Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

S2 episode 11


Kurudi sasa maneno hayaishi binti analalamika nashindwaje kumpa hela ya mtaji ila ya kujenga ninayo, hapo hasira zinapanda nawaza nilimfungulia biashara akaiua kwa ujinga wake mwenyewe... mi npo kimya analalamika tu nikawa nawaza hivi huyu najenga yeye analalamika mbona ni mpumbavu sana, basi akaongea we pale maneno ya shombo ikafika wakati nikasema enough is enough, hiyo siku nilimpiga kipigo utasema nampiga mwanaume mwenzangu, binti maneno mengi ila kupigwa muoga nakumbuka alipiga sana magoti ila wapi kipigo kipo palepale, nikampigia mama mkwe simu nikamwambia njoo mfate mtoto wako mi ntamuua huku


uliza kuna nini sikujibu nikakata simu nikaondoka zangu, badae narudi nakuta hawapo na milango hata hawajafunga, chunguza nakuta kabeba karibu kila kitu chake na laptop moja nilikua natumia nyumbani tu, mama mkwe anapiga simu mi sipokei wala nini, ikafika kesho mi kimya tu, mida ya 9 akaja mtu ofisini ananiambia kuna mgeni wako, naenda namkuta mama mkwe tukasalimiana pale akaanza kunihoji baba kulikoni? nikamwambia mwambie binti yako akueleze yeye ndo anajua vizuri, basi akaanza kuongea pale ohh mvumilie tu najua ni mkorofi ila fanya kwa ajili ya mtoto tu sasa, nikamwambia mi nshachoka naomba tuongee muda mwingine nina kazi, akasema sawa akaondoka



Muda wa kusafiri ukakaribia ikabidi nitafute kuna kijana ndugu yangu aje akae pale kwangu, ilivyokaribia muda nikaenda kwa kina Rachel nikawaaga mama mkwe nikamuachia pesa za matumizi kwa ajili ya mtoto kwa huo muda ambapo sipo ikafika tarehe huyo mi nikasafiri zangu


sasa kule njia ya mawasiliano rahisi ni kutumia whatsap, mama mkwe nae mambo ya smartphone hata hayajui ana simu ndogo, Rachel tushagombama hakuna anayemsemesha mwenzake


nimekaa kule vizuri tu nakumbuka muda mwingi nilikua naongea na Mary tu atleast napata amani kidogo, sasa kuna siku naona Rachel kaweka status yupo bar usiku wanakunywa nini sijui wapo na madem flani ivi, nikasema kumekucha hapo namuwaza mtoto tu nasema huyu mtu ataniharibia mwanangu, nikajua huyu anataka attention wala hata sitamtafuta


kama mwezi npo kule nikamtuma yule kijana anayekaa kwangu akanunua simu nakumbuka ya bei ndogo tu smartphone akasajili na laini na kuunga whatsap nikamwambia aende kwa kina Rachel asifanye chochote mpaka niongee na mama yake, kweli nikafanikiwa kuongea na mama yake nikampa maagizo ampe hiyo simu Grace mdogo wake na rachel ili niweze kumonitor hata maendeleo ya mtoto akasema sawa, nilifanya hivo maana kuna kipindi cha nyuma nilitaka kumnunulia mama yake Rachel smartphone akakataa akasema hata hajui kutumia


basi mara nyingi maendeleo ya mtoto nikawa napata kupitia grace akitoka shule, japo alijaribu kumfichia siri dada yake lakini badae nilikuja gundua rachel ameshakua mtu wa viwanja mara nyingi anachelewa kurudi nyumbani, hapo nakumbuka nilikua nawaza sana kuhusu huyu mtu kuniharibia mwanangu


nakumbuka nabakiza kama wiki nirudi huku wakanipa taarifa kua mtoto ameachishwa ziwa, yaani hapo ana kama mwaka na mwezi mmoja na sehemu nikasema tu sawa moyoni nikashukuru maana huyu binti nilikua simuamini kabisa....


kupitia yule kijana nikawatumia pesa tena siku hazigandi training ikaisha nikawa nimerudi
 
