Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Kweli kabisa usimdharau mtu usiye mjua.

Hata mm imenitokea hiyo kuna Mkaka mmoja mtaan kwetu ukweli sikuwahi kumuelewa kabisa. Kwanza nilikuwa namuona kama hajatimia kuitwa wa kiume kwa njisi tu alivyo alivyo. Hata salamu tulikuwa hatuna.

Kuna siku moja nilikuwa nimekaa nje kwetu na shoga angu akapita huyu kaka. Nikajikuta namwambia best yng "yaani katika watu nisiowaelewa hapa duniani huyu kaka wa kwanza. " akaniuliza kwa nini, nikamwambia basi tu simuelewi katika kila kitu.

Zikapita siku za kutosha. Siku moja nimetoka zangu mishe najiandaa kuingia bafuni mara shoga angu huyoo ananiita. Nikamwambia nisubiri ndani nakuja. Niliporudi ile naingia tu kuniona akaanza kucheka hatari. namuuliza wacheka nini wewe. akajibu yule kaka usiyemuelewa hapa duniani kanipa zawadi hii nikuletee. Anaomba kukutana na ww. Looh nikamwambia muongo ww naanzaje kwenda kumsikiliza na kwa nn umepokea zawadi hii ikiwa unajua kila kitu. akasema ndio hivyo nenda ukamsikilize uku anacheka hatari.

Kweli sikwenda siku hiyo. Ilipita kama wiki mbili hivi akuacha kunitumia zawadi. Ile kitu ikanifanya niwe namfikiria sana. Nikampa nafasi nikaenda kumsikiliza. Akamwaga sera zake pale nikazipokea taratibu nikaanza nikazifanyia kazi. Nakumbuka kauli yake ya kwanza alisema "Nakupenda, sitaki kujua kuhusu mahusiano yako uliyonayo ingawa ninchojua mm hujaolewa, so nipe nafasi alafu utachagua ww yupi anakufaa." Hakuwa na mengi

Looh mpaka leo siamini nimezama mwenzenu. Alivyo kwa nje na ndani tofauti kabisa. Na sasa ndoa imetangazwa.
Kweli usimdharau mtu usiye mjua
Kwa nje yukoje?
 
Kwanza naomba 'nidiclee' kwamba mm ni mmoja wa ME ambae si mtu wa fashion, yani mimi sijui kuvaa kabisa na sina hiyo passion ya pamba pamba. Nishawahi kusemwa sana na ma-ex wangu kuhusu uvaaji wangu lakini haikusaidia kitu.

Sasa weekend iliyopita nilienda sehemu moja flani hivi amazing, chimbo la uhakika haswaa, limejitenga na limetulia kweli. Nilipigilia kipensi changu na ka t-shirt flan hivi local nikachagua sehem nikakaa, kutizama vizuri nikaona kuna meza amekaa mdada mmoja hivi and of coz she is gud looking nikaamua kujitosa angalau kumpa hata hi 'coz tulikuwa wateja 2 tu, nikamfata nikamsalimu.

Yule dada kwanza alinishusha kuanzia juu mpaka chini then akaitikia salamu yangu ki-design kama namsumbua flani hivi. Nikaomba kujumuika nae kama asipojali. Jibu lake ndo lilinitoa confidence kabsa, alinambia: "Kwahiyo kaka unadhani kila msichana akikaa peke yake anahitaji kampani? Hapana sihitaji" Dah, mwanamme nikajizoazoa pale nikarudi nilipokaa. Nilikaa kama masaa ma3 hivi nikaamsha zangu. Sasa kilichotokea jana ndo kimenifanya niandike huu uzi.

Nilipokea maagizo kuanzia J3 ya wiki hii kuwa leo watakuja watu wa Taasisi flani ya kifedha kutoa semina kwa sisi wafanyakazi kwa ajili ya kutushawishi kujiunga na huduma za Taasisi yao, hivyo mimi nikapewa jukumu la kuwakaribisha na kuwapeleka sehemu ambapo semina itafanyika.

Asubuhi mida kama ya saa 3 hv ugeni ukafika, walikuwa watu kama 7 hivi, kati yao alikuwepo yule dada nilieonana naye weekend.

Wakaingia ofisini nikawakaribisha, wakati mkubwa wao anatoa introduction macho nikayakaza kwa yule dada, bahati nzuri tukagonganisha macho, akashtuka flani, nikajua kashanikumbuka.

