S3 episode 2
nikuaga na tabia moja tu hua nikuona sitaki kujadili mada flani hua sipendi kujibu ni bora nikae kimya tu, so grace wala sikuhangaika kumjibu... siku zinaenda hapo kumbuka grace ndo kila siku yupo nyumbani, atashinda na mwanangu watapika watakaa wote, atafua ikifika jioni mama yake atawapitia wote wataenda kulala, na mi hapo najitahidi sio matunda sio juice sio nyama za kila aina kwenye fridge muda wa kuondoka nawapa uhuru tu bebeni mnachoweza nendeni nacho
basi sijui kwanini ikatokea tu bond sana kati yangu na familia ya kina rachel japokua rachel sina mawasiliano nae hata kidogo, Grace akawa sasa mtoto anaanza kupiga hatua atamrecord atantumia whatsapp hata nikiwa kazini, akianza kujisemesha maneno atamrecord atanitumia tu na ndo ikawa ivo, na mimi nishawazoea kila nikitoka kazini siachi wachukulia zawadi
maisha yakaenda grace nikaanza kumuona ni wa maana sana maana ndo ashakua kama mama wa mtoto wangu, zawadi siachi kumletea kila nikimnunulia kitu d na yeye lazima apate chochote kitu
katika mawasiliano sasa na grace kuna siku washaondoka na mama mkwe wameenda kulala nachat nae sijui nilikua naulizia d(mwanangu sasa) anaendeleaje, hiyo siku tumepita na co workers mahali tunapiga vitu nikamuambia "hivi unajua wewe ndo mama yake na d? unamjua vizuri kushinda mama ake, usije badilika endelea kumpenda ivo ivo"
nae akanijibu usijali shem huyu ni kama mtoto wangu tu, basi bana muda ukazidi kwenda maisha yanaendelea kuna kipindi mama mkwe akapata safari tukakaa kujadiliana nikamwambia hawa waache tu hapa kwangu usiwe na wasiwasi
sasa tofauti kabisa na watu wanavyodhani grace mi nilikua namchukulia sana kama mdogo wangu wala si vingine kabisa hata, maana ndani ya hizo siku ambazo walikuja kulala kwangu(ye alikua analala na mtoto chumba tofauti) kuna siku nilikuja kulala hapa hapa nyumbani na naomi, kufika nauliza kuna chakula basi Grace akaamka akatutengea tukala akaenda kulala na sisi tukaenda kulala
kesho naamka nikamtoa naomi akaondoka narudi ndani si Grace wala mtoto hawapo, kwanza nikapanic, piga simu sana hazipokelewi hapo kumbuka mama mkwe hayupo yupo safari... baadae napata ujumbe kutoka kwa grace
"baba d usijali si tupo huku kwa mama tupo salama"
nikabaki nashangaa kwanini sasa wameondoka bila kuniaga, alafu huyu mbona hajawahi kuniita baba(jina la mwanangu) hata siku moja kila siku ananiita shem