Mimi hizo huwa nakutana nazo sana na imefika kipindi sasa nimezoea na pia nachukulia kama advantages yakuweza kusikia hata watu wanakuongea bila kujua kuwa ni wewe.
Hii imetokana na asset nazomiliki haziendani sana na muonekano wangu kwamaana hiyo Kuna kipindi nanunua viwanja nakuwa nimeshafika site ila bado unakuta muuzaji ananisubiri huku ananisema kuwa boss wenyewe hajali muda bila kujua ndie mimi.
Moja Kali nayokumbuka nilikuwa kwenye ujenz wa nyumba yangu yakuishi sasa kipindi nanunua mtendaji hakuwepo japo muhuli wake ulitumika kwa niaba, sasa nimeanza ujenzi nikawa nimemtoa mwenyekiti kidogo Ili anisimamie mambo ya kibali Cha ujenz kama mnavyojua ujenz wa dar unamambo mengi, basi nipo na mafundi nimejichanganya mara naona jopo la watu limenituzunguka wanataka mwenye nyumba yupo wapi, mafundi wakasema ongeeni na huyo wakanioneshea mm , nikamsogelea dada habari yako akajibu ahaa Mimi sitaki msimamizi nataka mwenye nyumba Yani anayejenga maana huyu atanielewa nn?
[emoji23]
Mafundi wakacheka huku wanasubiri kitatokea nn[emoji23]. Nikauliza sasa kama msimamizi maana kwaakuwa kaamua kunichukulia hivyo basi nikavaa huo uhusika, kwani dada Kuna shida gani? Akaanza nyie mnakibali au unakuja kusimamia vitu hujui kitu, kwanza taarifa yenu Sina kbsa asee taarifa ya huu ujenzi naamuru usimame mpigie boss wako, mwambie mtendaji kasimamisha ujenzi mpaka mpate kibali. Bahati yake site for men akatokea akamuita kwa jina we Fulani vipi hapo mbona mnaongea na boss wangu kwa ukali? Akabaki kamtolea macho kwa mshangao, akajikaza akasema namtaka mwenye nyumba. Jamaa akamjibu si huyo hapo ukonae [emoji23]
Nikabaki natabasam tu yy macho yamemtoka maana mjengo si haba ikambidi avunge, haijalishi anakibali sasa kwa sauti ya chini sasa [emoji23], jamaa akamwambia kamuulize mwenyekiti wako huyo kashamaliza Kila kitu. Daaaah akalowa eh basi kaka karibu sana tutasaidia kwenye mambo ya maendeleo mm huwa sipingi maendeleo ni utaratibu tu jamani, nikamuangalia tu akajizoazoa akasepa ikabaki gumzo tu pale aasee.