Kingfisher
JF-Expert Member
- May 22, 2015
- 4,740
- 7,679
Kwani saivi una ngapi!?labda kwenye 40's huko
Ila wakinga hawapo hivyo nina experience nao wewe utakua sio wa MaketeSasa hapo cha ajabu nini??
Wewe na viporo wanakuita upashe, kuna mwenzio huku kashaniitia mpk ukoo wao wote na nimegoma.!
Kawajaza pesa wale maanko jau lakini wapi, kanisusia mpk ofisi tulioanzisha wote na kila kitu labda nitakubali lakini hamna kitu.!!
Na sitegemei kumrudia hata mbwa apige mswaki..!
Wewe ungempakua masega au sio?Aisee we mvumilivu sana.
Wewe ungempakua masega au sio?Aisee we mvumilivu sana.
Kauli flani hivi so sadmwanangu asante kwa mjukuu, anza sasa kutafuta mke hapo hamna mke"
hii Ndio unakumbka😐Episode 3
Basi bana maisha yakaendelea vizuri tu huku nipo na Mary tunazidi kupanga mipango ya kimaisha vizuri tu yaani, kwa upande wa Samira sasa sijui wanaume tuna shida gani, ni kama tunapenda challenges flani ivi, yaani ukiona binti hakutaki ndo akili inahamia kwake ukiona anayekutaka sana ndo unakua huna muda nae, ujinga ukaanza kuniingia taratibu nikaanza kumpa ratiba za kazini za uongo mpenzi wangu Mary huku nikijifanya namuonea huruma anavyotoka mapema kuja kukaa kwenye gari akinisubiri mpaka nitoke kazini, mara awe anawahi anakuja hata kunipikia usiku.... Basi tu sababu nyingi maana nikaanza kuona ni kama ananibana yanii, nikamshawishi sana tukaja kununua kagari kadogo used kwa mshkaji wangu tukawa tunamlipa kwa installments, kila mtu akawa na gari lake, hapo ndo nikaanza ujinga rasmi
sasa hapo hawa washkaji kina john wakawa ndo washkaji zangu tukitoka kazini ni kwenda kupiga gambe nikawa mtu wa kurudi home sa tano, Mary mpole kweli hawezi hata kuongea narudi ananipakulia nakula ushahidi tu wala halalamiki, mpaka siku akaanza kunihoji mbona siku izi unakunywa kila siku afu hurudi mapema, nikawa namjibu stress za kazi tu afu ofisini kuna training tunachelewa kutoka ila tunalipwa overtime mke wangu usijali, akajibu sawa mme nakuombea tu....
Mimi sasa ndo nikaanza kuhangaika na Samira, kila nikitoka kazini nampitishia vizawadi, au niwachukue na marafiki zake niwatoe out basi tu yani, siku moja akaniambia patrick unajua nakupenda sana hata marafiki zangu wananiambia you are such a good guy ila naogopa kuumizwa na wewe tena unakunywa pombe sidhani kama tutawezana, nikaanza kumdanganya tu hapa na pale ila kuhusu pombe nikamwambia point blank siwezi kuacha kwanini nikudanganye
Ikaenda enda mpaka akaja kukubali nakumbuka first kiss tulikua coco pale upepo mwanana hapo Mary wangu ananisubiri ndani sikujua hata nilimdanganya nini siku hio maana nilishakua muongo kweli, huku samira nambembeleza tukalale hoteli yeye anakazana nataka nikalale kwako mtu hata sijui unaishi wapi, nikamzuga home kuna wageni tutaenda siku nyingine
Drive ya mapenzi na pombe ni a very bad combination aisee, huku nataka nikalale hoteli kule kwa Mary sijaaga hata wala sina plan yoyote, basi bana ikafika muda hapo simu nimezima tukaenda hoteli na samira mi nawaza tu leo huyu msomali sijui mdigo kazi anayo aisee, tumefika ndani tupo comfartable tu badae kufika kitandani mwenzangu kanibadilikia, akawa haeleweki, mara analia, kuvua nguo hataki yaani nikawa hata simuelewi kabisa, namuuliza kuna shida gani hakuna analosema la maana, kila nikitaka kumvua analia, basi nikatoa begi la kazini nikatoa pc nikaweka movie nikawa nimemkumbatia tunaangalia, alivyorelax kabisa nikamuuliza samira mama kwani kuna shida gani mbona sikuelewi,huku ameziba macho na mikono akaniambia patrick sijawahi kufanya hiki unachotaka kufanya
