Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Juzi juzi nilienda kumlipa Binti yangu ada kwenye shule fulani ya watoto wa kike kufika office ya Mhasibu nikamkuta mama flani namslimia akanishusha tu akaendelea na mambo yake. Nikamsalimia mara ya pili ndo akanijibu "nimeshakusikia" nikaamua kusubiri alipomaliza mambo yake ndo akaniita "haya unasemaje?" Nikamwambia nimekuja kumlipia ada ya Binti yangu anayesoma hapa
Akashtuka "ooh kumbe sikujua"
Nikatoa bank slip ya 3.5m ambayo ni ada ya mwaka mzima Pamoja na slip ya pili yenye laki 5 ya michango
Alipoona hivyo akaanza kujichekesha mpk akawaagiza wanafunzi wamwite Binti yangu amsalimie .
Alidhani wewe Nani?.

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
Ulizidi kukonda na kuchakaa...kuna mdada mmoja mkenya wanaishi Germany sasa ukimuona utazani beki tatu hana alama ya kutoka ulaya...amechakaa m
Hadi kero....ndio umenikumbusha huyu ndugu yetu mkenya.
Wakenya hata nuru huwa hawana halafu kuvaa hawajui, muonekano hawana wengi wao.
 
Mimi hata omba omba wanao kaa barabaran siwachukuli Poa , Una mdharau kumbe aingiza kipato kuliko wewe unaempa 500
Namjua omba omba flani alikua anapga mishe zake za omba omba POSTA lakini anakaa MBEZI MWISHO.

Nilimjulia ofisini kwangu alikua akipenda kuja na kibaiskeli chake cha walemavu kunywa SUPU kila asubuhi.

Trela linaanza kifungua kinywa chake ni kila siku bili ni 15,000 hiyo no yangu Jikoni. Asipopiga mchemsho wa samaki,ujue atapga mchemsho wa kuku.

Au lah atakupigia SPECIAL ya UTUMBO,sio poa huyu mjomba.

Hapo ofisini kuna dada alikua akitoka nae kimapenzi,ndie aliekuja vujisha kila kitu.

na huyu omba omba ndie alienifanya Hadi LEO siwezi saidia OMBA OMBA wa barabarani.

Omba Omba huyu (mlemavu asie na miguuu)

Kwake sio pa kisport sport,anapolala (hilo godoro + kitanda tu) achana na vitu za electronic video niliyoletewa, nilisema Sisaidii omba omba bila kujiridhisha.

Omba Omba ana hadi nguo za kazini,ah weeeeee Mimi kusaidia omba omba NEVER.
 
Dah 😂 sa we umejuaje mpya?
mi mwenyewe nina ID 10 ukiniblock hii,kesho napanda JF na zingine.

nikiwa kwa ID zingine ndio ninapojua huyu Depal id yake ni hiii,huyu kwini id yake hiii... Mambo wazi wazi, Dr kumbuka anakwambia Mambo Open Open,Kimbia toka nnje ya JF kbsa ila uki switch ID tu tunaswichika na wewe.
 
Namjua omba omba flani alikua anapga mishe zake za omba omba POSTA lakini anakaa MBEZI MWISHO.

Nilimjulia ofisini kwangu alikua akipenda kuja na kibaiskeli chake cha walemavu kunywa SUPU kila asubuhi.

Trela linaanza kifungua kinywa chake ni kila siku bili ni 15,000 hiyo no yangu Jikoni. Asipopiga mchemsho wa samaki,ujue atapga mchemsho wa kuku.

Au lah atakupigia SPECIAL ya UTUMBO,sio poa huyu mjomba.

Hapo ofisini kuna dada alikua akitoka nae kimapenzi,ndie aliekuja vujisha kila kitu.

na huyu omba omba ndie alienifanya Hadi LEO siwezi saidia OMBA OMBA wa barabarani.

