Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

Episode 7

Nikasema hapa ngoja tu nifanye maamuzi kiume, yule dada wa grocery akasema tulia sisi tutaenda kuongea na mdogo wetu Mary we hamtawezana kwa sasa, hapo kumbuka sitaki kushirikisha ndugu kabisa maana mkosaji ni mimi, nikaona sawa nikawanunulia bia pale tukaenda mpaka nyumbani nikawaacha sebleni maana nilikua naogopa hata Mary kumuacha peke yake, nikatoka nikaenda mpaka ofisini nakuta hakuna hata la maana wala sikutafutwa, nikamcheki mshkaji wangu John nikampa mkanda mzima, nikampa na kazi moja Samira akimtafuta amwambie nina msala ofisini akaulizwa aseme hajui ni nini



Nikatoka piga simu kwa samira akaanza nae masikhara mbona simpokelei simu au nina mke mwingine, hapo mi akili haisomi angejua yaani... Nikamwambia skia nina msala ofisini natafutwa hapa nilipo ntakua sipatikani mpaka nijue nafanyaje, akapanic umefanya nini patrick, nikamwambia siwezi kukuambia ila usijali mi mtoto wa kiume ntajua namna ya kumaliza, nikakata simu nika mblock pamoja na marafiki zake wote, mimi huyo mpaka nyumbani


Nafika nakuta Mary yupo na wale masista wanapiga story tu, wadada wanakunywa bia Mary nae wanamshindilia wine tena, nikasema eh kichaa leo kapewa rungu, mke wangu nimemuacha na vichaa... Mimi huyo nikaondoka zangu nikaenda bar nikapiga tungi tena maana kichwa kilikua kinawaka moto balaa


Narudi usiku wale wadada wamehamia grocery na Mary pale, hapo katulia, sikutaka msemesha, badae ndo namwambia twende tukalale kesho kazini akasema sawa, kufika ndani sasa, same old story akaanza kulia tena, unaniuliza unampenda huyo dada, nikamjibu hapana it was just a fling wala siongei nae tena, wapiiiiii..... Ni machozi tu usiku kucha, kesho akagoma kwenda kazini, hapo na mimi namuacha vipi, piga simu kwa supervisor nikampiga sound weee akanipa siku 2, Mary akaingia rasmi kwenye safari ya ulevi sasa, kazi hataki, akawa mtu mwingine kabisa yaani, ikabidi nimchane sister mkubwa akaongea nae sana lakini wapi, sister akanilaumu sana yani


Kazini kwao private hawataki ujinga wakampiga chini hapo ye hata hawazi kabisa, mimi kazini nikawa siendi kila siku natoa sababu mpaka siku nikamfata supervisor wetu nikamueleza kila kitu, jamaa alikua peace sana akaniandikia likizo ya dharura, Mary huku tukaanza kugombana sasa naona kama anajiendekeza, kuna siku nikatishia kumpiga... Big big mistake
 
...
 
Episode 8

Huu msala wote unaendelea hakuna ndugu yake Mary alikua anajua, maana kuna dada yake na kaka yake wote walikua wakiishi dar na tulikua na utaratibu wa kutoka out hata mara 2 kwa mwezi kama familia, hawa wamenijua tangu kipindi iko na walikua wananiamini sana, kwa hiyo Mary nae hakuwaambia kitu akawa awaficha




Basi bana huku kwa Mary tukaanza kukaa kwa hasira maana nimebembeleza mpaka nikachoka, nikamuambia kama huwezi nisamehe tuachane tu sasa kuliko unavyokua hivo, ye yupo kimya tu, ananunua pombe nazimwaga baadae unazikuta tena, nikasema acha nimuache kuliko aanze kuzinywea huko bar watakuja kumbaka bure



Kuna siku sasa nipo sebleni ye yupo zake chumbani( ndo siku nilitishia kumpiga) anakuja sebleni anafungua fridge anachukua wine anarudi chumbani, hapo mi naangalia movie hata siielewi wala nini, nasubiri Mary alewe aanze kulia tu maana ndo yalikua maisha yetu mapya, ishakua jioni sasa ashakunywa sijui vichupa vingapi mpaka hapo


