Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Hii ishanitokea wakati niko primary nilikuwa kichwa kuwa namba 1,2,3 kitu cha kawaida nilikuwa maarufu kuanzia shule nnayosoma mpaka shule za jirani so cku moja nkakutana na kichwa wa shule ya jirani yy alikuwa hanijui alikuwa ananichukulia poa kuna mwana akaniita jina langu yule kichwa akackia hakuamini kama ndo mm

Nyingine katika mishe zangu za udalali kuna mwarabu koko mmoja alikuwa anahitaji kiwanja cha kununua so akanipa kazi ya kumtafutia but nilipokutana alikuwa mtu wa madharau ghafla cmu yangu ikaita wakati tunaongea akawa anajisachi akijua cm yake kumbe ni cm yangu Samsung A 12 kipindi hicho ndo znatoka na yy alikuwa anayo kama hyo alinunua Dubai alijickia mnyonge kuona mchizi dalali tena Chanika anamiliki cm kama yake
 
Mimi huwa ni ngumu mtu kunitambua kama najua kitu au niko interested kwenye jambo fulani kwasababu ni mtu nisiyependa show off (kujionesha). Nitaelezea machache katika engo tofautitofauti

Madrasa
Enzi za udogo (ujana) nikiwa madrasa jamaa katika kusoma Quran akakosea halafu yeye ndo ana jukumu la kutufundisha basi alipotoka tu yule mfundishwaji nikamrekebisha kistaarabu kabisa jamaa alistaajabu sana ilibidi amuite yule aliyekuwa akifundishwa arudie upya. Ebana wee tangu hapo nikawa nimechokoza moto vijana (maustadh) karibia wote wakawa wakitaka kwenda kusoma (kuaridhi) kwa mwalimu lazima waanzie kwangu kwanza ili nikague makosa yao na alhamdulillah kwa uwezo wa Allah nilikuwa sibahatishi ingawa sura hizo sikuwa nimezifikia bado

Cherehani
Mzee alikuwa anapokea tenda fulani ya kushona halafu anampa kaka sasa ikafika kipindi kaka hayupo yule mtoa tenda akaambiwa safari hii ile kazi yule uliyemzoea hayupo utafanya na huyu (yaani Mimi) jamaa akawa haniamini tena akasema kabisa "huyu dogo hivi aisee ataweza?" Mzee akamwambia wewe usijali huku Mzee nae akiwa na mashaka kwenye spidi yangu basi nilikamatia ile kazi kwa ubora wa hali ya juu na ni ndani ya muda. Mbona walinyoosha mikono na mpaka kesho yule jamaa ananiita fundi

Sensa
Nimeitwa nikarekebishe kishikwambi cha karani, maudhui kaniambia niwakute ofisi ya kijiji basi nikachukua boda fasta. Kufika nakuta mtendaji anaongea na yule maudhui nawapa hai makarani wanaitikia, nawasogelea mtendaji nampa salamu akageuka tu kuniangalia kisha akaendelea kuongea mazungumzo yake nikaachana nae maana huwa sirudiagi salamu muda huo maudhui anafanya kama anandoka kunielekea eti yule mtendaji anamzuia "bwana aachana nao hao angalia huku bado sijamaliza mimi unaenda wapi?" (Akili yake akijua mimi na yule bodaboda labda ni wageni wake katika ofisi yake). Basi yule maudhui akamwambia huyu anahitajika kwingine akiondoka ndo basi tena basi akaambiwa huyu ndo IT wetu wa kata (kama unavyojua tena kwenye sensa watu tulibandikwa matitle makubwamakubwa wakati hatuna lolote- tulitambulika kama maafisa wa sensa ambapo karani aliitwa tu kawaida afisa wa sensa maudhui aliitwa afisa maudhui, mtu wa tehama aliitwa IT). Basi yule mdada aliduwaa yaani akapoa hadi nikawa namuonea huruma akiniangalia hanimalizi na Mimi kwa sifa nikashuhulikia kilichonipeleka kisha ndefu najidai nina haraka

Muvi
Imezoeleka wa shule za kata hatujui ung'eng'e sasa bana eti tunaangalia muvi enzi hizo ndo nimetoka form four jamaa akaniambia hii muvi hutaielewa maana haijatafsiriwa kama muvi zenu mlizozoea basi nikamwambia kama wanaandika (subtitles) basi nitajikaza akaniambia hakuna hiyo kitu. Kucheki ati jamaa akaanza kunishereheshea baadhi ya vipande sasa ikawa kamba nyingi ikabidi nimtolee uvivu mara paap! Mimi ndo namsaidia kumtafsiria tena

