Ushawahi kuhisi upo single ndani ya ndoa?

masai dada

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
16,207
Reaction score
14,343
Heri ya mwaka wandugu.

Ukweli nimeona nije na hii ID kabisa tu maana uchungu nilionao moyoni nahisi kufikia point ya kuhitaji msaada.
Nilikuja na ID hii mamii90 kuomba ushauri tu. Naomba uangalie ule uzi wa familia ya mume ndo utapata muendelezo wa hii.

Watu wengi walionishauri walisema ongea na mume wako moja kwa moja aisee ile siku najuta kwanini niliongea naye kwa uchungu sana, maana aliniambia mama yangu anakuja December kukutoa. Kwa hasira nikamjibu sitoki akasema "Hii nyumba haikuhusu, inamhusu mwanangu" ambaye sio mtoto wangu ni mtoto wake aliyemzaa kabla hatujafunga ndoa.

Ki ukweli roho iliniuma maana hii nyumba pia mimi nilikopa na ni pesa nyingi bado napambana riba. Baada ya ile siku niliona isiwe shida; zile ni hasira nikajirudi maisha yakaenda. Ila katika ushauri pia kuna member aliniambia jitahidi kumuweka karibu na mwanaye huyo (E).

Kweli nikamwambia likizo hii kamlete walau akae wiki kadhaa akamshawishi mama ake kweli mama yake akakubali mtoto akaja. Ki ukweli mtoto ni mtulivu sana, yaani ni rahisi mno kuishi naye. Yaani ni mpole mpaka raha, nilimpendaga tangu hapo lakini ni wa kike.

Sasa wakati amekuja kuna kitanda nilishamuandaliaga siku nyingi ila alitokea mgeni tukakifungua tukakiamishia chumba cha wanaume. Alivyokuja mchana nikamwambia mume wangu nisaidie tuhamishe hiki kitanda chumba cha dada
akajibu haina haja nitalala naye mimi. Kumbuka chumbani kwetu kuna vitanda viwili, kimoja cha mtoto wangu wa 2yrs bado ananyonya so huwaga nanyonyesha namlaza nahamia kitanda kingine, hiki chetu sasa.

Sasa wakati kaniambia vile nikamwambia huyu binti mkubwa hivyo tutalala naye vipi? Anaendea 7yrs. Ki ukweli haikuwa kwa ubaya kabisa ila hata katika hali ya kawaida ni ngumu; alibadilika sura pale ikabidi niwe mpole.

Kweli usiku ukaingia binti akaanza kulala na baba ake kwenye kile kitanda. Usiku wake mpaka niliota mandoto ya ajabu maana nilikuwa nawatizama tu, sikulala ki ukweli.

Ni kama wiki hivi tupo naye. So mimi nina maugwadu kama yote maana wiki ile nilikua period na hii tangu majuzi ndiyo dogo tunapoa naye rum. Mi nikawa namuonesha ishara tuingie hata chooni, anani-ignore.

So jana anacheki mpira watoto wanachenza nje nikamfata nikamwambia twende chumbani nikamwambie kitu, aliniangalia kabisa akagoma. Nikasema ngoja mpira uishe aisee hakuja, niliumia jana sana. Sema nikapotezea kiutu uzima. Ki ukweli dogo huyu wa kike namkubali sana aisee so nikasema ngoja nimute nijikaze mpaka nione mambo yatakavyojipambanua.

Leo asubuhi madogo kama kawa wakaamka wakasepa tukawa tumebaki wawili tu chumbani, akanifata kwenye kitanda changu; ki ukweli sikua hata na hamu kabisa maana nilishaishiwa na nguvu tangu majuzi huko. Nikamwambia tu ukweli tangu juzi nakubembeleza unanitolea nje (kiutani ila siriaz)

Nikamwambia tumuandalie kitanda cha dogo cha pamanent kwa dada maana huwa anakuja weekend sometimes ila huwa halali, ili hili lisitokee. Nikawa naendelea kumwambia, nikamwambia nilim-miss hatari.

Nikiri Mungu ananiona japo nina ID fake niliongea hilo bila chuki yoyote ila bila kutarajia akaniambia "HATAKUJA TENA ILI ASIKUSUMBUE"

Aisee maini yalikatika, daah moyo uliniuma nikakosa hata cha kuongea. Nikamwambia jamani ita hata mtu mzima kweli ni haki wewe kulala na binti mkubwa hivi kitanda kimoja, hakunijibu akaendelea kunipapasa.

Aiseee sikuloa hata chembe, nilikuwa mkavu wakati nina ugwadu kama wa 2wks na hii ni hilo neno liliniumiza sana. Ukicheki huyu binti nampenda namnunuliaga mazaga hadi mama ake ananikubali.

Angaika pale akafanya yake, akaondoka.

Kiukweli nikamtext kwamba najihisi mpweke kwenye hii ndoa.

Pale tuli-exchange texts kadhaa ila nikamwambia najuta kwa nini nilikopa nikaweka katika hii nyumba na siyo kwa sababu ulisema hii nyumba hainihusu, bali ni kwakua sina hata shilingi na unaninyanyasa kihisia namna hii. Akaniambia "Ndiyo nishakwambia haikuhusu, inamuhusu mwanangu mkubwa"

Nikamjibu sasa mimi na mwanangu twende wapi? Akasema omba Mungu nipate hela nitamjengea yeye ila jua hiyo nyumba haiwahusu.

Wakuu, kuna mengi hapo nayaskip, ila hii nyumba nimekopa kiasi cha pesa nikampa bado napambana na riba
Lakini kingine huyu ni mume wa ndoa kabisa.