Aisee akili ikaruka nikawa sielewi, ila moyoni nikasema hapana aisee huyu ananiona wa kuja, alivyo mrembo hivi na hili tako na hii rangi ya mtume wajanja wa dar hawajamuona nikasema patrick acha kujidanganya hapa unachezewa picha la kihindi
ebwanaaa eee gusa achia ubaya ubwelaWazee wa kukodi kwa Majadiliano [emoji23]
Mmh, hongera na pole. Ila ujue Kila mtu anampata wa kufanana nae na kiukweli huyu ndio saizi Yako wale wengine (Mary na Samira) hukuendana nao.S2 episode 9
Mama namjua ni mtu wa maneno mengi nikawa nimempotezea tu mpaka kesho yake nikampigia tukaongea nakamuambia jipangane tu mje mumuone mjukuu sasa akasema hakuna shaka
Baada ya Rachel kujifungua imepita kama wiki 2 ivi kuna siku mama mkwe ananipigia anauliza baba upo wapi namuambia npo najiandaa kutoka kazini hapa akaniambia njoo mara moja kuna shida nyumbani, basi nikatoka haraka nikaenda kufika pale nakuta kama kuna hali ambayo siielewi kama kuna watu watu wengi, nafika nikamvuta mama mkwe pembeni namuuliza nini tena hapa ndo ananiambia kua Rachel anadaiwa na wanakikundi wenzake sijui wameenda dukani kwake wamesafisha kila kitu hapa wapo kwangu wanataka kuchukua tv yangu kwa nguvu, nikachoka kwanza nikauliza kikundi gani hiki, na dukani wamechukuaje vitu mbona pamefungwa yeye mwenyewe ni kama haelewi
Basi nikamuita sijui ndo mkubwa wa kikundi naona wanakuja kama wote nikawapiga biti pale nataka kuongea na mmoja tu, akaja namuuliza mnadai bei gani anadai bado kama laki 6, kutokana na ile hali ya aibu pale nikaingia kwenye gari nikatoa laki 3 nikampa na namba zangu nikamuambia hio nyingine ntakupa kesho, ni kama alitaka kugoma ila kuna jicho fulani nilimkata akapokea hio pesa
Mama mkwe nae akaanza kuniomba msamaha pale ananiambia mwenzako sijui ana shida gani mbona mambo ya aibu haya mwanangu, sikumjibu kitu mi nikaondoka zangu, nikawa nawaza hapa sichezewi michezo ya kiswahili kweli? Hivi kweli ndo nimekuja tengeneza familia na watu kama hawa kweli? Hio siku yalinishinda kuna rafiki yangu mmoja nilimpigia nikamuelezea situation zote aisee mpaka akashangaa, mwishowe akanionea huruma akaniambia tu we angalia jinsi utavyokuja kumpata mwanao basi
Huku maisha yakasonga mi nikawa naenda tu wasalimia pale kwa kina Rachel nawapelekea mahitaji na nini, sasa ikapita zaidi ya mwezi mama na sister wakawa wanakuja mwanza, hapa katikati mahusiano na Rachel ndo yapo ivo ivo sema moyoni nilikua nishamtoa namuwaza mwanangu tu, nikampa taarifa mama mkwe kua amuandae binti aje huku kwangu ila akifika mama amkute nipo nae huku
Sasa sijui ni kiburi au ujinga wa huyu binti, akagoma kutoka kwao akasema watakuja kumsalimia huko huko, hapa nadhani alikua ananikomoa maana baada ya kumlipia lile deni na kuona ameua biashara niliacha kumpa financial favour yoyote, nikawa mme kwa kipemba kila kitu nanunua au namtuma boda, maisha ya kuniomba mara laki laki 2 nikapiga full stop, kwanza nikawa nawaza huyu sina hata malengo nae, hio siku nilichukia nikaenda kwao kufika baada ya maongezi ndo nikawaambia mama na dada wanakuja inabidi mje kwangu sasa, rachel anadai mi siendi kama kunisalimia watakuja huku huku, nikawa nimechukia nikawaambia basi nipeni mtoto wamkute kwangu kama we hutaki kuja baki
Rachel nae sijui ni wehu au nini akaropoka " mtoto mwenyewe hata mahari hujamlipia unaongelea mtoto gani? "
Sijakaa sawa mama yake akanyanyuka akaanza kumpiga huku analia "mwanangu mbona unanitia aibu kiasi hiki una shida gani mbona huniheshimu au mimi sio mama yako, unajua nimehangaika na wewe vipi?"
