Wakuu natumaini wote mpo salama na mnaendelea vyema kusherekea sikukuu hizi
Dah, kwa upande wangu mimi sipo sawa kabisa hapa najiona mkosefu sana na sijui hata jamii itanielewa vipi, nimekuja huku naamini kuna wakubwa na watu wenye busara naweza pata ushauri.. Nayopitia kwa sasa na jinsi nilivyokua na mahusiano imara huko nyuma ni mbingu na ardhi. Kisa ni kirefu kiasi chake hivyo naomba muwe wavumilivu
Mikosi ilianza kama miaka 7 iliyopita nikiwa nimemaliza chuo, nilikua na maisha bora sana yasiyo na misukosuko yoyote, nilianza mahusiano na mrembo mmoja tukiwa form four wote sema shule tofauti, yeye akisoma shule ya bweni ya wasichana pekee na mimi kipindi icho niko boarding school boys tupu,
Huyu binti mpaka kumpata nilitumia sana nguvu acha tu hua sitaki hata kukumbuka, ni binti ameshika sana maadili sidhani kama kuna binti wa namna hiyo endelea kufatilia huu mkasa utaelewa kwanini nakuambia hivo....ili iwe rahisi acha tumuite mary japo sio jina halisi ntajitahidi kuficha codes kadhaa
Mary alikua ametoka familia yenye uwezo mkubwa tu sana na yenye maadili mema, mama yake akiwa na wadhifa mkubwa tu serikalini na mzee wake akiwa mfanyabiashara, hatukua majirani bali nilikutana nae shuleni kwao nikiwa nimeenda kuhudhuria mahafali ya dada yangu mkubwa, bado hio siku naikumbuka kama jana kweli mapenzi yana nguvu unaweza kumuona mtu ukakaa wiki nzima bila kumtoa akilini kwako, sikufanikiwa hata kumsemesha hio siku nikawa nimeondoka na mawazo kibao tu huku namuwaza mtu ambae nilikua na imani sitokaa nije nimuone tena maishani..
Basi bana maisha yakaendelea mpaka siku nakumbuka nipo naangalia cd ya graduation ya sister kuna kipande walikua wanaimba madarasa ya chini ndipo nikamuona Mary bana, hapo nilikua nishaanza kusahau kuhusu yeye, nikamuita sister nijajikaza tu nikamuuliza unamjua huyu binti? Akamuangalia akajibu " vipi unamjua kwanini unaniuliza?" Nikamuambia hapana simfahamu ila nakumbuka nilimuona nilivyokuja shuleni kwenu kipindi kile, sister akaniambia anha huyo anaitwa Mary(disguise name) ni mdogo wake na fulani.... Akaniuliza vipi kuna nini...? Nikajibu hakuna kitu kwani wao wanakaa mkoa gani, uzuri akaniambia wanakaa mkoa mmoja na sisi tulipo, hapo mapigo ya moyo yanaenda kasi sana.
Basi kila nikipata muda nikawa namdadisi sister kuhusiana na yule binti mpaka kuna siku sister akaniambia na wewe nimechoka na maswali yako ngoja ntakuombea namba kwa dada yake, baada ya kama siku mbili sister akaja akanipa ile namba hapo nimechanganyikiwa nashindwa hata nianzie wapi,nikaja mtafuta kwa njia ya sms akanijibu nikatumia nguvu sana kujitambulisha uzuri alikua anamjua sister, akawa anakomaa tu anauliza unataka nini toka kwangu nikamuambia tukiwa marafiki itapendeza akanijibu hakuna shaka...
Nikaja kumuomba nimuone kabla shule hazijafunguliwa tukaja kuonana sehemu moja alikuja na mdogo wake ila hatukukaa sana wao wakaondoka,mawasiliano yakaendelea kwa njia ya barua kipindi hicho kishule shule sasa, kufika form 4 ndo nikaja kumfungukia hisia zangu kwake nakumbuka alikua mkali mpaka nusu urafiki ufe, lakini sikukata tamaa mpaka akaja kunikubalia tukawa wapenzi rasmi
Huyu binti alikua na msimamo sana maana hatukufanya chochote mpaka tukaja kumaliza six nakumbuka kwa mbinde nilimvunja usichana hio siku alilia sana akaniomba nisije kuacha kumuoa, kwa uzuri na tabia zake hakika nilishajihakikishia hapa mke nimepata, tukachaguliwa wote udsm hakika nilifurahi sana nikapanga ghetto huko ndo mapenzi yakawa rasmi sasa, jumatatu naenda nae chuo jioni namuacha anakaa hostel za chuo mpaka ijumaa tukitoka tunaenda wote ghetto mpaka jumatatu tena, hakika Mary alikua mzuri sana ndani ya muda watu wengi sana wakawa wanamjua, nakumbuka kuna siku nipo hall kwao tupo room wakaja wadada flani nilikua nasoma nao kozi moja Mary kuwaambia kua mi ni boyfriend wake wale wadada kila tukikutana nae lecture hall wakawa wananiambia we kaka ulimpata wapi binti mrembo vile.
To cut the story short, Mary hakuwahi kuniletea mauza uza yoyote kipindi tupo chuo, na ujinga sikufanya mwingi maana hakuna weekend yoyote ambayo sikua nae, maisha yakaendelea mpaka tukamaliza chuo mi nikapata kazi mwenye government institution moja ofisi zake zipo posta yeye akapata kazi kwenye private firm, after a while tukahamia kwenye nyumba nzima Mungu akajalia tukanunua na usafiri, asubuhi nampeleka job namuacha jioni anatoka anakuja ofisini kwangu ananisubiri mpaka natoka tunaenda wote home maana mi nilikua nachelewa kutoka, sikua na wasiwasi na Mary maana kuanzia chuo alishatongozwa sana na alikua akiniambia tu naomba uniamini siwezi kufanya ujinga
Basi tukaanza kuishi maisha ya Mume na mke rasmi, uzuri kwao wote kasoro wazazi tu ndo walikua hawanijui, na kwetu ivo ivo, tukaanza kabisa na kupanga mipango ya kutambulishana makwetu, dah kumbe bana ukipanga hivi shetani nae anapanga vile, nakumbuka kuna birthday moja nilihudhuria nikakutana na msichana mmoja wa kisomali mixture kidigo alikua anasoma chuo cha uhasibu TIA aisee najuta sana hio siku maana nahisi masaibu yangu yote mpaka leo hii nakula christmas kinyonge ivi yalianzia hapa...
Endelea kunifatilia naandika leo leo hii mpaka iishe hata kama ni saa 7 usiku.