Nakatwa kiasi kikubwa cha pesa kulipa ule mkopo na nilikuwa na biashara mwezi wa 11 walikuwa wanatengeneza ile barabara pale imeathiri hadi huo mradi. So namtegemea kwa kila kitu kwa sasa. Sitaki kufaiti kwa chochote nahitaji kuanza upya wakuu

Am soo scared nahisi naweza kuumia nikiendelea au kumuumiza mwanangu maana sijawaigi kuona ule upendo wa dhati kwa huyo dogo kutoka kwake japo wanafanana utafikiri wa mama mmoja. Sina namna yoyote ya kuanza upya ila natamani nianze upya niachane na hii nightmare.

Sina mia na sina chochote kile na ndo amepata point ya kunipiga vizuri. Kwa kifupi mwanangu nimepambana naye tangu hajazaliwa; nikielezea hili itachukua mada nzima.

Nimelia mpaka nahisi kuumwa.

Nisaidieni wakuu. Nikiri pamoja na changamoto zote sijawahi msaliti mune wangu hata tone.
 
Kwanza pole sana kwa yanayokukuta lakini pili,ili kufupisha maelezo yasiwe marefu ni wakati wa kuanza upya kabisa mazingira yako yanayokuzunguka anza hata kwa kupika maandazi au chapati kulingana na mahitaji ya eneo lako, ondoa aibu na kila kitu weka pembeni, pale utapoanza kujitegemea kwa kipato chako mwanaume hawezi kukusumbua, mia yako ni bora kuliko mia ya manyanyaso.
 
Pole sana dadangu!

Kuna uzi mmoja unasema wanawake wanapenda kujenga kwa siri! Nafikiri hii ni sababu mojawapo!!

Sasa inabidi usimame mwenyewe, acha hiyo hofu!! Kidogo unachopata kwenye mshahara wako jibane upate mtaji, naamini Mr anawajibika kwenye kulisha familia! Umeshamjua jinsi alivyo, usifanye tena kosa lingine kuwa imara zaidi na mvumilivu kwa ajili yako na mwanao!!

Yakikuzidia fanya venye moyo wako unakusukuma kufanya dear!!

Pole mama, Happy New year dear!!
 
Kazi nafanya ila nakwata almost pesa yote.

Na aliniambia iwe hivyo yeye atakua ananisapoti kw kiasi flan cha pesa ambacho nitakiweka ili nifanye biashara za hapa na pale. Hata hapo ambapo pameharibika kutokana na ujenzi wa barabara nilifaiti mwenye mpaka kupaweka.
 
Ningekua nimesimama kiuchumi hata kesho ningeanza upya.
Inaumiza sana kuishi na mtu asiekupenda ila wewe unampenda ni bora na wewe mapenzi yawe yameshaisha
 
Umeshawambia jamaa zako wanaokuzidi umri na waliopitia mengi?

Wao wamekuambiaje?...

Siwezi kumshauri mtu aiache ndoa yake maana kwenye maisha ups na downs zipo saana. Zinaweza kudumu hata kwa miaka.

Binafsi huwa napenda kuchukulia kila changamoto mtaji. Mwenyezi Mungu anakupitisha katika haya matatizo maana anajua unauwezo wa kudeal nayo...wewe una nguvu za kila aina kudeal na hii issue.

Nitaendelea kusisitiza ongea na wanaokuzidi umri, unaowaamini, wasiwe ndugu wa upande wowote maana watakuwa biased.

Namna nzuri ya kudeal na mtu wa namna hii ignore. Deal naye kisaikolojia yeye anafanya kukukomoa sasa wewe muoneshe haujali.

NB: kipindi unachopitia kwa wanawake ni kibaya saana. Usije ukajaribu kutafuta faraja nje. Faraja ya siku moja inaweza ikaharibu maisha yako yote.
 
Kuwa kwenye mahusiano na mtu mwenye watoto kabla yako ni ngumu sana. Birthday yangu ni New Year, huo mwaka nilichukua holiday kazini nilijua New Year na birthday itakuwa romantic time. Khee nimeambiwa wanakwenda sea side
 
Pole dada....niulize kwanza ndio yule nliyekutana mianzini zanzibar wakati upo internship?....by the way ukitaka kuachana naye kwa huo mzigo haki unayo kwenye swala la kugawana mali.
 
Asante sana..siwezi kutoka nje ya ndoa

Ila sasa unajua binadamu tupo tofauti tulivyoumbwa yaani mimi ni ile type ya siwezi ku ignore kabisa hata kama nikinyamaza nitaingia chumbni na nitalia sana.

I wish niwe na uwezo huo nahisi naweza kusogeza siku mbele maana naona mambo yamenilemea sana.
Ushauri nilimuomba mama yangu ki ukweli huwa anasema nipambanie ndoa ila mimi siwezi kabisa.naona nimeshindwa kuhold on..nazipi kupata maumivu tu kila uchao.
 
Kuwa kwenye mahusiano na mtu mwenye watoto kabla yako ni ngumu sana. Birthday yangu ni New Year, huo mwaka nilichukua holiday kazini nilijua New Year na birthday itakuwa romantic time. Khee nimeambiwa wanakwenda sea side
HBD.

Zawadi uje uchukue nyumbani.
 
Kuwa kwenye mahusiano na mtu mwenye watoto kabla yako ni ngumu sana. Birthday yangu ni New Year, huo mwaka nilichukua holiday kazini nilijua New Year na birthday itakuwa romantic time. Khee nimeambiwa wanakwenda sea side
Kama anakupemda kwa siku moja kumwamcha sio mbaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…