Nikaona huu ujinga sasa mimi huyo nikaondoka zangu, nikaanza utaratibu mpya, situmi matumizi wala simu zao nikawa sipokei, haikupita siku mama na sister wakaja tukafanya mpango tukaenda wasalimia, sasa sijui kina mama wanakua na nini naona mama akawa busy tu anamkagua mtoto muda tunaondoka akaniambia huyu ni wa kwetu kuna kishimo nimekiona sikioni wanangu wote niliwazaa mkiwa nacho, nikapata faraja kidogo ila hapo bado machale yanacheza tu
Basi kina mama wakawa wanaenda kusalimia huko wanashinda jioni wanarudi kwangu, sister sasa ndo akaanza kunchamba ananiambia mdogo wangu kweli ulimuacha Mary ndo umeanguka huku..... Nakuonea huruma...... Walikaa kama siku 4 wakaaga wakaondoka wakiwa njiani naona sms ya mama "mwanangu asante kwa mjukuu, anza sasa kutafuta mke hapo hamna mke"
SubhanallahMkuu Patrick mimi ntakuwa wa mwisho kukubali kwamba hukumfira
Kudaddadadeek,,🤣Umeyatyampula,🤣S2 episode 3
Mahusiano huku yakawa tofauti sana tu, unajua unapotoka kwenye mahusiano haya mara nyingi tunategemea kukuta yaleyale kwenye mahusiano mapya huku mambo yakawa tofauti kabisa yani, nilishazoea mengi kwa Mary huku ikawa tofauti kabisa, Rachel nilikua nampenda sana na alikua mnyenyekevu sana kwa huo muda ila kosa tulilofanya nadhani tuli move haraka sana kabla hatujajuana vizuri, miezi mitatu tu ya mahusiano mimba tayari ila nikawa naona sawa tu
Katika kitu sikozoea ni kuombwa bills kila siku maana kwao ni kama walianza kumtegemea rasmi, ikiwa kila muda kuna hiki kuna hiki, sio kwamba nilikua sitaki kutoa pesa ila tu kuna usumbufu na ni vitu sikuzoea kabisa, siku nikamuita Rachel nikamwambia hebu tafuta basi biashara nikupe mtaji ufanye kazi sio kila kitu uwe unaomba kwangu, kweli akanipa idea awe anakata nguo za watoto tukatafuta frem tukalipa akawa na goli lake na yeye,
Sasa kuna siku natoka job nikapita hapo golini kwake tukawa tunapiga story mbili tatu mara akaja mdada/mmama yaani ni ile age huelewi yupo wapi hasa, alivyonikuta pale akili ikaanza kubishana nimpe shikamoo au nimsalimie kawaida tu, nikajikuta namuambia "dada habari" kabla hajajibu Rachel ni kama alinisukuma mgongoni akaniambia "salimia vizuri mama huyo" dah nikasema hapo nishayakanyaga nikamuambia mama shikamoo akajibu marahaba mwanangu
akili yangu ni kama iligoma kuendelea kukaa maeneo hayo nikatafuta sababu nikaondoka nikawaacha hapo, ikija kupita kama wiki siku nimetoka kazini Rachel kaniambia njoo utanikuta nyumbani, ile nafika home naingia sebleni yaani nusu nizimie namkuta yupo ndani na mama yake, hawana hata wasiwasi wananikaribisha vizuri tu.... Nikawa nashangaa tu pale nikawasalimu nikaingia chumbani Rachel akanifata, nikaanza kuongea nae taratibu mama yake asiskie hapo nshachukia sana tu nikamuuliza inakuaje kamleta mama yake pale ni mi bado sijaenda kujitambulisha rasmi, akajibu simple tu si mlishakutana dukani, mara mama hana shida tumekua nae kama rafiki yangu tu hua hatufichani kitu
