Ushawahi kufanya roho mbaya ilimradi kuweka jambo fulani sawa?

Ushawahi kufanya roho mbaya ilimradi kuweka jambo fulani sawa?

BoManganese

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2017
Posts
980
Reaction score
2,679
Mambo niaje wanaJF ni matumaini yangu nyote ni wazima na wasio wazima basi twazidi kuombeana.

Basi bila kupoteza wakati sote tunajua katika maisha kuna wakati hutokea tuu inakubidi ubadilike ili kuhakikisha unaweka mambo fulani sawa moja ya mabadiliko ndio mfano kama kufanya ukauzu au kuwa kama una roho mbaya fulani japo inaweza kuwa tabia yako halisi ila kuna sababu tu zinakulazimisha uwe hivyo, naimani hali hii wengi wetu tumeshaipitia.

Mfano mimi mkasa wangu ulikuwa ni miaka fulani hivi kipindi hiko bado niko chalii sasa home kwetu tulipata ugeni na hapo tulikuwa tunaishi mimi, mshua, braza, mama na dada wa kazi kwa hiyo na huyu mgeni pia nae akaongezeka pale. Alikuwa ni binti mzuri tu mtoto wa shangazi alikuja likizo baada ya kumaliza form six sasa pale home mara nyingi sana hakukuwa na watu sababu wazazi wote wanakwenda kazini pia braza anakwenda kwenye mizunguko yake na hata huyu dada wa kazi baada ya kumaliza shughuli zake huwa anakwenda kujifunza ufundi chereani, hivyo mimi baada ya kutoka shule huwa nabaki pekeyangu pale home, sasa baada ya ujio wa huyu binti ndio mara nyingi tukawa tunabaki wawili pale home.

Baada ya wiki chache nikaona huyu binti mtoto wa shangazi kashaanza kuzoea mazingira pale sababu pindi pale home kunapokuwa hakuna watu kuna jamaa alikuwa ana kuja pale huyu alikuwa bwana wake na mtoto wa shangazi so alikuwa anakuja kumnyandua pale pale home. Ile kitu ilikuwa inanikera na kuniumiza sana na mimi ndio nilikuwa mtu pekee nashuhudia. Ile ishu iliendelea hatimae nilishindwa kuvumilia kuona binti mzuri japo mtoto wa shangazi anakuja kunyanduliwa tena home kwetu kabisa.

Sasa nilichokifanya ni kusubiri siku ya yule jamaa kuja, kweli siku akaja akaingia ndani fresh mimi wakati huo nipo uwani jamaa alivyo ingia nikaenda kulock geti la nje kabisa kisha nikaenda kwenye banda la mbwa nikisubiri jamaa atoke. Na niliwaambia kabisa wale mbwa jamaa akitoka wasifanye makosa wamgeuze kitoweo kabisa so baada yule jamaa kumaliza kufanya mambo yake ndani akatoka na mimi nilikuwa nyuma ya nyumba nilivyo sikia hivyo tuu nikafungulia wale mbwa fasta aisee wale madogii walivyo kutana na yule jamaa walimtoa baruu yule sista alikuwa mlangoni fasta akangia ndani akalock mlango na jamaa akakimbilia getini kuhangaika kufungua geti mimi nilishalilock mbwa walimparamia pale lakini alifanikiwa kupata upenyo akachomaka japo aling'atwa alikimbila ukutani jinsi ukuta wetu ulivyo kuwa umejengwa kwa ndani ilikuwa ni rahisi sana kupanda.

So jamaa alipanda hadi juu alijitupa upande wa pili kama gunia nilisikia kishindo tu kwa nje. Kilichobaki pale ni damu damu tuu chini nahisi jamaa alijeruhiwa sana na wale mbwa uzuri wale mbwa tulikuwa tunawapa chanjo so na uhakika jamaa hakupata madhara zaidi ya vidonda tuu. Yule sista alikuja kuniuliza nikamwambia nilikuwa nawapa mbwa maji bahati mbaya wakatoka kwenye banda. Na tangu hapo sikuwahi kumuona tena yule jamaa.

Mnisamehe jamani sijui kufupisha stori.

Vipi upande wenu wakuu jambo gani la roho mbaya uliwahi kufanya ilikusudi kuweka jambo fulani sawa, hebu tiririkeni hapo visa na mikasa.

Karibuni.
 
Unamuonea wivu hata dada yako mkuu? Ulitaka umkate wewe au?
Khaaaaaaah kwahiyo ulitaka uwe nae wee? Makubwa haya lol
Kamati ya roho mbaya..[emoji23]
mkuu huu wivu wakishamba kweli, bora ungemwambia tu huyo dada nawe akakuhudumia
Kwa kweli mi sikuwa na mpango na huyu sista ila kitendo cha jamaa kuja kumnyandulia sista pale pale nyumbani mi nilikuwa naona kama dharau au ni matusi iliniuma aisee...ila ni uchaliii tuu nao[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa kweli mi sikuwa na mpango na huyu sista ila kitendo cha jamaa kuja kumnyandulia sista pale pale nyumbani mi nilikuwa naona kama dharau au ni matusi iliniuma aisee...ila ni uchaliii tuu nao[emoji23][emoji23][emoji23]
Hongera
 
Ila sio poa, ungemtisha kwanza na kakitisho kadogo then ukafata sasa hiyo yama dog.
 
Hauko mwenyewe. Naam, Magufuli na NEC wanafanya hivyo muda huu kwa vyama vya upinzani ili waendelee kutawala.

Jecha, CCM na ZEC walifanya hivyo hivyo mwaka 2015 kule Zanzibar. Walifuta ushindi wa Maalim Seif ili Shein aendelee kutawala!

Binadamu wana sumu kali kuliko ya nyoka.
Mkuu ya ngoswe yatupasa kumwachia ngoswe mwenyewe
 
haikua roho mbaya mkuu... ulitumia maamuzi ya busara sana, maana huto sistaduu alishindwa kupaheshimu na kupathamini hapo kwenu,.. ilifaa na yy umtie adabu..
Kweli mkuu ile dharau nilishindwa kuvumilia
 
Back
Top Bottom