Baada ya semina kuisha ikafika kipindi cha watu kujiunga sasa kwa walioshawishika. Nikamfata yule dada nikamuomba aje anielekeze namna ya ujazaji fomu. Alivyofika tu, nikamuuliza "Unanikumbuka?" Akachekaaa, akaniambia "Yani wewe, sikutarajia kama unaweza kuwa unafanya kazi huku", nikamuuliza ulitarajia niwe nafanya kazi wapi? Akaishia kucheka tu. Mawasiliano yake kanipa; fresh bila shida kabisa.

Sasa naomba kuuliza wadau, mshawahi kukutana na situation ya namna hii?
Yote tisa ulimtafuna?.Km Mwanaume,mwanamke akikuletea shobo za hivyo muonyeshe kuwa wewe ni level Zingine.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Sisi wengine baada ya hapo ndio huwa tunafunga vioo mazima, yaani fanya kama hatujawahi kukutana.

Mimi jamaa alinisimulia hii tabia ya kudharau mikakati ya mtu katika maisha yake, usione mtu kazini yupo yupo tu miaka inaenda ukamdharau kwamba hana mipango, utajichanganya.

Jamaa anasema wameanza kazi mwaka mmoja na huyo mshikaji wake, yeye akawa amepanga nyumba ya gharama kama 250k, usafiri wa kusumbulia watu mjini nk. Mwenzake yupo yupo tu, nyumba katafuta ya 120k, gari hakununua nk.

Wamefanya kazi kama miaka 8 hivi, baadae siku moja wanapiga story jamaa yangu sasa akaanza maneno ya kumsimanga jamaa, oooh we vipi bana hela hatuoni wapi unapeleka, upo upo tu kama mshamba. Jamaa akakereka ikabidi amuonyeshe salio bank, akasoma kwa utulivu ilikuwa ni 68 mil, kwenye simu kuna 7 mil.

Baada ya pale jamaa siku yake iliharibika sana.
Umeona eenhh?!!.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Mtu unayemdharau either Kwa mwonekano au kazi anayofanya .wengi wamebeba vitu unavyohitaji maisha mwako 100%.kama Kuna kitu unakihitaji duniani haijalishi nicha ukubwa kiasi gani basi watu wa Hali hiyo wanajua namna gani ya kukusaidia...

Mimi nilishasaidiwa vitu viwili vikubwa sio vidogo na MUUZA MAJI YA MADUMU anayesambaza kwenye majumba..unaweza kusema mtu huyu atanisaidiaje na Hali yake hii ya chini? Nilidhani mtu anayevaa tai na smart ndio anaweza kunisaidia ..Ukimwona mtu anafanya kazi ya Hali ya chini usimdharau wengi wao huwa pia na michongo mikubwa Sana na wakikupa unatoboa..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Upo sahihi kabisa mkuu,
Binafsi mimi niliwahi kuunganishwa na matajiri na wenyw vyeo kupitia watu wa kawaida mno ambao binafsi huenda nisingekaa nionane nao au wanifahamu.

Niliwahi gundua kwanini matajiri wanawaheshimu watu wanaonekana hawana kitu ni kwa sababu baraka za watu wengi ziko kwa watu ambao huwadhanii!
 
Kuna footballer mmoja maarufu Sana aliwahi kucheza timu ya aseno(jina limenitoka) nadhani timu yake ya taifa ni Sweden.

Huyu jamaa, Kuna stories nilipata kusimuliwa Kuna siku alienda mgahawani huko kwao, Sasa alivyofika wahudumu hawakumtambua wakawa wanamchukulia poa. Kile kitendo kilimkera Sana, kwa hasira akaamua kuununua ule mgahawa fastaaa
Chai hii
 
nakumbuka kuna kidemu kilikua kinanidharau sana enzi hizo bush, basi nilivyomaliza shule pale kijijini nikaondoka kwenda Dar ikapitwa miaka 4 nikasikia kapewa mimba na aliyempa mimba nimshikaji niliesoma naye na alipewa mimba akiwa bado anasoma, basi kwakuwa jamaa nayeye alikua na ndg Dar ikabidi wakimbilie Dar es salaam kwa ndg wa mshikaji baada ya mwaka mmoja kupita ndipo wakashauriwa waende hospital kwa ajili ya kufanya uzazi wa mpango na hospital ilikua maeneo ninayoishi basi mshikaji ndg yake akamwambia nenda utamkuta rafiki yako uliesoma naye akuelekeze bwana weee

