Designer_3434
JF-Expert Member
- Dec 4, 2015
- 4,901
- 3,941
Kweli kabisa usimdharau mtu usiye mjua.
Hata mm imenitokea hiyo kuna Mkaka mmoja mtaan kwetu ukweli sikuwahi kumuelewa kabisa. Kwanza nilikuwa namuona kama hajatimia kuitwa wa kiume kwa njisi tu alivyo alivyo. Hata salamu tulikuwa hatuna.
Kuna siku moja nilikuwa nimekaa nje kwetu na shoga angu akapita huyu kaka. Nikajikuta namwambia best yng "yaani katika watu nisiowaelewa hapa duniani huyu kaka wa kwanza. " akaniuliza kwa nini, nikamwambia basi tu simuelewi katika kila kitu.
Zikapita siku za kutosha. Siku moja nimetoka zangu mishe najiandaa kuingia bafuni mara shoga angu huyoo ananiita. Nikamwambia nisubiri ndani nakuja. Niliporudi ile naingia tu kuniona akaanza kucheka hatari. namuuliza wacheka nini wewe. akajibu yule kaka usiyemuelewa hapa duniani kanipa zawadi hii nikuletee. Anaomba kukutana na ww. Looh nikamwambia muongo ww naanzaje kwenda kumsikiliza na kwa nn umepokea zawadi hii ikiwa unajua kila kitu. akasema ndio hivyo nenda ukamsikilize uku anacheka hatari.
Kweli sikwenda siku hiyo. Ilipita kama wiki mbili hivi akuacha kunitumia zawadi. Ile kitu ikanifanya niwe namfikiria sana. Nikampa nafasi nikaenda kumsikiliza. Akamwaga sera zake pale nikazipokea taratibu nikaanza nikazifanyia kazi. Nakumbuka kauli yake ya kwanza alisema "Nakupenda, sitaki kujua kuhusu mahusiano yako uliyonayo ingawa ninchojua mm hujaolewa, so nipe nafasi alafu utachagua ww yupi anakufaa." Hakuwa na mengi
Looh mpaka leo siamini nimezama mwenzenu. Alivyo kwa nje na ndani tofauti kabisa. Na sasa ndoa imetangazwa.
Kweli usimdharau mtu usiye mjua
[emoji23]