Nimekumbuka kisa kingine......Miaka ya nyuma nikiwa nasoma nilikuwa na ndoto yakufanya kazi kwenye NGO moja hapa nchi, nilikuwa siachi kuangalia website yao kila wiki. Basi wakati masomo yana karibia nikaenda physically kabisa kujitambulisha na kuomba kujishikiza, uzuri nikakutana na rafiki wa dada yangu ndo programme manager akanipokea poa kweli akaniambia nafasi hamna lakini zikipatikana tutakwambia basi nikatoka moyo kweli
Nikaendelea kuomba na sehemu nyingine, uzuri nikaja kupata kujishikiza kwa miezi sita kwa wadau wengine ambao actually wenyewe wanatoa funds kwa NGOs including ile ambayo rafiki yake dada yupo. Basi maisha yakawa yanaendelea sasa ule mwezi wa sita ulipofika ikabidi nianze kutafuta exit strategy nikaenda tena kwa yule rafiki wa dada, nikamwambia kule niliko jishikiza mkataba ni miezi sita tu hawawezi kuextend kwa hiyo kama itawezekana anisaidie nijishikize......weeeeeee huo moto alioniwashia sio wa nchi hii kwanza akaniambia kama ungekuwa unafanya kazi vizuri wangekuajiri, halafu kwanin unang'ang'ania kazi kwetu tu kweni hamna kwingine, i was so shocked sikuamini ni mtu yule yule wa mwanzo.....Nikampigia sista anakaniambia ndo watu walivyo mdogo wangu
Asee Mungu sio Athumani, miezi sita inaisha, naletewa mkataba wa kuwa assistant portifolio manager yaani hawataki hata kuitangaza yaani with immediate effect. Yaani yule mzungu ananipa mgongo nilifunga mlango nikapiga magoti nakulia kwa uchunguuuu mwingiii mnooooo nikamshukuru Mungu sana.
Sasa basiiiii proposal za NGO zikawa ili zifike kwa portifolio manager lazima nizipitie kwangu, guess whaaat ile NGO ikawa inaleta pia proposals. Nikamwambia Mungu i want to be different sita ipendelea sita ionea wameandika utumbo natupa kule wameandika vizuri na irecommend......one time wakapata CEO mpya wakaomba kuja kuonana na Manager wangu bahati nzuri jamaa alikuwa kaenda holiday na familia yake kaniachia kila kitu ni handle.....Wamekuja yule programme manager ananiangalia hanimaliziiiiiiii.......Jamani huyu Mungu huyu muoneni hivihivi