Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Kabla sijawa jobless wa kitaa kuna kazi nilikuwa nafanya kwenye NGO fulani sasa kuna siku tulikuwa na kikao na viongozi wa mkoa. Nilipofika kwenye ukumbi wa mkuatano nilikuta kuna washkaji kutoka ofisi ya mkoa wamekaa nikawapa salamu wakaitikia ila dharau flani hivi ( niliwahi ili kuweka mambo flani sawa hapo ukumbini kumbe na wao waliwahi nadhani kungalia mambo ya Security) walikuwa wanajiskia kinomanoma. Mkuu wa mkoa akafika na viongozi wengine nikawa nasalimiana nae kishkaji sana wale jamaa wakabaki wanashangaa nadhani walifikiri kuna mtu mwingine ndo ataendesha kile kikao ajabu wakakuta ni mimi naendesha kile kikao. Ulipofika muda wa kuwasainisha zile posho zao wakaanza kuleta shobo za kinafki ila niliwakaushia tu kuonyesha ushkaji, from there mambo yangu yaliyohitaji sapot kutoka ofisi ya mkoa yalikwenda fresh sana maana jamaa waligeuka washkaji sana. Sema now nimekuwa jobless ila tukikutana wananiita mkuu hawajui tu kuwa nimeshakuwa jobless wa kitaa sina lolote
Hakikisha unalinda brand mkuu usiwaonyeshe now huna job
 
Dakika 10 anakutazama tu. That's too much my nigga!! I can't take it anymore.
Nimesema km, inawezekana hazikufika 10, ila zilikaribia, ilichukua mda cku ile.
Nweiiii ishapita, na imebaki story.
 
2007 ndo nlimaliza chuo RMIT, 2008 nikaajiriwamoja ya mikoa maskini sana km mwalimu wa chuo, 2009 nikaanza kuishi na mchumba wangu she was 20 yrs old mm nlikua 27, nlikua na ka mwili kadogo sana, yeye pia,
Tulipanga nyumba nzima na tulikuwa na mtoto 1 ofcourse tulimpata 2007 tukiwa wanachuo, sasa siku moja jamaa kaelekezwa kwangu alikuwa ana shida ofisini akaja weekend. Sehem nilokuwa nimepanga ilikuwa ushuani sana walikua wanaishi watu mabosimabosi tu, ulinzi kama wote maana ni nyumba za taasidi flani ya kidini.
Alinikuta nafanya kazi ya usafi uwanjani nipo na wife nina kipensi na wife pia kipensi, tukasslimiana ila alituchukulia km watoto wa pale, akauliza nimewakuta wenye nyumba, wife akamjibu ndio yupo, akaomba aitiwe wife akamwambia ndo sisi, jamaa alishtuka waziwazi tena mshtuko bila kujificha, akasema hata hamfananii kabisa.

La pili limenikuta mwezi ulopita, mm ni professional yangu ni mtaalam wa IT, sasa kwa sasa ni kiongozi mkubwa tu bext to principal, wakaja watu wa utumishi kufanyisha online aptitude test, walinikuta nimevaa simple tu Tshirt na kadet na raba simple tukapiga kazi sana na mashine jama 20 hivi zilizingua so baada ya kumaliza majukumu ya siku hiyo mida ya saa2 usiku nikaanza kuzirekebisha hadi saa 8 usiku, jamaa tulipiga nao hadi mda huo, kwa ajili ya maandalizi ya kesho yake coz kulikuwa na nyomi. Tulivomaliza jukumu ikaja muwind up, mkuu alisafiri so nikawa nimeachiwa chuo, it was mobday so huwa navaa kulingana na kazi za siku hiyo wakanikuta nimevaa suti safi, nao walishtuka sana jamaa akanichana kuwa hakufikiri kabisa kuwa mm nina nafasi ile alifikiri ni mtu tu wa IT pale chuon,nikamjulisha mm pia ni mtu wa IT hujakoseana mwenzangu kasafiri kikazi ndo maana uliniona kule, japo kwa sasa huku ndo ofisini kwangu.
 
Pamoja na yote,ila tuseme ukweli..mkuu unaonekana ni mtu wa visifa flani hivi.
 
Naenda zangu dar mida saa 3 ivi kutoka dodoma, nimekurupushwa tu kwa ofis nikaona sio mbaya nikapita zangu pale stend ya cbe kwa mama bwashee hua ana supu nzuri gari niliacha inaoshwa kona pale, basi wakat naingia pale nikakuta wadada wanne pisi haswa na mshkaji moja nao wanaingia na mabegi yao nikawasalimia kwa mbwembwe sana mi ni mtu utani sana, duh nilipandishwa na kushushwa aisee, binti mmoja tu ndo alipokea salam wengine hata habar na mimi hawana.

sijakoma nikaendelea kuwachangamkia jamani mnaenda dar nina usafiri? wakaniangalia tena juu mpaka chini nimevaa simpo sana kipensi na sendoz, yule yule dada aliyenipokelea salam ndo akajibu ndio boss, nikamwambia mbele yao we unaonekana mstaarabu sana hutolipa nauli, ajabu hata mwanaume mwenzangu eti kama hanioni....
basi tumekula pale nikainuka nikamuaga yule mrembo nakuja nafata gari sogea pale pemben ya barabara akacheka akasema sawa bos, nikafata chuma nafika pale nawaona wanajivuta lakin wadada wa3, mdada mmoja na mshkaji wamekaa zao hawana hata habari...
 