Misikitini
Kwa wale wanaoenda kuswali misikitini mtanielewa zaidi. Tumehamia sehemu kwahiyo ikabidi nihame hata msikiti niende ulio karibia na kwetu. Sasa kawaida yangu (kawaida yetu vijana wa madrasa) huwa hatujirembirembi katika maswala ya dini basi swala ikikimiwa tu tayari nipo beside ya mkimuji mbele kabisa. Basi siku hiyo ustadh mkimuji akanitoa ananambia nikae nyuma hapo mbele niwaachie mashekhe (wakati kiuhalisia nikiwaangalia ni mashekhe umri yaani wazee na sio mashekhe kwa elimu). Mungu si Athumani bwana siku hiyo tumechelewa swala kidogo na yeye akiwemo basi mmoja akasema Fulani tuswalishe bana (akinitaja Mimi) basi tangu hapo yule jamaa akawa akiniangalia tu hanimalizi

Wakati nipo chuoni tena (ualimu) msikiti mmoja jamaa mmoja nae alichelewa nikamswalisha swala ya sauti basi kutoka akaniambia "mbona mtu akikuangalia hawezi kuamini kama ni wewe uliyeswalisha pale? Yaani uvaaji wako na namna ulivyo me nkadhani wewe ni mkristu."

Huku kazini nimeswali nao karibia mwaka hawajanigundua sasa kilichokuja kuniponza ni somo la Dini. Ikabidi nijidhihirishe tu lakini na wao walidhani ni muislamu jina tu hata majina yangu walidhani ni majina tu ya mchongo
Hata sio Sifa bali vitu vingine ni aibu kusimulia, yaani muislam wajigamba kwa kutukufahamika dini yako!! Aibu gani hii
 
Mimi kuna jamaa tumesoma wote form 1&2 tulikuwa washkaji maana ndo tulikuwa tunaongoza class
Nikafukuzwa so 3&4 tulikuwa tunakutana likizo tu
Baada tukapotezana Ila me nilikuwa napata data zake alimaliza degree ya mambo ya afya akaingiza jeshi then akapelekwa mondul kusomea sijui vyeo then akapangwa mikoan huko
2020 sm inaita ni jamaa " Flan vip? Za siku niomeambiwa uliacha kazi ya ualim now unapiga umachinga dar? Tuonane basi ndg" ni kweli niliachaga ualim nikajichanganya kariakoo kabla sijatoboa kibiashara ambayo hakuwa anajua kuwa nilitoboa tena kwa kiwango kikubwa
Basi tukakutana Mliman me ndo nilitangulia pale Grano
Jamaa akaja "agiza chochote ntalipa kaka " mbwembwe nyingi
Me na mwili mdogo halaf kwenye uvaaji me ni 0% so ngumu sana mtu kujua huyu yuko vzr au la!
Tukiwa pale dem wangu akaniambia nimfate kazin kumrudisha home alkkuwa mjamzito nikamwambia mshkaji akajibu " haina shida na usafir kaka twende tutamchukua tu nishanunua gari siku hizi mambo yangu fresh "
Nikakubali tukatoka nikamwambia tupite nichukue langu tuongozane ndo anaanza kushangaa " kwan una gari? Machinga ana gari mura au nimedanganywa!?"
Tumefika mzee anaona BIMA imepaki nafungua namwambia twende na hii tukirud tutapitia yako
Jamaa alikosa aman sikujua why ila alikosa aman kabisa
Tumemaliza kule namrudisha Mliman kumbe ana Swift old mole dah jamaa tangu pale alikata mawasiliano mpk leo tunaview tu status

Yan kuna watu sio wachawi lkn matendo yao km wachaw hv wanapenda kuona wao ndio wako juu tu kuliko wenzao au watu wanaowazunguka...huyo jamaa ako umemkata vibe viby san alijua atakukuta choka mbaya uanze kumlilia shida na kumnyenyekea[emoji38]
 
Mbona kama nakujua
 
Enzi hizo bimkubwa na mzee CRDB wana zile VisaGold so wanahudumiwa kishua....kwahiyo dada akajua huyu sio kwamba anauza matunda kwa dhiki. Mimi huwa simdharau mtu nisiyemjua kabisa
Kuna katabia haswa wakikuona umepoa kumdharau mtu yaani ni ugonjwa wa taifa huo sijui shida nini

