Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Kuna siku niliazima gari nikaenda pale best bite kuchukua zaga.

Sasa nilivyoingia ndani nikakutana na pisi tatu za kwenda zinatoka ndani, nikazipa hi zikachuna full kunipandisha na kunishusha, nikaona POA tu nikafuata kilichonipeleka.

Sasa ile natoka nje nikazikuta ziko bize zinajisnap kwenye gari niliyokua nayo, hiiiiiiiiii bagoshaaa, mbona walikoma kunijua.

Nilianzisha zogo la maana makusudi kabisa, nikaita mpaka uongozi wa pale nikawaambia wawaambie wateja wao wafute picha zote walizopiga gari yangu otherwise niite Askari pale obey waniambie Wana lengo gani na picha za mkwaju wangu?
Aisee
 
Kuna siku nipo nilikuwa sina kazi nyingi ofisini nikatoka nje hivi nikamweleza PA wangu nipo nje nachukua Juice Fresh kutoka nje kuna gari limeingia Parking kwa speed kidogo liniingie miguuni jamaa hawakuwa na hekima walinitusi Mpuuzi wewe...nimerudi Ofisini naambiwa na PA wangu Meneja kuna wageni wako nikawaruhusu waingie nakuta wale jamaa walionitusi nikawakaribisha na sentensi fupi 'Karibu ABSA' wanageuzageuza nyuso zao hawajui waanze vipi.
Wangari Maathai 😂😂😂
 
Dah mkuu umenikumbusha mbali sana, nlikua na mwanangu nae ana mshkaji wake flan mtumishi wa halmashauri, siku moja mwana kaniambia tukutane chako, mitaa flan Dom, akaja na yule mwana, tukapiga misosi na story wakapotea, kumbe jamaa aliona mimi mrugaruga flan hivi sistahiki kamapani yao. Akamchana mwana kwa text kwamba amsindikize maeneo wakasepa ili kunikataa! Njiani akamwambia yule mpuuz anakuaje rafiki yako? Jamaa akamwambia mwana anapiga PhD afu ana geto mbili mjini hapa...heshima tangu siku hiyo
Chai.
 
we nakuona unataka kunifundisha tabia mbaya wewe..
Hahaha, unajua wabongo hizi hoteli za 5 Star tunakosea sana ukifika unaanza chips kuku mala pizza. Ww wasumbue naomba glas ya juice alafu baada ya dk 40 niletee fungu la mchicha usiungie kitunguu weka karot tu na ndizi moja ya kuchemsha pembeni. Ukishatoa maelekezo unawasha data unaanza kuchati huku unasubiri washkaji waje.
 
nakumbuka kuna kidemu kilikua kinanidharau sana enzi hizo bush, basi nilivyomaliza shule pale kijijini nikaondoka kwenda Dar kwa kaza ikapitwa miaka 4 nikasikia kapewa mimba na aliyempa mimba nimshikaji niliesoma naye na alipewa mimba akiwa bado anasoma, basi kwakuwa jamaa nayeye alikua na ndg Dar ikabidi wakimbilie Dar es salaam kwa ndg wa mshikaji baada ya mwaka mmoja kupita ndipo wakasahauliwa waende hospital kwa kwa ajili ya kufanya uzazi wa mpaka na hospital ilikua maeneo ninayoishi basi mshikaji ndg yake akamwambia nenda utamkuta rafiki yako uliesoma naye akuelekeze bwana weee

si wakaja mpaka home yule demu hukuamin kama ndiyo mimi aliekuwa ananidharau kule bush basi nikawasindikiza mpaka hospitalini kisha tukarudi nikawapeleka mpaka stendi yule demu nafsi ilimsuta sana mpaka aliamua kunitumia sms akisema kweli nimeamini usimdharau mtu ktk hii Dunia nilikuwa nakuchukulia poa poa kijijini leo unaijua mitaa ya Dar kiasi hiki na umetupeleka mpaka hospitali

aliishia kusema nisamehe, nami sikumjibu maskini.
Kuijua mitaa ya dar tu ndio unajisifia?
 
Kuijua mitaa ya dar tu ndio unajisifia?
Nilijua tuu watu kama nyie hamkosi maeneo haya

Ila elewa dhamira ya uzi mkuu, uzi unasema tulio wahi kuchukuliwa powa powa sasa na mimi huyo demu alinichukulia powa kule bush kana kwamba ckuwa na umuhimu ktk hii Dunia pia mpaka yeye mwenyewe alidiriki kunitumia sms akíkiri makosa yake unafikiri kuna nini hapo kama siyo nafsi ilimsuta.
 