Omba Omba huyu (mlemavu asie na miguuu)

Kwake sio pa kisport sport,anapolala (hilo godoro + kitanda tu) achana na vitu za electronic video niliyoletewa, nilisema Sisaidii omba omba bila kujiridhisha.

Omba Omba ana hadi nguo za kazini,ah weeeeee Mimi kusaidia omba omba NEVER.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
dah kuna demu nilipita naye celebrity maarufu nilimpiga sound mimi nina miliki kampuni ya ujenzi na usafirishaji wa mizigo DRC, zambia, SA nk..

Kiukweli amekula kula sana vichenji vyangu huku nikitumia Vogue Vera yakuazima ya mwanangu mmoja + Nissan patrol V8.. demu akaona kapata kidume, nilimla kotekote kupunguza hasara zangu..

Dah alivyojua sina lolote naungaunga tu mjini ila wanangu wengi wako sawa wanachenjichenji hizi bongo hapa akanikimbia na ananichukia balaa... ILA ANA JINA KUBWA SANA MJINI BONGO shida njaa njaa sana hawa celebrity..
 
hujaendana na uzi wenyewe
 
Mada hii toka imepostiwa huwa natamani kuchangia but ubize na uvivu wa kuandika vinanishinda Nguvu.

Ngoja leo nitoe kisa kimoja katika visa vyangu vingi vya maisha yangu.

Mwaka 2008 nikimuuguza mzee wangu katika hospital moja kigoma ipo sehem mmoja panaitwa Manyovu ile hospital kama sijasahau itakuwa inaitwa Nyamasovu.

Nikiwa kijana mdogo katika watu walokuwa wakiwauguza na kusimamia wagonjwa wao, Manessi walinichukulia poa sana. Mda mwingne walinifokea kipindi wananipa maelekezo.

Namkumbuka nessi mmoja mdogo kama wa miaka 20-22 hivi. Mzee alikuwa kafanyiwa sajari na alikuwa kawekewa mipira yakutolea uchafu mwilini hivyo kuna muda ilikuwa ikijaa naenda kumwita yule nessi aje atoe na kum badirishia mfuko wa uchafu , alikuwa ananitizama kwa dharau sana. Kuna siku akanitamkia kabisa " we kaka mbona msumbufu? Nikajibu nessi me naangalia uhai wa mzee wangu akanambia Kwani baba yako ndo atakuwa wa kwanza kufa, ? Ivi mnahisi Manessi tunafurahia kuchezea uchafu wa wagonjwa wenu? Ungesoma nawewe ukawa nessi ukaona tunachokifaidi sisi. " duh! Kiukweli niliumia sana.

Kwa uwezo wa MUNGU mzee akapona , siku ninaendea ruhusa ili tumrudishe nyumbani kale kanessi kakaniambia kwa kejeli "Baba wa Taifa amepona " nikajifanya sijaelewa kakaongeza et "unahangaika utafkiri unamuuguza Yesu " kipindi hicho nilkuwa bado nasoma ko nikawa napretend ustaarabu ili nisiharibu cv .

