Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Haaahaaa ABSA kama ABSA

na utapigwa life ban zezetaa wewe, ID nyingi humu unatafuta kazi ama?

Mara ujidai umekufa, mara ufufuke we mwanaume wa aina gani, ngoja nifukue makaburi yako ya ovyo ovyo ..

Mfyuuuuu [emoji57][emoji57]
[emoji2][emoji2][emoji2]
 
1.Mimi kwenye nyumba ya ibada siku hiyo nilivaa shati na sweta kubwa kisha juu yake nikavaa kizibao fulani jamaa alinipa nje nimshikie...

kwenye kuswali (msikitini) sasa vijijini mashekhe wana tabia ya umwinyi swala inakimiwa wanajivuta kupanga swafu me nikaona isiwe tabu nikajipeleka pale mbele kabisa nakumbuka yule jamaa akaniondoa huku akisema hapa ni nafasi ya mashekhe mpaka leo simsahau na mpaka leo walio wengi hawajuagi kuwa mimi nimeiva kwenye dini

2.Nilienda shule fulani ndanindani huko kabisa kipindi cha dini watoto wa kiislam wanashangaa shangaa tu kisa hakuna mwalimu wa dini (hakuna mwalimu mwislamu)

Basi nikaamua kuwakusanya nikawapigisha pindi mbona ilienda kuwa gumzo makwao... nakumbuka walikuwa wanakuja mpaka wanakijiji kwenye kipindi cha dini na mpaka naondoka hawakuamini kama kweli kilichotokea ndicho

3.Wengine nao wakanichokoza lugha fulani kujibu mashambulizi mbona wakaingia mitini wenyewe na mpaka leo hawanimalizi
 
Salute mkuu
 
Ikitokea mkawa business partners na kuwa watu wa karibu, inaonyesha baadaye mtarudi kwenye mahusiano yale yale mliyofanikiwa kuyajenga siku ya kwanza mlipokutana. First good impression on the first day of meeting huwa ni ya muhimu sana kisaikolojia kwa mtu ambaye hakufahamu. Ukiharibu siku ya kwanza the chances ni kwamba utaendelea kuharibu tu siku zote zitakazofuata mbele yako, kitu ambacho kinaweza kupelekea kukosa hata madili mazuri ya biashara.
 
asalaaam aleikum ya habib
 
Mi nakumbuka ile ya Uswisi iliyomuhusu pia Oprah
 
Always wadada huwa wanapenda sana wakaka wanaovaa na kuwa na magari wakijua ndio wenye hela
Kwangu nilikuwaga chuo nilikuwa na vaa hovyo na sijawahi panda piki piki for all 4 years hivyo kila demu alikuwa ananichukulia easy mixer kudharauliana but mwisho wa siku wanakuja gundua nilikuwa na miliki biashara ya maana baada ya baba wa demu moja kukopa kwenye biashara yangu
Ni story ndefu but niishie hapo kuwa baba wa huyo manzi alimwambia huyu mwamba na mheshimu sana ananisaidia biashara zinazopelekea kukulipia ada ili kuwa last semistar walijigonga mamanzi kwangu but huwa sinaga hisia nao
 
Walipishana na gari ya mshahara hivihivii😅
 
Kweli kabisa usimdharau mtu usiye mjua.

Hata mm imenitokea hiyo kuna Mkaka mmoja mtaan kwetu ukweli sikuwahi kumuelewa kabisa. Kwanza nilikuwa namuona kama hajatimia kuitwa wa kiume kwa njisi tu alivyo alivyo. Hata salamu tulikuwa hatuna.

Kuna siku moja nilikuwa nimekaa nje kwetu na shoga angu akapita huyu kaka. Nikajikuta namwambia best yng "yaani katika watu nisiowaelewa hapa duniani huyu kaka wa kwanza. " akaniuliza kwa nini, nikamwambia basi tu simuelewi katika kila kitu.

Zikapita siku za kutosha. Siku moja nimetoka zangu mishe najiandaa kuingia bafuni mara shoga angu huyoo ananiita. Nikamwambia nisubiri ndani nakuja. Niliporudi ile naingia tu kuniona akaanza kucheka hatari. namuuliza wacheka nini wewe. akajibu yule kaka usiyemuelewa hapa duniani kanipa zawadi hii nikuletee. Anaomba kukutana na ww. Looh nikamwambia muongo ww naanzaje kwenda kumsikiliza na kwa nn umepokea zawadi hii ikiwa unajua kila kitu. akasema ndio hivyo nenda ukamsikilize uku anacheka hatari.

Kweli sikwenda siku hiyo. Ilipita kama wiki mbili hivi akuacha kunitumia zawadi. Ile kitu ikanifanya niwe namfikiria sana. Nikampa nafasi nikaenda kumsikiliza. Akamwaga sera zake pale nikazipokea taratibu nikaanza nikazifanyia kazi. Nakumbuka kauli yake ya kwanza alisema "Nakupenda, sitaki kujua kuhusu mahusiano yako uliyonayo ingawa ninchojua mm hujaolewa, so nipe nafasi alafu utachagua ww yupi anakufaa." Hakuwa na mengi

Looh mpaka leo siamini nimezama mwenzenu. Alivyo kwa nje na ndani tofauti kabisa. Na sasa ndoa imetangazwa.
Kweli usimdharau mtu usiye mjua
 
Unexpected journey [emoji179]
 
kwa hiyo dudu la jamaa limekudatisha mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…