...wadada wenyew hawajajua bdo kama ndo mm, chuma vxr inawaka...wakaja wale jamaa ''mzee wapi nina wa dar 3'' nikamwambia waite wale wadada ndo naenda nao...akawaita wadada wanasogea ndo mm kwanza wakaishiwa pozi, wpaka wanaogopa kupanda nikawambia twendeni au hamuendi? wakaingia mmoja akataka akawaite wale wenzao nikawakataa tu, nikachukua na jamaa mmoja pale mie huyo safari....wale wadada wengine kila nikiwachungulia kwa kioo n kama wameishiwa sana pozi angalau yule mwingine hata stori anapiga....

anasema yani boss ilikuwa ngumu kuamini kama kwel ulikuwa na gari, mi tabasam tu....
tulitoka dom saa 4 saa nane nipo mbez, wadada wanasema hawajawahi kusafir dar to dom kwa muda mchache ivo, wanawapigia wale viazi tuliowaacha ndo kwanza wapo gairo......
basi nkawashusha mbez nkachota namba zao pale mie huyooo.....usiniulize kilichofuata......
 
Namjua omba omba flani alikua anapga mishe zake za omba omba POSTA lakini anakaa MBEZI MWISHO.

Nilimjulia ofisini kwangu alikua akipenda kuja na kibaiskeli chake cha walemavu kunywa SUPU kila asubuhi.

Trela linaanza kifungua kinywa chake ni kila siku bili ni 15,000 hiyo no yangu Jikoni. Asipopiga mchemsho wa samaki,ujue atapga mchemsho wa kuku.

Au lah atakupigia SPECIAL ya UTUMBO,sio poa huyu mjomba.

Hapo ofisini kuna dada alikua akitoka nae kimapenzi,ndie aliekuja vujisha kila kitu.

na huyu omba omba ndie alienifanya Hadi LEO siwezi saidia OMBA OMBA wa barabarani.

Omba Omba huyu (mlemavu asie na miguuu)

Kwake sio pa kisport sport,anapolala (hilo godoro + kitanda tu) achana na vitu za electronic video niliyoletewa, nilisema Sisaidii omba omba bila kujiridhisha.

Omba Omba ana hadi nguo za kazini,ah weeeeee Mimi kusaidia omba omba NEVER.
Kuna mmoja pale kariakoo anakula biriani ya ngamia 9000, maji ya buku na anakuja kazini na pikipikj na kuondoka na pikipiki 15000 kila siku. Hapo sijawah kuiona chai yake. Nasikia mwanae yuko St. Francis mbeya.. omba omba ana uchumi ambao mm siuwez
 
W
dah kuna demu nilipita naye celebrity maarufu nilimpiga sound mimi nina miliki kampuni ya ujenzi na usafirishaji wa mizigo DRC, zambia, SA nk..

Kiukweli amekula kula sana vichenji vyangu huku nikitumia Vogue Vera yakuazima ya mwanangu mmoja + Nissan patrol V8.. demu akaona kapata kidume, nilimla kotekote kupunguza hasara zangu..

Dah alivyojua sina lolote naungaunga tu mjini ila wanangu wengi wako sawa wanachenjichenji hizi bongo hapa akanikimbia na ananichukia balaa... ILA ANA JINA KUBWA SANA MJINI BONGO shida njaa njaa sana hawa celebrity..
Wewe kama mm tu
 
Nilikuwa form one siku hiyo nilienda shule na nguo za nyumbani afu nilikuwa nimechelewa, nikakutana na mwalimu wa zamu getini na ni mwalimu wa Civics pia, sasa akawa ananisema pale mara ooh una sura mbaya umevaa nguo za nyumbani, huna akili na maneno kibao pale na fimbo juu, akaniruhusu niende darasani. Nipo darasani kuna mtu anakaja akaniambia naitwa na mwalimu wa Civics kwenda kule mwalimu ananiambia sijakuita wewe namtaka mtu fulani nikamwambia ndo mimi akashangaa akaniambia kumbe una akili nilikuwa nimepata 97% wa pili alipata 47% kwenye somo lake
 
Story
Kuna dada mmoja tajiri sana alikuwa anamiliki ndinga lake kali aina ya mercedez benz latest model.
Bac siku moja akawa amesafiri nnje ya mji(country side) isivyo bahati gari lake likaharibika na alipokuwepo hamna garage au usaidiz wowote! Maeneo hayo palikuwa na mzee ambaye umri umeenda (mstaafu ambaye ameamua kutulia zake nnje ya mji),Bac mzee baada ya kuona gari la bibie limeharibika at the middle of nowhere,

Mzee:Akamuuliza naweza kukusaidia?
Bibie:Akawa anampuuzia huku akionekana kumtafuta mtu kwenye simu.
Mzee:Acha niangalie tatizo ni lipi mzee akasisitiza
Bibie:Hutaweza kufanya chochote haya sio yale magari ya enzi zenu.
Mzee:Hakujibu akasogea karibia na gari akafungua boneti hazikupita dakika 3 akawa amemaliza akamwabia bibie awashe saa ngapi gari halijaitika!
Bibie:Kwa mshangao akamwambia mzee nikupe kitu gani kwa msaada huu sema chochote!
Mzee:Sihitaji chochote
Bac kwasababu mzee alionekana kutotaka chochote bac....
Bibie:Akamwambia Ahsante akajitambulisha kuwa anaitwa Nataliah
Mzee: Akajibu karibu naitwa mercedez benz.
 
Back
Top Bottom