Hii ilimtokea kaka yangu wa tumbo moja atoke yeye ntoke mimi, mtaa wa pili kulikuwa na demu mmoja mfupi,mweusi tii ana macho makubwa yamemjaa usoni, mekundu utafikiri ana red eyes hadi bi mkubwa akawa anamwogopa akawa anasema anavuta bange, kumbe bro alikuwa anapiga bwana, washkaji zake wakamwotea siku moja walishangaaje ukichukulia na mapigo ya yule dem, baada ya kumbana bro akasema anapiga mara moja anasepa.Ule mwaka haujaisha jioni moja tunapokea wageni,wazazi wa yule binti wamekuja kushtaki bro kashamtia mimba, kuitwa jamaa kuthibitisha akakiri ni kweli ye ni mhusika istoshe hadi kadi ya klinic ina jina lake kama baba, daah!! bi mkubwa alichokaje, ikawa haina jinsi, mshua akajitoa kwa maneno mengi makali, ikabidi mzigo tuubebe sisi na bi mkubwa ukichukuli bro hakuwaga na hela kabisa,daah hapo katikati mpaka binti anajifungua yalitokea mambo mengi ya kustaajabisha sometimes hadi nalia nikiyakumbuka..wee acha tu