Baada ya miaka kupita nikiwa nishasahau siku moja nipo kwenye ndege pakawa kuna mdada siti ya mbele yangu (kama siti ya3 toka kwangu upande wa kushoto) ananiangalia sana. Yani kila dakika anageuka tukikutabisha macho me naangalia pembeni nikiinua macho tena nakuta ananiangalia tena. Nikahisi labda ni x wangu flan iv katika ma x zangu. Tulivyoshuka mw/ Julius Nyerere watu wakaanza kushuka nikawa nimeinamia simu naiwasha baada yakuizima kipindi ndege inaanza safari nikainuka ile navua mkanda nainuka kuotoa begi juu nakuta watu wengi washashuka kabaki dada mmoja tu na wahudumu wa ndege. Nikashuka chini ile nipo kwenye ngazi akanigusa mtu kwa nyuma nikageuka sikuwa namkumbuka akajitambulisha kumbe ndo yule nessi. Kwakuwa sikuwa mtu wakuweka kinyongo nikamchangamkia tukatoka nje nikawa nasubiri Dogo aniijie na gari la home kumbe yeye hana usafiri anawaza tax nikamkazia kama sioni shida yake akajishusha mwenyewe akaomba lift nikamchukua hadi tunafika ubungo hajasema anaenda wapi kumbe alijiendeleza kielim ko anasoma Md muhimbili ila dsm hana mwenyeji ko nikampeleka napoishi akalala (mana ilikuwa ishakuwa usiku) kesho asbuhi me nayeye hatukuweza kuonana mana nilikuwa nina mishe zangu zilizonileta mjini ko alivyoamka akaoga akapata chai dogo akampeleka chuoni. Aisee alinipigia simu usiku wake eti ndo ananiuliza mzee anaendeleaje. Then sikutaka tuyaongelee ya kipindi kile ila alinisihi sana nimsamehe na kuanzia siku hiyo heshima mpaka sasa
Mpuuz Sana hyu nesi "eti unamuuguza yesu,pumbafu sana

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mimi kuna jamaa tumesoma wote form 1&2 tulikuwa washkaji maana ndo tulikuwa tunaongoza class
Nikafukuzwa so 3&4 tulikuwa tunakutana likizo tu
Baada tukapotezana Ila me nilikuwa napata data zake alimaliza degree ya mambo ya afya akaingiza jeshi then akapelekwa mondul kusomea sijui vyeo then akapangwa mikoan huko
2020 sm inaita ni jamaa " Flan vip? Za siku niomeambiwa uliacha kazi ya ualim now unapiga umachinga dar? Tuonane basi ndg" ni kweli niliachaga ualim nikajichanganya kariakoo kabla sijatoboa kibiashara ambayo hakuwa anajua kuwa nilitoboa tena kwa kiwango kikubwa
Basi tukakutana Mliman me ndo nilitangulia pale Grano
Jamaa akaja "agiza chochote ntalipa kaka " mbwembwe nyingi
Me na mwili mdogo halaf kwenye uvaaji me ni 0% so ngumu sana mtu kujua huyu yuko vzr au la!
Tukiwa pale dem wangu akaniambia nimfate kazin kumrudisha home alkkuwa mjamzito nikamwambia mshkaji akajibu " haina shida na usafir kaka twende tutamchukua tu nishanunua gari siku hizi mambo yangu fresh "
Nikakubali tukatoka nikamwambia tupite nichukue langu tuongozane ndo anaanza kushangaa " kwan una gari? Machinga ana gari mura au nimedanganywa!?"
Tumefika mzee anaona BIMA imepaki nafungua namwambia twende na hii tukirud tutapitia yako
Jamaa alikosa aman sikujua why ila alikosa aman kabisa
Tumemaliza kule namrudisha Mliman kumbe ana Swift old mole dah jamaa tangu pale alikata mawasiliano mpk leo tunaview tu status
Duuu [emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
Kipindi hicho nmeingia form 1 kuna jamaa alikuwa anaitwa Juma , uniform zake zilikuwa zimechoka choka inaonekana shati alikuwa anatumia darasa la saba au Kuna mtu alimwachia alaf alikuwa sio muongeaji sana tofouti na wanafunzi wengine kila mtu alikuwa anajifanya mjanja

Sasa mimi nikawa na muona Kama boya flani hivi nikajua hata akili atakuwa hana japo nilikuwa simuoneshi kama na mchukulia poa , sasa imefika mitihan ya mwez wa 6 tumefanya tumeenda likizo tumerudi matokeo yamebandikwa sasa nauliza huyu juma ndo nani naoneshwa jamaa na ambiwa jamaa toka primary uwaanaongoza kiwilaya toka siku hiyoo respect akawa na rafiki yangu tunaenda kusoma wote .
 
