Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

adi Oprah Winfrey ilishamkuta.. muuzaji alikataa kumuonesha pochi ya beii akamwambia hataweza kuiafford
 
Juzi juzi nilienda kumlipa Binti yangu ada kwenye shule fulani ya watoto wa kike kufika office ya Mhasibu nikamkuta mama flani namslimia akanishusha tu akaendelea na mambo yake. Nikamsalimia mara ya pili ndo akanijibu "nimeshakusikia" nikaamua kusubiri alipomaliza mambo yake ndo akaniita "haya unasemaje?" Nikamwambia nimekuja kumlipia ada ya Binti yangu anayesoma hapa
Akashtuka "ooh kumbe sikujua"
Nikatoa bank slip ya 3.5m ambayo ni ada ya mwaka mzima Pamoja na slip ya pili yenye laki 5 ya michango
Alipoona hivyo akaanza kujichekesha mpk akawaagiza wanafunzi wamwite Binti yangu amsalimie .
 

Hii nimeipenda Mtu akijifanya keki mteme tu
 
Kikubwa ni yupo ikulu
 
Askari gani hao wa Suma au
 
Miaka fulani nilikuwa na likizo ndefu ya chuo basi nikaona nisikae bure nikafungua kamgahawa katikati ya mji. Nilikuwa nauza bites zote, juice fresh na matunda fresh.

Nilikuwa karibu na ofisi nyingi na banks. Basi nikawa napata oda ya kupeleka bites na maziwa asubuhi pamoja na matunda.

Dada mmoja staff wa pale CRBD aliweka oda ya matunda kila ikifika saa 6 mchana, ikawa siku nyingine ukipeleka anakwambia umechelewa nishakula kwingine, au leo sili basi narudi nayo. Au ukienda siku nyingine anakuangalia tuu hapokei matunda unabaki umesimama kama sanamu na matunda yako.

Siku moja nikaenda nikiwa na shida ya kufungua joint acc, kufika kwake hata sijamsalimia kanijibu leo sitaki matunda. Nikamwambia nina shida nyingine kabla sijaeleza akajibu tena "hapa tunasikiliza za kiofisi tuu hivyo ondoka". Sijui alijua nataka msaada wa hela au vipi.

Ikabidi niwe mpole maana alikuwa peke yake kwa muda ule customer service pale. Nikamweleza nahitaji fomu kufungua joint acc na mama yangu. Akachukua fomu akanipa akaniuliza "utaweza kusoma na kuzijaza kweli na mama yako??" Nikamjibu ndio. Akaniambia viambatanisho vinavyohitajika nikaondoka kesho nirudishe fomu.

Kesho yake nimeenda na mama, kufika pale akamkaribisha akakae kwenye kiti mimi akaniambia kasubiri pale yaani pembeni, ndio mama akamwambia nimekuja na binti yangu tunafungua joint acc, kwanza alistuka akamuuliza ni mwanao kumbe mama sikujua. Akaishiwa pozi.

Basi katika kupiga stori na bimkubwa akamwambia sikujua kama una binti mkubwa, bimkubwa akamwambia mara nyingi hayupo nyumbani kwasasa yupo likizo anasoma masters huko mkoa X. Alishangaa kwa nguvu Masters?? Aliniangalia sana. Miaka hiyo bimkubwa na mzee walikuwa wafanyabiashara wakubwa sana mkoani na chapaa zipo za kutosha wanajulikana kila kona. Bank pale walikuwa wanajulikana sana.
Enzi hizo bimkubwa na mzee CRDB wana zile VisaGold so wanahudumiwa kishua....kwahiyo dada akajua huyu sio kwamba anauza matunda kwa dhiki

Dada alikosa raha sana hadi muda anatoa copies akaniambia dada kakae kwenye kiti [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] toka siku hiyo alianza na kunisalimia na kunichangamkia. Mimi wala sikumwonyesha tofauti nikaendelea kumpelekea matunda.
 
Vipi sasa kuhusu Ph.D mkuu,
Umeshaipiga au bado kidogo?
 
[emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Sikuhizi wana ku jugde Kwa SIMU unayo tumia
 
Inaonekana una passion sana na mambo ya misosi bila shaka wewe ni mtaalamu wa maskolodinyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…