Mi kuna manzi mmoja katika harakat za kusaka tonge ikatokea tuna mawasiliano na yalikua strictly kikaz zaid cz wao walikua na ma distributor wa products flan hiv za security na mi nikawa moja ya wateja wao.
Sikua namjua kiundani na mawasiliano yetu yalikua nadra sana ile kikaz kaz na mazoea kwa mbaaaali.Status zake watsap na view na yy zangu anaziona.Kwakua napenda muzik basi alikua ananikosha kwa baadh ya vi clip anavyotupia mara moja moja sana navi comment.
Siku moja nikawa sina ishu kabisa job na niko bored na bahat mbaya sana akaweka status ilonivutia basi kama kawaida nika comment (yy zangu huwa ha respond japo hizo mara moja moja sana naziweka) basi aka respond finaly tukaanza kuchat.
Tukachat mara ujinga ukaingia humo ndani na u cant believe siku hiyo hiyo nikamgonga mzigo vizuuri tu kiroho safi.

SASA iko hiv,
Ofcz mm nilimchukulia poa kumbe hayuko hivyo.Anajimilikia ka usafir kake mwenyewe kazur tu (mi zangu daladala so mpaka nampanga akajaa nikajua na yy wa level zangu 😁😁😁). Mida tunakutana ndio nikalijua hilo,nikapiga mzigo na kwa aibu nikamshikisha 40k ila manka yule akazikataa kata kata.Nikaona oohoh leo nimepima vibaya kumbe na yy akanichukulia mambo safi hela ninazo asijue mimi ni bahili kishenzii 😂.
Sikua na mpango na game tena na yy akanitengenezea mazingira next week yake nikagonga tena.Ohoooh sijui alijua na leo nitapanda dau tena!!!!???. WAPII.
kesho yake akapiga mzinga nikachomoa..
Week ijayo yake akani set tena Shi 100 mfukon sina.
Kwa mara nyingine akani text "leo ninw hamu kitimoto, ningepata kilo 1 jion yangu ingeisha freshi." Nikaona isiwe kesi nikamtumia 5000- elfu 5 😊 bila ya kutoleo.AKANIPOTEZEA MAZIMA hata message za kikazi hajibu tenaa..

Baadae saaaana huko akajaga ni text, HUENDANI KABISA NA UNAVYOONEKANA. WW BAHILI SANA.

Kwa kifupi alinichukulia nina hela kumbe njaa tu 😆😆😆😆😆
Nimefurah 😂😂 Ila pia nimejifunza ,girls love to be cheated...
 
Nlimwagizia mtu mzigo flan, wakati wa kufanyiwa delivery kwa maagizo yake bila kunihusiha mimi bahati mbaya mzigo wake ukapata shida, alivoniita akademand mzigo mpya bila kujal kua sikua na dhamna nao tena baada ya yeye kutoa maagizo apelekewe.
Siku nmekutana nae akiwa na mzee wake walinidharau sana mzee alitamka wazi waz huyu hio hela ataitoa wapi? Maana ilikua kama 18m
Mzee akasema huyu awekwe ndan ndg zake watafute io hela tena nataka anilipe 20m
Nliumia sana, nkamwambia mzee bas nilipe harama ya mzigo mzee alikataa katu katu af n swala 5.
Nikamwambia nipe miez 2-3 nikulipe akakataa katu katu akanambia labda ndan ya mwezi unilipe 19 then io 1 unilipe baada ya miez miwil nkamwambia sawa
Baada ya mwez mzee alijikoki akijua ananiweka ndani, nilimpa hela yake ikabak 1
Siku inakaribia a week before mtt wake akanichek sasa ile 1 vp tumalizane niliumia sana maana walinilipisha kitu ambacho wao ndo chanzo cha mzigo kutokuwafikia, hawakua under standable, walinidharau sana na maneno ya kebehi
All in all nilimalizana nao nikasepa
But sitasahau
 
Aisee pole sana mkuu.. So mzigo uliopotea ikawa ni hasaraa yakoo...???
 
Mleta mada niliposoma kichwa cha habari cha uzi wako nilijisemea Huyu atakuwa umeandika utopolo lakini niliposoma andiko lako mpaka mwisho nikakuta lina mashiko na watu wanachangia kwa wingi nimejifunza kitu usikijaji kitabu kwa muenekano wa kava lake
 
Mada hii toka imepostiwa huwa natamani kuchangia but ubize na uvivu wa kuandika vinanishinda Nguvu.

Ngoja leo nitoe kisa kimoja katika visa vyangu vingi vya maisha yangu.

Mwaka 2008 nikimuuguza mzee wangu katika hospital moja kigoma ipo sehem mmoja panaitwa Manyovu ile hospital kama sijasahau itakuwa inaitwa Nyamasovu.