Kwanza naomba 'nidiclee' kwamba mm ni mmoja wa ME ambae si mtu wa fashion, yani mimi sijui kuvaa kabisa na sina hiyo passion ya pamba pamba. Nishawahi kusemwa sana na ma-ex wangu kuhusu uvaaji wangu lakini haikusaidia kitu.

Sasa weekend iliyopita nilienda sehemu moja flani hivi amazing, chimbo la uhakika haswaa, limejitenga na limetulia kweli. Nilipigilia kipensi changu na ka t-shirt flan hivi local nikachagua sehem nikakaa, kutizama vizuri nikaona kuna meza amekaa mdada mmoja hivi and of coz she is gud looking nikaamua kujitosa angalau kumpa hata hi 'coz tulikuwa wateja 2 tu, nikamfata nikamsalimu.

Yule dada kwanza alinishusha kuanzia juu mpaka chini then akaitikia salamu yangu ki-design kama namsumbua flani hivi. Nikaomba kujumuika nae kama asipojali. Jibu lake ndo lilinitoa confidence kabsa, alinambia: "Kwahiyo kaka unadhani kila msichana akikaa peke yake anahitaji kampani? Hapana sihitaji" Dah, mwanamme nikajizoazoa pale nikarudi nilipokaa. Nilikaa kama masaa ma3 hivi nikaamsha zangu. Sasa kilichotokea jana ndo kimenifanya niandike huu uzi.

Nilipokea maagizo kuanzia J3 ya wiki hii kuwa leo watakuja watu wa Taasisi flani ya kifedha kutoa semina kwa sisi wafanyakazi kwa ajili ya kutushawishi kujiunga na huduma za Taasisi yao, hivyo mimi nikapewa jukumu la kuwakaribisha na kuwapeleka sehemu ambapo semina itafanyika.

Asubuhi mida kama ya saa 3 hv ugeni ukafika, walikuwa watu kama 7 hivi, kati yao alikuwepo yule dada nilieonana naye weekend.

Wakaingia ofisini nikawakaribisha, wakati mkubwa wao anatoa introduction macho nikayakaza kwa yule dada, bahati nzuri tukagonganisha macho, akashtuka flani, nikajua kashanikumbuka.

Baada ya semina kuisha ikafika kipindi cha watu kujiunga sasa kwa walioshawishika. Nikamfata yule dada nikamuomba aje anielekeze namna ya ujazaji fomu. Alivyofika tu, nikamuuliza "Unanikumbuka?" Akachekaaa, akaniambia "Yani wewe, sikutarajia kama unaweza kuwa unafanya kazi huku", nikamuuliza ulitarajia niwe nafanya kazi wapi? Akaishia kucheka tu. Mawasiliano yake kanipa; fresh bila shida kabisa.

Sasa naomba kuuliza wadau, mshawahi kukutana na situation ya namna hii?
Hizi dharau mbona kwa Bongo ni kitu cha kawaida kabisa. Hasa wadada ndio maana wanaangukiaga kubaya kwenye mahusiano
 
Hata sio Sifa bali vitu vingine ni aibu kusimulia, yaani muislam wajigamba kwa kutukufahamika dini yako!! Aibu gani hii
Kwani peponi walio watakatifu wataingia kwa kigezo cha dini? Mwenyezi MUNGU ni dini gani?
 