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mimi kuna jamaa tumesoma wote form 1&2 tulikuwa washkaji maana ndo tulikuwa tunaongoza class
Nikafukuzwa so 3&4 tulikuwa tunakutana likizo tu
Baada tukapotezana Ila me nilikuwa napata data zake alimaliza degree ya mambo ya afya akaingiza jeshi then akapelekwa mondul kusomea sijui vyeo then akapangwa mikoan huko
2020 sm inaita ni jamaa " Flan vip? Za siku niomeambiwa uliacha kazi ya ualim now unapiga umachinga dar? Tuonane basi ndg" ni kweli niliachaga ualim nikajichanganya kariakoo kabla sijatoboa kibiashara ambayo hakuwa anajua kuwa nilitoboa tena kwa kiwango kikubwa
Basi tukakutana Mliman me ndo nilitangulia pale Grano
Jamaa akaja "agiza chochote ntalipa kaka " mbwembwe nyingi
Me na mwili mdogo halaf kwenye uvaaji me ni 0% so ngumu sana mtu kujua huyu yuko vzr au la!
Tukiwa pale dem wangu akaniambia nimfate kazin kumrudisha home alkkuwa mjamzito nikamwambia mshkaji akajibu " haina shida na usafir kaka twende tutamchukua tu nishanunua gari siku hizi mambo yangu fresh "
Nikakubali tukatoka nikamwambia tupite nichukue langu tuongozane ndo anaanza kushangaa " kwan una gari? Machinga ana gari mura au nimedanganywa!?"
Tumefika mzee anaona BIMA imepaki nafungua namwambia twende na hii tukirud tutapitia yako
Jamaa alikosa aman sikujua why ila alikosa aman kabisa
Tumemaliza kule namrudisha Mliman kumbe ana Swift old mole dah jamaa tangu pale alikata mawasiliano mpk leo tunaview tu status
Msenge san huyo
 
Miaka fulani nilikuwa na likizo ndefu ya chuo basi nikaona nisikae bure nikafungua kamgahawa katikati ya mji. Nilikuwa nauza bites zote, juice fresh na matunda fresh.

Nilikuwa karibu na ofisi nyingi na banks. Basi nikawa napata oda ya kupeleka bites na maziwa asubuhi pamoja na matunda.

Dada mmoja staff wa pale CRBD aliweka oda ya matunda kila ikifika saa 6 mchana, ikawa siku nyingine ukipeleka anakwambia umechelewa nishakula kwingine, au leo sili basi narudi nayo. Au ukienda siku nyingine anakuangalia tuu hapokei matunda unabaki umesimama kama sanamu na matunda yako.

Siku moja nikaenda nikiwa na shida ya kufungua joint acc, kufika kwake hata sijamsalimia kanijibu leo sitaki matunda. Nikamwambia nina shida nyingine kabla sijaeleza akajibu tena "hapa tunasikiliza za kiofisi tuu hivyo ondoka". Sijui alijua nataka msaada wa hela au vipi.

Ikabidi niwe mpole maana alikuwa peke yake kwa muda ule customer service pale. Nikamweleza nahitaji fomu kufungua joint acc na mama yangu. Akachukua fomu akanipa akaniuliza "utaweza kusoma na kuzijaza kweli na mama yako??" Nikamjibu ndio. Akaniambia viambatanisho vinavyohitajika nikaondoka kesho nirudishe fomu.

Kesho yake nimeenda na mama, kufika pale akamkaribisha akakae kwenye kiti mimi akaniambia kasubiri pale yaani pembeni, ndio mama akamwambia nimekuja na binti yangu tunafungua joint acc, kwanza alistuka akamuuliza ni mwanao kumbe mama sikujua. Akaishiwa pozi.