Ghafla huyo kaja kalegea sana yupo na kopo la dawa( tulikua na emergency kit kabatini tunaweka pain killers,dawa za kuharisha, band aids, plaster etc) nikachukua kopo namuuliza dawa zipo wapi, akasema nimezinywa, akaanza kulia kwaheri mme wangu tutakutana maisha majayo, aisee akili ikaruka nikaona hapa naishia segerea mimi, huyu mtu na hizi pombe na hizi dawa hapa hata hospitali sifiki
 
Episode 9

Nikaangalia kwenye fridge kuna maziwa yale ya bakressa ya boksi, nikachukua nampa anywe akakataa, nilikua sijawahi kumpiga Mary hata kofi kuanzia tupo nae ila hio siku alikunywa maziwa kwa kichapo na makofi mengi, hapo nawaza nikimchekea atakufa huyu, akamaliza boksi la kwanza nikamshindilia la pili, aisee alitapika vibaya sana, dawa nzima nzima, zingine zishaanza kua uji uji, hayo ma wine yote, yaani alitapika mpaka majirani wakaja pale...


Tukamtoa nje tukamlaza kwenye upepo, namuangalia hatamaniki nikaanza kutokwa na machozi, that innocent girl namfanya amekua ivi, nikataka mpeleka hospital kuna mzee ni jirani akasema hapana muache tu atakaa sawa, nikaona this is too much, kuficha naficha nini sasa ishakua aibu mtaa mzima, nikampigia dada ake na kaka ake nikawaeleza kila kitu



After a while wakafika wameongozana, dada mtu kuona mdogo wake vile akaanza kulia tu, kaka mtu akantoa pembeni, ananiuliza Patrick mbona hivi mbona tunakuamini sana, dada ake akaingia ndani akamtolea nguo kadhaa wakampakia ivo ivo wakaondoka nae, mimi nae huyo nikaenda bar
 
Kule kwenye ndala zangu tupo episode ya 10A
 
Episode 10

Nipo bar nawaza tu, kwanza ishakua aibu kwa mashemeji, pili bado kuna samira kuna msala kama huu unanisubiri tena,nikasema kazi ninayo, kesho yake nikampigia simu samira hapokei, badae akapokea rafiki yake anasema samira anaumwa sana, mpo wapi anasema hostel... Nikaenda.... Kule kwa mary naogopa hata kupiga simu mashemeji sijui wananichukulia aje,


Kumbe hizi siku nimepotea samira alishafunga sana safari kwenda kwenye lile ghetto lingine, kanitafuta bila mafanikio, mpaka siku majirani wakamwambia hua sikai hapo na wao hata hawajui naishi wapi maana kila nikija hapo nipo na samira sasa, tukiondoka sionekani tena mpaka tuje wote, majirani nyoko😔, samira nae akapanick akawa haelewi anajua naishi hapo siku zote


Nimefika pale nilikaa zaidi ya lisaa hata kunsemesha neno moja aligoma mpaka baadae nikaamua niondoke zangu tu, huku kwa Mary dada angu mkubwa akafunga safari kuja tukae kikao, siku ya kikao tunafanyia nilipokua naishi na Mary wanaongea Mary analia tu, sijui nilishikwa na nini nikasema acha tu mi nimuachie kila kitu Mary mi ntaenda kuanza upya maana naona hawezi kunsamehe huyu akiendelea kuniona atakuja kujiua



Kikao hakijaisha nikaingia ndani, nikasomba vyeti vyangu, begi la kazini, vitu vyangu vidogo vidogo na baadhi ya nguo sikutaka kikao tena nikaondoka zangu.... Kiutani utani tu hivo nikaondoka, nikaenda kule kwenye nyumba ya magendo nikamuita samira akaja, nikasema kuja kuua watoto wa watu kisa nini, amefika nikamueleza kila kitu a to z wala sikumficha kitu, akaanza kulia ananiuliza ulikua na mpango wa kumuacha mkeo au, nikamwambia hapana, aise alilia sana akawa ananiambia usione mpaka umri huu nilikua nimejitunza mimi mpaka ukubwa huu tukirudi nyumbani hua tunakaguliwa na mama mambo ya aibu kabisa, nilipanga nikirudi nikatae tu maana ndo nishafanya sasa, akaniambia najua familia hata ningetengwa ila kwasababu yako niliamua liwalo na liwe, nilikua hata nipo radhi nibadili dini unioe, aisee aliongea sana baadae akaondoka analia tu akaniambia kwaheri Mungu atakulipa
 
Samira naye anakulaani🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…