Siku moja tumekaa pale morogoro round about Stendi ya viahice kwà fundi viatu anaitwa shomari. Wamekaa watu wengi kwenye mabenchi tunapiga stori sasa tulikuwa tumekaa na jenerali mstahafu wa jwtz akiwa amepaki gari yake kwenye kituo cha mafuta pale round about sass wakaja watu wa wrong parking wakalitia mnyororo lile gari. Bila kujua ni lanani yule jenerali akamtuma kijana mmoja mchoma mihogo akamwambia akawaambie wale jamaa wa wrong parking wafungue gari yake. Jamaa wakakataa. Jenerali akapiga simu kwà mkuu wa mkoa duuu dakika sifuri ffu hawa hapa tukashangaa jamaa wa wrong parking ndio wako juu ya karandinga wanaenda mahabusu.
Ishu kama hii nimewahi ishuhudia pia sehemu, kuna siku nilikuwa nimekaa na jamaa yangu mmoja alikuwa na kibanda cha MPESA, ghafla akaja mzee mmoja na Hilux Double cabin la zamani akali-park kando ya barabara then akaja kutoa pesa hapo kwenye kibanda, kumbe jamaa wa wrong parking mbio mbio wakaliwahi gari wakapiga chain...mzee kurudi kwa gari wakaanza mabishano weeeh na mbaya zaidi alikuwa na mtoto mgonjwa kwenye gari ndo anamuwahisha hospitali, jamaa wa wrong parking sijui wanakuwaga na matatizo gani...waligoma kumfungulia yule mzee mpaka akapiga simu mahali, punde si punde wakaja FFU...FFU wameshuka kwa gari lao wanamfuata mzee wanamsalimia 'afande'...eeh bhana eeh I wish mgeona sura za wale jamaa wa wrong parking[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]kumbe mzee ni kamanda mstaafu alikuwa na cheo sana......[emoji28][emoji28] vijana wa wrong parking walibebwa na chain zao...
 
[emoji81][emoji81][emoji81][emoji81][emoji81]
 
Mimi kuna jamaa tumesoma wote form 1&2 tulikuwa washkaji maana ndo tulikuwa tunaongoza class
Nikafukuzwa so 3&4 tulikuwa tunakutana likizo tu
Baada tukapotezana Ila me nilikuwa napata data zake alimaliza degree ya mambo ya afya akaingiza jeshi then akapelekwa mondul kusomea sijui vyeo then akapangwa mikoan huko
2020 sm inaita ni jamaa " Flan vip? Za siku niomeambiwa uliacha kazi ya ualim now unapiga umachinga dar? Tuonane basi ndg" ni kweli niliachaga ualim nikajichanganya kariakoo kabla sijatoboa kibiashara ambayo hakuwa anajua kuwa nilitoboa tena kwa kiwango kikubwa
Basi tukakutana Mliman me ndo nilitangulia pale Grano
Jamaa akaja "agiza chochote ntalipa kaka " mbwembwe nyingi
Me na mwili mdogo halaf kwenye uvaaji me ni 0% so ngumu sana mtu kujua huyu yuko vzr au la!
Tukiwa pale dem wangu akaniambia nimfate kazin kumrudisha home alkkuwa mjamzito nikamwambia mshkaji akajibu " haina shida na usafir kaka twende tutamchukua tu nishanunua gari siku hizi mambo yangu fresh "
Nikakubali tukatoka nikamwambia tupite nichukue langu tuongozane ndo anaanza kushangaa " kwan una gari? Machinga ana gari mura au nimedanganywa!?"
Tumefika mzee anaona BIMA imepaki nafungua namwambia twende na hii tukirud tutapitia yako
Jamaa alikosa aman sikujua why ila alikosa aman kabisa
Tumemaliza kule namrudisha Mliman kumbe ana Swift old mole dah jamaa tangu pale alikata mawasiliano mpk leo tunaview tu status
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mtu unayemdharau either Kwa mwonekano au kazi anayofanya .wengi wamebeba vitu unavyohitaji maisha mwako 100%.kama Kuna kitu unakihitaji duniani haijalishi nicha ukubwa kiasi gani basi watu wa Hali hiyo wanajua namna gani ya kukusaidia...

Mimi nilishasaidiwa vitu viwili vikubwa sio vidogo na MUUZA MAJI YA MADUMU anayesambaza kwenye majumba..unaweza kusema mtu huyu atanisaidiaje na Hali yake hii ya chini? Nilidhani mtu anayevaa tai na smart ndio anaweza kunisaidia ..Ukimwona mtu anafanya kazi ya Hali ya chini usimdharau wengi wao huwa pia na michongo mikubwa Sana na wakikupa unatoboa..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom