Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Lakini salamu sio lazima mkuu. Maana hata ukimsalim mtu akakujibu hayuko salama utamsaidiaje mkuu?
Pengine uko sahihi. Sina sababu ya kukubishia maana tumelelewa, tunalea na kunaishi katika mazingira tofauti.
 
Kuna kipindi mzee alipata ajali moshi alikuwa ameenda kumchukua dogo shule mzee anakacheo serikalini sasa walianza kumzingua pluss na kaprocess kibao alipata ajali mida ya saa tano ila alikaaa kituon mpaka saa mbili kisaa process nyingi yeye mwenyewe alikiri wanamzingua sana na mzee ni introvert hanaga maneno mengi luckly enough siku iyo gari yake ya kazini ndo ilikuwa inakuja kumchukua stk baada ya lile gari kufika pale alisema mambo yalikuwa marahisi zaidi aliondoka na kesho yake asubuhi wakamaliza process dakika 0 akarudi kazini

Kipindi nasoma o level ilikuwa likizo nilikuwa nasoma tuition mjini yaaaan kulikuwa nakaumbali nilikuwa mtundu by the time nakula nauli sana afu mida ya kurud home nazinguana na madereva nq makondakta mpaka wakanizoea nilikuwa nawalilia shida sana by the time mzee alikuwa anamiliki hiace nne ambazo zinapiga route hayo maeneo kiukwel nilikuwa nafaham mbili tu sasa siku wanaleta maesabu home ilikuwa sio kawaida kuyaleta home walikuwa wanakutanaga huko wanapoyapark wakanikuta na mzee walicheka huku wakishangaaa walimpaa mzee a to z wakamuambia kwadogo anavyoleta mbanga huko town hata hafananii sema walidhani mtoto wamasikini kupita kiasi
 
Nimekumbuka kisa kingine......Miaka ya nyuma nikiwa nasoma nilikuwa na ndoto yakufanya kazi kwenye NGO moja hapa nchi, nilikuwa siachi kuangalia website yao kila wiki. Basi wakati masomo yana karibia nikaenda physically kabisa kujitambulisha na kuomba kujishikiza, uzuri nikakutana na rafiki wa dada yangu ndo programme manager akanipokea poa kweli akaniambia nafasi hamna lakini zikipatikana tutakwambia basi nikatoka moyo kweli

Nikaendelea kuomba na sehemu nyingine, uzuri nikaja kupata kujishikiza kwa miezi sita kwa wadau wengine ambao actually wenyewe wanatoa funds kwa NGOs including ile ambayo rafiki yake dada yupo. Basi maisha yakawa yanaendelea sasa ule mwezi wa sita ulipofika ikabidi nianze kutafuta exit strategy nikaenda tena kwa yule rafiki wa dada, nikamwambia kule niliko jishikiza mkataba ni miezi sita tu hawawezi kuextend kwa hiyo kama itawezekana anisaidie nijishikize......weeeeeee huo moto alioniwashia sio wa nchi hii kwanza akaniambia kama ungekuwa unafanya kazi vizuri wangekuajiri, halafu kwanin unang'ang'ania kazi kwetu tu kweni hamna kwingine, i was so shocked sikuamini ni mtu yule yule wa mwanzo.....Nikampigia sista anakaniambia ndo watu walivyo mdogo wangu

Asee Mungu sio Athumani, miezi sita inaisha, naletewa mkataba wa kuwa assistant portifolio manager yaani hawataki hata kuitangaza yaani with immediate effect. Yaani yule mzungu ananipa mgongo nilifunga mlango nikapiga magoti nakulia kwa uchunguuuu mwingiii mnooooo nikamshukuru Mungu sana.

Sasa basiiiii proposal za NGO zikawa ili zifike kwa portifolio manager lazima nizipitie kwangu, guess whaaat ile NGO ikawa inaleta pia proposals. Nikamwambia Mungu i want to be different sita ipendelea sita ionea wameandika utumbo natupa kule wameandika vizuri na irecommend......one time wakapata CEO mpya wakaomba kuja kuonana na Manager wangu bahati nzuri jamaa alikuwa kaenda holiday na familia yake kaniachia kila kitu ni handle.....Wamekuja yule programme manager ananiangalia hanimaliziiiiiiii.......Jamani huyu Mungu huyu muoneni hivihivi
 