Nikiwa kijana mdogo katika watu walokuwa wakiwauguza na kusimamia wagonjwa wao, Manessi walinichukulia poa sana. Mda mwingne walinifokea kipindi wananipa maelekezo.

Namkumbuka nessi mmoja mdogo kama wa miaka 20-22 hivi. Mzee alikuwa kafanyiwa sajari na alikuwa kawekewa mipira yakutolea uchafu mwilini hivyo kuna muda ilikuwa ikijaa naenda kumwita yule nessi aje atoe na kum badirishia mfuko wa uchafu , alikuwa ananitizama kwa dharau sana. Kuna siku akanitamkia kabisa " we kaka mbona msumbufu? Nikajibu nessi me naangalia uhai wa mzee wangu akanambia Kwani baba yako ndo atakuwa wa kwanza kufa, ? Ivi mnahisi Manessi tunafurahia kuchezea uchafu wa wagonjwa wenu? Ungesoma nawewe ukawa nessi ukaona tunachokifaidi sisi. " duh! Kiukweli niliumia sana.

Kwa uwezo wa MUNGU mzee akapona , siku ninaendea ruhusa ili tumrudishe nyumbani kale kanessi kakaniambia kwa kejeli "Baba wa Taifa amepona " nikajifanya sijaelewa kakaongeza et "unahangaika utafkiri unamuuguza Yesu " kipindi hicho nilkuwa bado nasoma ko nikawa napretend ustaarabu ili nisiharibu cv .

Baada ya miaka kupita nikiwa nishasahau siku moja nipo kwenye ndege pakawa kuna mdada siti ya mbele yangu (kama siti ya3 toka kwangu upande wa kushoto) ananiangalia sana. Yani kila dakika anageuka tukikutabisha macho me naangalia pembeni nikiinua macho tena nakuta ananiangalia tena. Nikahisi labda ni x wangu flan iv katika ma x zangu. Tulivyoshuka mw/ Julius Nyerere watu wakaanza kushuka nikawa nimeinamia simu naiwasha baada yakuizima kipindi ndege inaanza safari nikainuka ile navua mkanda nainuka kuotoa begi juu nakuta watu wengi washashuka kabaki dada mmoja tu na wahudumu wa ndege. Nikashuka chini ile nipo kwenye ngazi akanigusa mtu kwa nyuma nikageuka sikuwa namkumbuka akajitambulisha kumbe ndo yule nessi. Kwakuwa sikuwa mtu wakuweka kinyongo nikamchangamkia tukatoka nje nikawa nasubiri Dogo aniijie na gari la home kumbe yeye hana usafiri anawaza tax nikamkazia kama sioni shida yake akajishusha mwenyewe akaomba lift nikamchukua hadi tunafika ubungo hajasema anaenda wapi kumbe alijiendeleza kielim ko anasoma Md muhimbili ila dsm hana mwenyeji ko nikampeleka napoishi akalala (mana ilikuwa ishakuwa usiku) kesho asbuhi me nayeye hatukuweza kuonana mana nilikuwa nina mishe zangu zilizonileta mjini ko alivyoamka akaoga akapata chai dogo akampeleka chuoni. Aisee alinipigia simu usiku wake eti ndo ananiuliza mzee anaendeleaje. Then sikutaka tuyaongelee ya kipindi kile ila alinisihi sana nimsamehe na kuanzia siku hiyo heshima mpaka sasa
Dah nimefedheheka sana kwa uliyotendewa na huyo baradhuli namuombea afe mapema hata sasa ikiwezekana
 
Dharau na kibri ni ugonjwa kama yalivyo magonjwa mengine na mbaya zaidi wengi wetu hatujui ukubwa wa maradhi haya na ndio maana ni vigumu pia kuyatafutia tiba.

Mtu anaweza kudharau kwa sababu na bila sababu, inategemea na ukubwa wa tatizo.

Huu ni ugonjwa mbaya watu wanatakiwa wajiepushe nao kama Corona.

Upande wa pili, kuna watu wanalazimisha wadharaulike. Mtu mzima mwenye akili timamu ukikojoa mbele ya watoto wako unataraji watoto hao wakuheshimu? Never! Nani wa kulaumiwa? Ni mdharauliwaji na si mdharadhauji.
Mtu mdomo wake hauchagui neno eidha iwe kwa mkubwa au mdogo, bado unataraji heshima tu? Hapana!

Na jingine ni kwamba, watu wana 'inferiority complex', hii inawatesa wengi kwa kudhani kuwa wamedharauliwa kwa vile jinsi walivyo. Mtu anaweza akakusalimia kipindi ambacho akili yako imehama hivyo usiweze kuisikia salam yake na kushindwa kuitikia, atalalamika "jamaa kanidharau kwa vile mimi mfupi" kumbe tatizo ni jambo lingine na si ufupi.
Mwingine hana kawaida ya kusalimia no matter who you are, kwa asiyemjua atasema jamaa hanisalimii kwa sababu 'ananidharau' kumbe hata baba yake anayempa kula nyumbani hajamsalimia pia.

