Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Du[emoji26]
 
Heshimu yeyote bila kujali umemkutaje. Vingine havipo kama unavyoviona/kufikiria.
Dada zetu wanachemka sana hapa.
Mkuu kuna wanawake hawaonagi mbele, wanafikiri situation ya mtu kuwa hohehahe ni permanent.....ikibadilika wanashangaa......Kuna mwanamke alinikataa katakata nikiwa chuo katakata yaani asee acha tu.......last year nilikuwa na chat nae ananiambia ananipenda namwambia mimi nishaoa anasema hivyo hivyo anataka awe side chick......she is pretty ana kazi yake na maisha yake.....lakini sahivi age ishatembea hakuna mdau anatangaza nia, halafu kazi yake ni porini hamna wadau hata wakumuona.....nadhani anataka anitegeshee mimba......
 
Hahahahaha

Sent from my SM-N910W8 using JamiiForums mobile app
 
Ulitisha mkuu
 
Nipe namba zake plz
 
Huyo katibu mkuu nae atakuwa siyo mstaarabu tu. Kusalimia watu kwake ni shida? Ni mmoja wa wale waliolewa madaraka.
Lakini salamu sio lazima mkuu. Maana hata ukimsalim mtu akakujibu hayuko salama utamsaidiaje mkuu?
 
Nahisi wewe utakuwa mrembo sana na combination uliyosoma ni PCB/PCM. Mwalimu alitegemea uwe HKL.
Hahah wala sio hivyo bhana, ila ni Kweli nimesoma 1 ya comb kati ya hizo ulizotaja.
 
Kuna mpangaji mwenzangu tulikuwa tunaishi vzri sana ila sasa ni muongo mnafiki sana akawa anatangaza kwamba mimi na wife tuna maisha magumu tuna lala chini Mungu mme wake anajua kutafta pesa niliumia mwzi wa 8 mme wake amefumaniwa akapigwa mpka kufa mwanamke alikuwa haongeagi na majirani baada ya kupata taarifa za mme wake kuawa akaanza kuomba msamaha
 
Imeniuma sana hii...inafanana kabisa na mimi
 
Ulitisha mkuu
 
Niliwahi kwenda ofisi fulani (kampuni ya simu) kwa ajili ya kuonana na mtu wa marketing kuna mradi ofisi yetu ilikua inafanya nao.
Sikua na appointment kwa makusudi ili nijionee wanavyohudumia wateja maana mradi ulikua unahusisha kutoa huduma kwa wateja ambao ba sisi wanatuhusu.
Nilifika na kukaa zaidi ya dakika 10 bila kua attended af si mnajua kuna maofisi Mlinzi anamamlaka utasema meneja anavyoamrisha [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]. I was very patient na observe tu. Meneja alikua na ka meza kake kwenye kona....I walked to him nikamsalimia "Habari kaka"....hakuhangaika wala kujibu salamu akauliza "Una shida gani???" Nikamsahihisha nikamuambia "Sio kila anaekuja ana-shida ungeniambia karibu ni kuhudumie kisha mimi ndio ningesema kama nina shida ama nahitaji huduma nyingine"....kabla hajapata nafasi ya kujibu nikajitambulisha.
Natamani kuchora picha uso wake ulivyotahayari ila itoshe kusema aliona aibu [emoji1].
 
Mwaka 2012 wakati nipo kituo cha Tembon - Mbezi wingu la mvua likatanda ghafla kwa sababu nilkuwa naelekea maduka tisa ikabidi nikodishe bajaji fasta ili hata mvua ikinyesha kabla sijafika nisilowe basi bhana wakati naita bajaji kwa pembeni mbali kidogo na nilipo alisimama manzi fulani hivyo baada ya kuelewana na bajaji nikapanda nashangaa haondoki kumbe anasubria manzi apande anajua niko naye hadi nikamwambia mbona unazubaa au unataka mvua inikute hapa wala hakusema kitu akawasha chombo tukasepa wakati tupo njian ndo ananiambia ninaonekana ni mtu wa totoz hivyo alijua yule niko nae, nikwambia ndo maana umenipga parefu unajua nipo na demu siwezi kuchomoa yaan muda wote alibaki kunishangaa kwamba kumbe mi mstaarabu kuliko alivyonidhania mtu wa totozi
 

Huo mstari wa mwisho umebeba kila kitu. Nimemuonea huruma japo simjui. Maisha yanabadilika mno dah
 
Uzi mzuri huu.unafundisha sana
Mnoooo.... kwa miaka yangu kadhaa ya kuishi nimeona mambo ya kutosha kunifunza kuto dharau/ kushusha thamani mtu.
Asubuhi napo ingia mzigoni sina kale katabia kakupita mlinzi au mfagizi kama sio mtu; nasalimia na kuulizia hali ya familia kisha naendelea na siku yangu. Dereva , mhudumu wa chakula wote nawapa heshima inayostahili.
Nishawahi ingia kwenye mgahawa nikamsalimia mdada vizuri tu na kumtania kirafiki kisha nikaagiza...Huwezi amini aliniambia hicho usile sio fresh bora ule chakula flani ni fresh na kimepikwa vizuri. Ningeingia kwa nyodo na dharau ningejulia wapi hayo [emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…