Mnoooo.... kwa miaka yangu kadhaa ya kuishi nimeona mambo ya kutosha kunifunza kuto dharau/ kushusha thamani mtu.
Asubuhi napo ingia mzigoni sina kale katabia kakupita mlinzi au mfagizi kama sio mtu; nasalimia na kuulizia hali ya familia kisha naendelea na siku yangu. Dereva , mhudumu wa chakula wote nawapa heshima inayostahili.
Nishawahi ingia kwenye mgahawa nikamsalimia mdada vizuri tu na kumtania kirafiki kisha nikaagiza...Huwezi amini aliniambia hicho usile sio fresh bora ule chakula flani ni fresh na kimepikwa vizuri. Ningeingia kwa nyodo na dharau ningejulia wapi hayo [emoji3]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka saan lol
 
Binafsi huwa sipendi MTU anayependekeza salamu. Ujue salamu ni aina ya malipo ama kumnunua MTU moyo wake ili akusaidie kitu Fulani. Ina mana bila ya salamu husaidiwi.
MIE hata ukinipita bila ya salamu afu unarudi umepotea njia nakuelekeza kiroho safi na hata ukinisalimia kama kuninunua ili ndipo nikuelekeze MIE naipotezea salamu yako na kama Nina muda nakupeleka mpaka unakoenda.

Warusi ukiwauliza kitu afu wakakusaidia na ukiwashukuru wanaikataa shukrani yako kwa kuuliza ya nini iyo shukrani. Ina mana wako willing kukusaidia bila hata kuwalipa.

Sasa bongo ndipo utashangaa MTU anakomalia salamu utadhani itamuwekea chakula mezani.

Binafsi sipendi kusalimiwa naonaga kama ni utumwa Fulani yaani ni lazima usalimie kila asubuhi. MIE wangu aishanielewa hakuna salamu hata kama nikitoka kwa wiki nzima. Nikirudi unapita muda kidogo tunaanza story za huku home na huko nilikokuwa.

Wazazi wangu hawakuwa watu wa kudemand salamu kila siku asubuhi. Ilikuwa ni kuamshwa kuwahi shambani basis.
Mpaka umri huu huwa nikienda home salamu ni zile siku za ugeni wiki ikishapita hakuna salamu.

Pia siamini kuwa salamu ndio heshima.

Nina imani masikini anapenda sana salamu mana kwa njia hiyo anajisikia faraja sana anadhani naye anajariwa. Masikini ndiye anayetembelea ndugu zake waliofanikiwa na kuwaongelea na kuringishia watu. Kuwa usinidharau yule karibu mkuu ni mdogo wangu nimemsomesha MIE. Ni kama Mwita weitara akasomeshwa na kaka yake aliyekuwa nauza mayai hapo kipunguni saivi sijui wanakaa kivule.
Ni mfano tu nimetolea hapa kwa karibu mkuu.

Salamu ni muhimu ila isiwe lazima jamani .yaani kuna watu wanaifanya kuwa basic needs kwao.
Binafsi nikiwaga home kwetu huwa siishi kwa furaha mana kila unayepishana naye yabidi u pay attention kwake na umpatie salamu tena usimame mpige story kidogo.sasa ole wako uje upite usalimie ukipunga mkono nakuambia ,Fulani anaringa kisa akasoma ,ama ana Hela.

Ila nikiwa town salamu sio lazima naishi kwa Uhuru hakuna MTU anayejiliza kuwa umetupita bila ya salamu rafiki.

Binafsi kunyenyekea ama kunyenyekewa sipendi.

Haya shikamooni wana jf wote waliozaliwa 65 kurudi nyuma. Wa 66 mpaka 1990 mambo vipi. Waliozaliwa 90 mpaka 2020 mnipe heshima Yangu

Unadhani kwa salamu Umepata nini katika maisha yako hata nisingekusamia si ungebaki na shida zako zilezile ama kuna kitu kimeongezeka.

Binafsi I hate salamu ingawa ni opener ya maongezi. Kuna watu naowakubali sana binafsi unamuuliza MTU kitu anakujibu mwishoni unashukuru na kumpatia salamu yake unasepa. Watu wa ivyo huwa naowanga ni matajiri rohoni kwao ni matajiri rohoni mwao!!!!!
Hii nimeipenda nchini MALAWI , hamnaga mambo ya salamu ni kuulizia shida yako then sepa.