Basi katika kupiga stori na bimkubwa akamwambia sikujua kama una binti mkubwa, bimkubwa akamwambia mara nyingi hayupo nyumbani kwasasa yupo likizo anasoma masters huko mkoa X. Alishangaa kwa nguvu Masters?? Aliniangalia sana. Miaka hiyo bimkubwa na mzee walikuwa wafanyabiashara wakubwa sana mkoani na chapaa zipo za kutosha wanajulikana kila kona. Bank pale walikuwa wanajulikana sana.
Enzi hizo bimkubwa na mzee CRDB wana zile VisaGold so wanahudumiwa kishua....kwahiyo dada akajua huyu sio kwamba anauza matunda kwa dhiki

Dada alikosa raha sana hadi muda anatoa copies akaniambia dada kakae kwenye kiti [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] toka siku hiyo alianza na kunisalimia na kunichangamkia. Mimi wala sikumwonyesha tofauti nikaendelea kumpelekea matunda.
Ulimfundisha somo kubwa sana,una masters na huwazi unafanya biashara zile zinaonekana ni za wenye vipato vidogo
 
Siku moja tumekaa pale morogoro round about Stendi ya viahice kwà fundi viatu anaitwa shomari. Wamekaa watu wengi kwenye mabenchi tunapiga stori sasa tulikuwa tumekaa na jenerali mstahafu wa jwtz akiwa amepaki gari yake kwenye kituo cha mafuta pale round about sass wakaja watu wa wrong parking wakalitia mnyororo lile gari. Bila kujua ni lanani yule jenerali akamtuma kijana mmoja mchoma mihogo akamwambia akawaambie wale jamaa wa wrong parking wafungue gari yake. Jamaa wakakataa. Jenerali akapiga simu kwà mkuu wa mkoa duuu dakika sifuri ffu hawa hapa tukashangaa jamaa wa wrong parking ndio wako juu ya karandinga wanaenda mahabusu.
Matumizi mabaya ya madaraka
 
Juzi tarehe 20 Jan 2023 nipo zangu Mwanza nimekuja kupiga mishe 2, 3!
Kuna mdada ni mpangaji kwenye nyumba yangu hapa lkn hatukuwahi onana zaidi ya kutumiana contracts kusign na mawasiliano ya simu.

Basi last week nikampigia simu kuwa nitakuwepo Mwanza kwa ajili ya kazi fulani ya marekebisho hapo nyumbani (kimsingi kuongeza ubora wa nyumba) basi nikafika J2 pale site... nikaanza kazi na mafundi piga kazi hadi jioni nikasepa zangu...J3 nikafika tena site...piga kazi za hapa na pale na mafundi mara pap sister ameingia akanisalimia tu kishikaji nikaitika akaingia ndani baadae akaja kuwapokea watoto wanatoka shule jioni hiyo saa 11 hv... baadae nikamwambia sister sorry niliona simu yako jana lkn late sana nilikuwa nishalala akahamaki; simu nikamwambia ndiyo...nadhani aka recall baadae akasema wewe ndo baba mwenye nyumba nikamwambia yap....ghafla akakunja mikono kama nidhamu fulani akasema sorry sikukutambua nami nikamwambia worry out ... basi akaniletea maji ya kunywa tukapiga story tu kidogo.....

Baadae akafunguka kuwa dah yaani mi naongea na wewe siku zote najua ni bonge la mbaba...nikacheka zangu tu nikamwambia surely ni bonge la mbaba sema nafanya sana mazoezi ndo maana sina nyama zembe wala tumbo la kuwekewa puto....
Umeanza vizuri mkuu ila mwisho hapo umeiharibu weekend yangu [emoji3]
 
Ulimfundisha somo kubwa sana,una masters na huwazi unafanya biashara zile zinaonekana ni za wenye vipato vidogo
Na watu wengi hawajajua biashara simple ndio zinazotoa faida sana. Kuna watu huwa wananiambia wewe ungekuwa umesoma ungekuwa mbali sana basi huwa nacheka tuu.
Ila kuna baba mmoja alikuja nikamhudumia wakati anakula akaniambia binti yangu inaonekana umesoma eeh tena elimu ya juu nikamuuliza kwann baba, akasema kuanzia customer service yako, lugha yako kwa mteja na hata ulivyo organised inaonesha elimu ipo.
 
Nawambiaga watu.. Muuza Karanga alie na Degree na Muuza karanga ambae halijui Daftari ni vitu viwili tofauti.

Mpika Chips mwenye Diploma na Mkaanga chips wa darasa la saba ni vitu viwili tofauti.

Elimu haijifichi hata ufanye kazi ya zege au uwe kondakta ,kuna kitu common kinapatikana kwa WASOMI tu huwezi kikuta kwa mtu ambae hajasoma.

Ndio mana nimesema Ntakujaga rudi kuzitafuta MASTERS na PHD baadae,sina kazi nazo ila nazitaka tu cause najua kuna kitu kikubwa sana nitajiongezea nikiwa kama MACHINGA wa biashara ya mtaji ELUFU HAMSINI.
 
Back
Top Bottom