*Watu wanao jiamini, wana malalamiko machache ya kudharauliwa kuliko wale wasio jiamini!*

KUPANGA NI KUCHAGUA KWAHIYO KAZI KWENU WAUNGWANA.

Sent from my SM-N910W8 using JamiiForums mobile app
 
Mada hii toka imepostiwa huwa natamani kuchangia but ubize na uvivu wa kuandika vinanishinda Nguvu.

Ngoja leo nitoe kisa kimoja katika visa vyangu vingi vya maisha yangu.

Mwaka 2008 nikimuuguza mzee wangu katika hospital moja kigoma ipo sehem mmoja panaitwa Manyovu ile hospital kama sijasahau itakuwa inaitwa Nyamasovu.

Nikiwa kijana mdogo katika watu walokuwa wakiwauguza na kusimamia wagonjwa wao, Manessi walinichukulia poa sana. Mda mwingne walinifokea kipindi wananipa maelekezo.

Namkumbuka nessi mmoja mdogo kama wa miaka 20-22 hivi. Mzee alikuwa kafanyiwa sajari na alikuwa kawekewa mipira yakutolea uchafu mwilini hivyo kuna muda ilikuwa ikijaa naenda kumwita yule nessi aje atoe na kum badirishia mfuko wa uchafu , alikuwa ananitizama kwa dharau sana. Kuna siku akanitamkia kabisa " we kaka mbona msumbufu? Nikajibu nessi me naangalia uhai wa mzee wangu akanambia Kwani baba yako ndo atakuwa wa kwanza kufa, ? Ivi mnahisi Manessi tunafurahia kuchezea uchafu wa wagonjwa wenu? Ungesoma nawewe ukawa nessi ukaona tunachokifaidi sisi. " duh! Kiukweli niliumia sana.

Kwa uwezo wa MUNGU mzee akapona , siku ninaendea ruhusa ili tumrudishe nyumbani kale kanessi kakaniambia kwa kejeli "Baba wa Taifa amepona " nikajifanya sijaelewa kakaongeza et "unahangaika utafkiri unamuuguza Yesu " kipindi hicho nilkuwa bado nasoma ko nikawa napretend ustaarabu ili nisiharibu cv .

Baada ya miaka kupita nikiwa nishasahau siku moja nipo kwenye ndege pakawa kuna mdada siti ya mbele yangu (kama siti ya3 toka kwangu upande wa kushoto) ananiangalia sana. Yani kila dakika anageuka tukikutabisha macho me naangalia pembeni nikiinua macho tena nakuta ananiangalia tena. Nikahisi labda ni x wangu flan iv katika ma x zangu. Tulivyoshuka mw/ Julius Nyerere watu wakaanza kushuka nikawa nimeinamia simu naiwasha baada yakuizima kipindi ndege inaanza safari nikainuka ile navua mkanda nainuka kuotoa begi juu nakuta watu wengi washashuka kabaki dada mmoja tu na wahudumu wa ndege. Nikashuka chini ile nipo kwenye ngazi akanigusa mtu kwa nyuma nikageuka sikuwa namkumbuka akajitambulisha kumbe ndo yule nessi. Kwakuwa sikuwa mtu wakuweka kinyongo nikamchangamkia tukatoka nje nikawa nasubiri Dogo aniijie na gari la home kumbe yeye hana usafiri anawaza tax nikamkazia kama sioni shida yake akajishusha mwenyewe akaomba lift nikamchukua hadi tunafika ubungo hajasema anaenda wapi kumbe alijiendeleza kielim ko anasoma Md muhimbili ila dsm hana mwenyeji ko nikampeleka napoishi akalala (mana ilikuwa ishakuwa usiku) kesho asbuhi me nayeye hatukuweza kuonana mana nilikuwa nina mishe zangu zilizonileta mjini ko alivyoamka akaoga akapata chai dogo akampeleka chuoni. Aisee alinipigia simu usiku wake eti ndo ananiuliza mzee anaendeleaje. Then sikutaka tuyaongelee ya kipindi kile ila alinisihi sana nimsamehe na kuanzia siku hiyo heshima mpaka sasa
Kuna watu wanafanya kufuru kwenye matatizo ya wenzao mpaka unajiuliza hivi hawa kesho yao wanaijua vizuri eeh!!! Pole sana maana nahisi maumivu uliyopata
 
Back
Top Bottom