Sent from my TA-1024 using JamiiForums mobile app
 
mkuu kwanza nikupongeze kwa ujinga wako wa shobo za kitoto
ungetakiwa umpoteze apaparike yeye sasa
wewe umeanza tena shobo kwake kweli nyani haoni kundule
atakupenda kwa sababu ya unapofanyia kazi nasio real love

amka kaamuombe alaaah akufungue senge wewe
 
hii iliwai nikuta bagamoyo nimeenda kuichakata pisi yangu moja tamu sana rangi kama wale watoto wa Brazil kule hotel ni millennium sea breeze resort nililala room ya laki mbili sasa asubui nimeamka na demu wangu tumeenda kunywa chai jamaa wakawa wanatuuliza mmelala room gani nikawaonesha na walituona wakati tunashuka toka room jamaa bado wakawa wanaleta dharau wakasema tukalete kadi ya kufungulia mlango tukaleta eti ndio wanaamini wanaanza kushoboka na kutuudumia vizuri nili boreka sana na hotel haikuwa na watu wengi sasa sijui kwa umri wangu walijua siwezi ku afford iyo room wakati nilikua na milioni tisa ya kula bata kwenye akaunti niliwazarau sana wale jamaa watu maskini sijui wana mentality gani
badili Avatar
 
Mnoooo.... kwa miaka yangu kadhaa ya kuishi nimeona mambo ya kutosha kunifunza kuto dharau/ kushusha thamani mtu.
Asubuhi napo ingia mzigoni sina kale katabia kakupita mlinzi au mfagizi kama sio mtu; nasalimia na kuulizia hali ya familia kisha naendelea na siku yangu. Dereva , mhudumu wa chakula wote nawapa heshima inayostahili.
Nishawahi ingia kwenye mgahawa nikamsalimia mdada vizuri tu na kumtania kirafiki kisha nikaagiza...Huwezi amini aliniambia hicho usile sio fresh bora ule chakula flani ni fresh na kimepikwa vizuri. Ningeingia kwa nyodo na dharau ningejulia wapi hayo [emoji3]
Ukiwa peace na kila mtu kuna Mambo unaweza yaepuka .
 
Hii nimeipenda nchini MALAWI , hamnaga mambo ya salamu ni kuulizia shida yako then sepa.

Sent from my TA-1024 using JamiiForums mobile app
Ndo mana yake mkuu. Uelewe kama sio shida ya huyo jamaa hakuna salamu ungeipata. Tangiapo ukiipata iyo salamu haikuongezii wala kukupunguzia kitu chochote.
Sema hapa unakuta hapa MTU ana shida zake ama ni masikini wa Mali,pesa,elimu,wadhifa,uongozi ama umasikini wowote ule. So kupitia salamu pekee ndipo anataka naye aheshimwe mana hajawahi kuheshimiwa ama kuongoza ama kumzidi mwingine kwa chochote. MTU kama mwalimu ama no dewj anashida ya salamu ya kunyenyekewa kwa salamu. Mana hizo mambo akazipata mpaka amechoka yaani zimemkinai. Ni kama MTU akienda sehemu Mara ya kwanza kama ulaya na hana uhakika wa kurudipo lazima atafanya mauzo mtandanoni
 
Nimekumbuka kisa kingine......Miaka ya nyuma nikiwa nasoma nilikuwa na ndoto yakufanya kazi kwenye NGO moja hapa nchi, nilikuwa siachi kuangalia website yao kila wiki. Basi wakati masomo yana karibia nikaenda physically kabisa kujitambulisha na kuomba kujishikiza, uzuri nikakutana na rafiki wa dada yangu ndo programme manager akanipokea poa kweli akaniambia nafasi hamna lakini zikipatikana tutakwambia basi nikatoka moyo kweli

Nikaendelea kuomba na sehemu nyingine, uzuri nikaja kupata kujishikiza kwa miezi sita kwa wadau wengine ambao actually wenyewe wanatoa funds kwa NGOs including ile ambayo rafiki yake dada yupo. Basi maisha yakawa yanaendelea sasa ule mwezi wa sita ulipofika ikabidi nianze kutafuta exit strategy nikaenda tena kwa yule rafiki wa dada, nikamwambia kule niliko jishikiza mkataba ni miezi sita tu hawawezi kuextend kwa hiyo kama itawezekana anisaidie nijishikize......weeeeeee huo moto alioniwashia sio wa nchi hii kwanza akaniambia kama ungekuwa unafanya kazi vizuri wangekuajiri, halafu kwanin unang'ang'ania kazi kwetu tu kweni hamna kwingine, i was so shocked sikuamini ni mtu yule yule wa mwanzo.....Nikampigia sista anakaniambia ndo watu walivyo mdogo wangu

Asee Mungu sio Athumani, miezi sita inaisha, naletewa mkataba wa kuwa assistant portifolio manager yaani hawataki hata kuitangaza yaani with immediate effect. Yaani yule mzungu ananipa mgongo nilifunga mlango nikapiga magoti nakulia kwa uchunguuuu mwingiii mnooooo nikamshukuru Mungu sana.