Andika ndefu mkuu
 
S2 episode 12


baada ya training kuisha nikarudi, nakumbuka kipindi hicho pesa ilikuepo si haba maana tulijibana na posho tulipewa nyingi ukizingatia maisha yetu ya kibongo, basi nakumbuka nikarudi nikaenda wasalimia na kupeleka zawadi nikaondoka zangu, Rachel akaanza nitafuta mme wangu nakuja tulee mtoto wetu na blah blah kibao nikamwambia we nipe muda ntakuambia, ikapita muda mi kimya tu naenda kuona mtoto naondoka zangu, hapo kuna muda simkuti maana mtoto alishaacha na kunyonya



katika hela nilizobakiwa nazo nikaenda site nikamwaga tofali za kutosha nikaanza kuinua boma taratibu, sasa kuna kipindi Rachel akawa anauliza vipi kuhusu zile m3 nilizokuomba za mtaji mi nikwambia kwa sasa sina pesa nina ujenzi, basi sijui ni hasira au kesho yake akaniambia " kuna mtu kanitafutia kazi geita najiandaa kuondoka na mwanangu"



nikawa nawaza huyu mwanamke mbona kila siku ana jambo tu, lengo lake nipate stress tu au nini, nikampigia namuuliza sawa umepata kazi huko ukienda na mtoto na maisha hata hujaanza huko mtaishi vipi na wapi? akajibu " tutaishi tu mbona mi nilikua bila baba"


basi nikaona huyu mtu ni kama anataka ligi, jioni nikaenda kwao nikamkuta yupo na mama mkwe na grace, yule mdogo wao mdogo wa mwisho wa kiume kuna kipindi baba yake mzazi alikuja kumchukua, basi baada ya salamu na nini mama mkwe nikamueleza kila kitu tukawa kama tupo kikao, nikawaambia mwanangu haendi popote kama wamemchoka nimchukue nimpeleke kwetu maana na kunyonya kashaacha, uzuri huyu mama mkwe nachompenda hakua kabisa upande wa binti yake kwenye mambo ya kipuuzi, mama mkwe akawa mkali sana akasema mtoto haondoki mahali akawa anamwambia mtoto wake kama umepata bwana huko we ondoka ila mjukuu wangu haendi popote, baadae huyu mama akaanza kulia anamuuliza rachel umesahau maisha tulioishi kwanini unajitafutia matatizo bure ni nini ambacho hupati



hapo na mi nina hasira nikamwambia yule mama mtoto wangu nafanya mpango wa kuja mchukue na kuanzia leo mi najitoa ule utambulisho hebu ufate siku huyu akileta mwanamme mwingine we mpokee tu na mahari chukua, mi nikaondoka zangu


kweli bana ikapita muda Rachel akaja kuondoka akaenda geita nilikuja kujua baada ya muda kua alipata mwanamme alikua ana maduara mgodini huko ndo alimtoa huku ila uzuri mtoto alimuacha kwao, Mungu nae ni mpaji mi nikabadilishwa kitengo nikaenda kitengo kingine tulikua tunapata pesa sana nyumba yangu inazidi kukimbia tu moyoni nina amani, kuhusu swala la mahusiano sikua na mahusiano rasmi tena ikawa ndo hivo tena tunatoka kazini tupo na co workers tunaenda viwanja tu, wadada wa kujiliwaza hapa na pale walikuwepo wengi tu hasa hasa wanafunzi wa saut pale



mawasiliano na rachel yatakataa rasmi, nikawa namuambia mama mkwe sasa nitafute mfanyakazi nianze tu kukaa na mwanangu, akawa anagoma ananiambia italeta picha mbaya ukizingatia upo mwenyewe hapo, kumbuka hapa huyu mama kashakua kama mama yangu mzazi haishi kunipigia simu, kila siku ananiambia mwanangu Mungu atakusaidia tu mtoto atakua


Grace nae akamaliza form 4 ndo ikawa muda wote yupo na mtoto maana mama mkwe alipata kibarua mahali, kwa hio muda mwingi ikawa ndo mtu ninayewasiliana nae sana kujua mahitaji na hali ya mtoto na nini japokua karibu kila baada ya siku 2 nilikua naenda kuwaona


sasa kuna kipindi mama mkwe akaanzisha utaratibu, siku za weekend anamtuma huyu Grace wanakuja kushinda huku kwangu ili nipate muda wa kukaa na mtoto, Grace nae atafanya usafi huku, kufua nguo , kupanga vitu na kupika n.k, ye akitoka kazini ndo hua anawapitia wanaenda nyumbani, ikafika mahali wakazoea nawaachia tu funguo hata siku npo kazini watakuja kukaa kwangu badae mama mkwe atawapitia waondoke



nakuja na season 3 sasa ambayo ndo itakua mwisho huku ndo kuna balaa zito, stay tuned
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…