu huo mkoa moya ukianza bagamoyo na kibaha ziende wapi,
 
Mwanaume wa mkoani una-suggest vitu vya hovyo kabisa hata wazazi na ukoo wako wakisikia watasikitika!

Anyway Dar was part of Pwani mpaka miaka ya sabini. Ndio ilikuwa makao makuu ya mkoa wa Pwani,pale Ilala Boma. Na wakazi wa Dar na Pwani wote wanafanana. Wazaramo na Wandengereko. Kwa wao ni sawa ila kwa wewe unayejitahidi kujisahaulisha mkoa ulipotoka/your orgin unaumia kiasi cha kuanza kuwabagua wamachinga,wamakua na wamakonde wanaoishi Mbagala ambao ni sawa na wewe wakuja.
 
Kama nakupata vile ,alafu huo mkoa moya ukianza bagamoyo na kibaha ziende wapi,
Kibaha na bagamoyo zitabikia zilipo

Na hata Mhe SSH alipo kwenda Mkuranga last time wana mkuranga wenyewe wali propose ilo na waliambiwa wajiandaae kimipango then likipatikana fungu basi watafikiriwa

Which is true, unakuta mtu anakaa mkuranga anataka kuja ofisi ya mkoa anasafiri mpaka Dsm then akamate mwendokasi mpaka kimara then mwendokasi tena wa kuja kibaha
 
Kibaha na bagamoyo zitakuwa mkoa gani
 
Kimsingi dsm ibaki kama ilivyo..ila ardh yote irudi serikalini na wakazi wadsm wahamishwe serikali ijenge magorofa appartments za kutosha kisha warususiwe kuja kupangisha tu..hakuna kuruhusu mtu kujenge kama unataka kujenge nenda kajenge pwani huko.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mwache mdukuzi ajikoroge mkuranga iwe na bandari yake alaf aone kama kariakoo haijagawana matumizi na mbagala
Bandari bubu zipo.mpaka.Mbweni huko, kunduchi mbona hatujaona iyo kariakoo mpya ?

Kuwa na eneo lililo changamka kibiashara ndani ya mkoa, wilaya ni faida ya mapato so hata ukipatikana mkoa mpya

Utakao jumuisha mkuranga Dc, Rufiji, Mafia, Kibiti bado kariakoo itabakia kariakoo tu kinachotazamwa hapa ni urahisi wa upatikanaji wa huduma za kiserikal kwa urhisi
 
Mbweni, kunduchi mkuu hazifanan n mbagala.. Haziifikii hata nusu kibiashara mkuu fanya utafiti ujue mbagala Ina soko la wat kias gan kibiashara.. Idad ya wat hapa usiku ni tishio Kam Ile ya Kongo mchana! Fanya tafiti kabla za kiufanano
 
Hili suala nimekua nikiling'amua pia.
Dar es salaam needs expansion kama si sasa basi huko mbele itahitajika hivyo.

Psychologiacally people are uncomfortable to live outside dar es salaam's boundaries

Hivyo kwa maana ya kukuza uchumi wa mji ni lazima tuepuke retention of population humo jijini kwa kuliongezea mipaka ya kijiografia.

Tanzania_location_map.svg.png

Kuna faida kadhaa kufanya hivyo kuliko kubaki hivyo lilivyo
 
Mimi ningekua na uwezo ningehamisha mkoa mzima wa pwani na morogoro na kuuleta Dar ili kutengeneza mkoa mmoja, service delivery ingekua ndio msingi sio utitiri wa hii kitu,nchi nzima mikoa 12 tu.
Umuhimu wa provinces(majimbo).
 
😂😂😂 Ukubwa ulionao Morogoro kwa sasa hujatosheka nao unataka uiongezee na pwani pamoja na Dar boss😅 fikiria kwanza
Wewe ndio ufikirie mkuu, people's wants services delivers sio ukubwa wa eneo!Zambia wana mikoa isiyozidi 15,Botswana sio zaidi ya 12 na SA ambayo ni kubwa kuliko yetu Ina mikoa 9tu(na wanataka kuipunguza)maendeleo sio utitiri wa wilaya au mikoa, middle class wewe Lina utarudi and smell roses on the ground?
 
Back
Top Bottom