Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

ulimchana kuhusu dharau zake??
 

Umenikumbusha mbali sana!

Father yangu anapenda sana swala la undugu, yeye mtu wa mbali kabisa atakuambia 'kamtafute huyo ndugu yetu kabisa'.

Wakati nimepangiwa kazi mkoa fulani, kuna ndugu yake father alikuwa Meneja wa litaasisi likubwa sana(kafariki now). Father akapiga kelele sana mtafute huyo mtu ni ndugu yetu kabisa usikae kipweke. Akawasiliana nae kabisaa kumwambia uwepo wangu huko. Akamjibu poa.

Siku, nimetoroka ofisini fresh nikaenda ofisi yao fasta ili sasa kumsalimia na kutambuana, kufika getini nikajitambulisha kama mgeni wa nani kwa walinzi.

Akapigiwa simu (extension) kutoka getini kutaarifiwa ujio wangu, yaan namsikia kabisa anahoji ni nani huyo akaambiwa kila kitu ila mwisho wa siku akawaambia walinzi mwambieni sipo na msimruhusu kuingia.

Angewaambia kwamba mwambieni nipo busy, ningemuelewa ningemtafuta siku ingine ila kitendo cha kusema eti mwambieni sipo! Nilikata mguu na sikutaka hata kumjua tena, father alipiga kelele sana wala sikuhangaika tena.

Hamadi! Kuna mkulu mmoja alikuja kwa ziara ya taasisi yetu na kwenye majumuisho akaomba wakuu wa taasisi zote za umma na binafsi pale mkoani waalikwe! Ilikuwa inaanza saa moja jioni.

Kwenye utambulisho tulianza sisi, tuliokaa high table jirani na mkulu tena MC anakutaja we unapungia. Wao waalikwa wakajitambulisha wenyewe, unapewa mic unajitaja unatokea taasisi gani na cheo chako. Coz namjua jina nipolisikia jina lake tu nikawa makini kumuangalia maana sikuwahi kumuona physically.

Kumbe naye aliponisikia akawa makini kuniangalia.

Kwenye coctail party anajileta leta kinoma halafu anashangaa sana na kuniuliza, kumbe we ndo mtoto wa fulani?! Mi namjibu vyema kabisa na hakuficha mshangao wake.

Baada ya siku ile alinitafuta yeye, tukawa na undugu imara! Alianza yeye kuja home ndo nami nikaenda kwake.

Moyoni nikajua alinikwepa awali akijua kinachofuata ni kuombana misaada akidhani ndiyo naanza maisha!
 
Huyu ni msomi aliyekosa direction, lzm adate[emoji16]
Bimdash unashombo mzigo kama uwendi chooni we F.

Nakausha kwasababu kuna ishu nachonga na mtu Current sitaki Ban ila wewe ni unashombo za kisen ku makini.
 
Hongera Boss. Inaonekana wewe ni mstaarabu sana na umepata exposure kubwa kwa nchi za wenzetu ndio maana hukujali sana hata pale ulipodharaulika.

Safi sana
 
Mkuu usingemalizia kwa kusema una mwili mdogo,ningekwambia mimi.
 
Huu uzi full kujimwambafai Full kuvutia upande wako Sio wa kinyonge yani

Humu ndio utaona chumvi za mawe na chumvi za unga,nimeandka kisa changu

nimekisoma mwenyeweee nikaona Hapana Hii hebu nitulie nayo kabatini maana.

Tupeane story za ukweli wajuba mnao ongeza chumvi ongezeni kwa kiasi sio mpk inakereketa.
 
Angalau wewe hata visa vyako vina muelekeo hubabaiki

Sio kina mwafulan " mi meneja mara boss aaagh, vitu havina uhalisia kabisa aagh[emoji21]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…