Dah nikatoa excuse pale nimesahau kitu kazini nikaondoka ila nikawa nimechukia sana, nikafika mahali nikakaa nikawa nawaza mmmhhh hapa naenda kuoa kwenye familia gani mbona ni kama hawafati hata maadili ya kiafrica kabisa, au nikawa nawaza huyu mama kutokana na kutomjibu ile sms ameamua kama kuonyesha kutaka kumiliki zone kwa nguvu, maana mpaka anakuja kwangu vile ni kwamba sitakua na option zaidi ya kua na binti yake au kwa lugha nyingine ameamua tutambulishane kwa nguvu tu
Siku zikakata nikaja kumueleza sister yangu mkubwa kua huku nakaa na mtu na nishampa na ujauzito, ila ni kama hakua interested sana na hizo story, kumbuka sister alikua anampenda sana Mary, akaja tu badae my kunijibu " we mambo yako ya mahusiano nimeshakushauri mpaka nikachoka" basi nikamtumia sister namba za Rachel nikamuambia ukipata muda mtafute nae hata hakumtafuta kabisa, huku Rachel nae anasumbua nataka kuongea na wifi sijui nini nikawa namchenga tu maana akili za dada yangu nazijua
Muda hausimami mimba inazidi kua kubwa tu ikabidi nianze kufanya mpango niende kwa kina Rachel rasmi tu nijitambulishe, hapo mzee wangu alishatangulia mbele za haki na mama sikutaka kumpa hizi habari kwa sasa ingawa niliamini dada atakua ashampa umbea, nikaongea na baba yangu mdogo mmoja ni mzee wa mishen town huyu mjanja mjanja akatafuta mzee mmoja ikafika siku tukaenda kwa kina Rachel sasa
Hio siku Rachel anasema kwao mama ndo kila kitu so tutaenda kuongea nae yeye tu wala hataki kuleta watu wengine, basi nikaona kheri itakua rahisi kuliko watu wakiwa wengi tutaanza kusumbuana tu, nikauliza utaratibu wa zawadi tukawa tumenunua, hapo kila kitu cha sherehe maandalizi yote ilibidi mimi ndo nimpe pesa Rachel maana hali ya kwao naijua, ikifika siku sisi hao tukaongozana kwenda sasa, tukiwa njiani ni kama nilihisi kitu nikapita atm nikaongeza akiba niliyokua nimejiwekea nikasema hii itakua emergency tu
Kufika kwao ilikua nyumba ya wapangaji tu,tukapokelewa vizuri na kijana ambae sikumjua hata, ile kuingia nae wote tukabaki tumeshangaa, tulitegemea kumkuta Rachel na mama yake tu kama walivyosema, aisee tukakuta hata wao hawapo kuna jopo la wazee kama 6 wameweka sura za kazi nikasema aisee leo hapa kazi ipo
Blood naelewa Hilo..... 😂Hii stori ilifaa ipewe heading
😅😅 Mi napendelea Story za kimafia.