si wakaja mpaka home yule demu hakuamin kama ndiyo mimi aliekuwa ananidharau kule bush basi nikawasindikiza mpaka hospitalini kisha tukarudi nikawapeleka mpaka stendi yule demu nafsi ilimsuta sana mpaka aliamua kunitumia sms akisema kweli nimeamini usimdharau mtu ktk hii Dunia nilikuwa nakuchukulia poa poa kijijini leo unaijua mitaa ya Dar kiasi hiki na umetupeleka mpaka hospitali

aliishia kusema nisamehe, nami sikumjibu maskini.
Mkuu hapa sijaelewa. Kumbe ukiijua mitaa ya Daslam nayo heshima kubwa hivi?
 
Nakumbuka siku nareport shule kuanza 4m 5, sasa kufika pale ofisin kwa makamu wa shule kufanya usajiri,
Ile alivoniona akakaa kimya km dakika 10 anantazama tu, baadae akaniuliza full details zangu nkatoa kumpa (result slip na leaving) plus resit za michango mbalimbali.

Then akaangalia kweny file la selection alipoliona jina langu alishtuka na kuhamaki mno, akasema "ulivyo hufanani na kusoma tahasusi hii, tena kwa shule km hii, na matokeo yako ya 4m 4 na shule uliyotoka hufanani nayo" kiukweli nilijskia vibaya sanam

Ila still maisha yaliendelea hadi nikahitimu, siku nimeenda pale kuchukua results slip na leaving, ndo akanambia kuwa alivyokua anadhani sivyo na alivotegemea wala kuwepo.

Mie huyo nikasepa zangu.
Dakika 10 anakutazama tu. That's too much my nigga!! I can't take it anymore.
 
Kabla sijawa jobless wa kitaa kuna kazi nilikuwa nafanya kwenye NGO fulani sasa kuna siku tulikuwa na kikao na viongozi wa mkoa. Nilipofika kwenye ukumbi wa mkuatano nilikuta kuna washkaji kutoka ofisi ya mkoa wamekaa nikawapa salamu wakaitikia ila dharau flani hivi ( niliwahi ili kuweka mambo flani sawa hapo ukumbini kumbe na wao waliwahi nadhani kungalia mambo ya Security) walikuwa wanajiskia kinomanoma. Mkuu wa mkoa akafika na viongozi wengine nikawa nasalimiana nae kishkaji sana wale jamaa wakabaki wanashangaa nadhani walifikiri kuna mtu mwingine ndo ataendesha kile kikao ajabu wakakuta ni mimi naendesha kile kikao. Ulipofika muda wa kuwasainisha zile posho zao wakaanza kuleta shobo za kinafki ila niliwakaushia tu kuonyesha ushkaji, from there mambo yangu yaliyohitaji sapot kutoka ofisi ya mkoa yalikwenda fresh sana maana jamaa waligeuka washkaji sana. Sema now nimekuwa jobless ila tukikutana wananiita mkuu hawajui tu kuwa nimeshakuwa jobless wa kitaa sina lolote
 
Kabla sijawa jobless wa kitaa kuna kazi nilikuwa nafanya kwenye NGO fulani sasa kuna siku tulikuwa na kikao na viongozi wa mkoa. Nilipofika kwenye ukumbi wa mkuatano nilikuta kuna washkaji kutoka ofisi ya mkoa wamekaa nikawapa salamu wakaitikia ila dharau flani hivi ( niliwahi ili kuweka mambo flani sawa hapo ukumbini kumbe na wao waliwahi nadhani kungalia mambo ya Security) walikuwa wanajiskia kinomanoma. Mkuu wa mkoa akafika na viongozi wengine nikawa nasalimiana nae kishkaji sana wale jamaa wakabaki wanashangaa nadhani walifikiri kuna mtu mwingine ndo ataendesha kile kikao ajabu wakakuta ni mimi naendesha kile kikao. Ulipofika muda wa kuwasainisha zile posho zao wakaanza kuleta shobo za kinafki ila niliwakaushia tu kuonyesha ushkaji, from there mambo yangu yaliyohitaji sapot kutoka ofisi ya mkoa yalikwenda fresh sana maana jamaa waligeuka washkaji sana. Sema now nimekuwa jobless ila tukikutana wananiita mkuu hawajui tu kuwa nimeshakuwa jobless wa kitaa sina lolote
Life goes on
 
Back
Top Bottom