Sasa basiiiii proposal za NGO zikawa ili zifike kwa portifolio manager lazima nizipitie kwangu, guess whaaat ile NGO ikawa inaleta pia proposals. Nikamwambia Mungu i want to be different sita ipendelea sita ionea wameandika utumbo natupa kule wameandika vizuri na irecommend......one time wakapata CEO mpya wakaomba kuja kuonana na Manager wangu bahati nzuri jamaa alikuwa kaenda holiday na familia yake kaniachia kila kitu ni handle.....Wamekuja yule programme manager ananiangalia hanimaliziiiiiiii.......Jamani huyu Mungu huyu muoneni hivihivi
God is GOOD
 
Kuna siku niliazima gari nikaenda pale best bite kuchukua zaga.

Sasa nilivyoingia ndani nikakutana na pisi tatu za kwenda zinatoka ndani, nikazipa hi zikachuna full kunipandisha na kunishusha, nikaona POA tu nikafuata kilichonipeleka.

Sasa ile natoka nje nikazikuta ziko bize zinajisnap kwenye gari niliyokua nayo, hiiiiiiiiii bagoshaaa, mbona walikoma kunijua.

Nilianzisha zogo la maana makusudi kabisa, nikaita mpaka uongozi wa pale nikawaambia wawaambie wateja wao wafute picha zote walizopiga gari yangu otherwise niite Askari pale obey waniambie Wana lengo gani na picha za mkwaju wangu?
Hah hah hah daah we jamaa noma sana
 
Mimi imenitokea hii:

Niliweka tangazo kule love connect kuwa 'natafuta mke ' sio kuwa amepotea - hapana; yaani lengo langu nivute jiko niweke ndani.

Wakati naandika tangazo nilikuwa na asilimia 100 kuwa JF imesheheni wadada wasomi na wanaojielewa. Natambua kuwa wapo wasomi hadi kufikia level ya PhD lakini Diploma + bachelor na masters wapo wengi mno. Jamani msiwadharau wadada wa humu wengi ni wasomi na wana kazi zao za heshima mnoo.

Kwenye sifa zangu: nimesema mimi ni mweusi, mwembamba na elimu yangu ni darasa la saba[emoji2][emoji2][emoji2]

Aiseee yaani wadada wa Jf wote waliopitia tangazo langu hata wale wenye uhitaji kama mimi na sifa wanazo; wote wamenidharau wamepita kimya kimya. Huwezi amini; hadi leo hii sijapata pm hata moja[emoji23][emoji23] kweli hakuna wa kunifaa?, nahisi nadharaulika kwa hii elimu yangu ya darasa la saba[emoji23][emoji23].

NB: najua tatizo ni elimu yangu ya darasa la saba , na wadada wengi jf ni wasomi wa hali ya juu - form four hadi mbele huko PhD .
Jamani pamoja ni darasa la saba lakini ninatafuta mke jamani, kuwa mimi la saba sio ishu jamani.
Hadi leo hii bado wamenidharau na wala sijapata PM ya kumpata mwanamke wa ku-anzisha nae familia pamoja.

Bado nafasi ipo wadada jamani ...acheni kutudharau sisi darasa la saba.
Wadada wenye akili wamekusikia mkuu na uhakika atakaekuja atavuna haswa shida hawa dada zetu wanafikiri kwa kutumia makalio
 
mkuu kwanza nikupongeze kwa ujinga wako wa shobo za kitoto
ungetakiwa umpoteze apaparike yeye sasa
wewe umeanza tena shobo kwake kweli nyani haoni kundule
atakupenda kwa sababu ya unapofanyia kazi nasio real love

amka kaamuombe alaaah akufungue senge wewe
[emoji3][emoji3]..matusi ya nn sasa?kwan wapi ulisikia nimesema AM LOOKING FOR REAL LOVE?
 
Miaka 20 ilikuwa ni around 2000 na simu za kumilikiwa na madereva daladala hazikuwepo. Madereva wakadrive km kadhaa kuja kuonesha magari nanyi mkiwa mmengojea[emoji23]
Mbona kaweka neno pale "i think" au hujui matumizi yake
 
Back
Top Bottom