S3 epi 18
Sasa kufika pale ba mdogo nae mchezo ashausoma, akaanza kulalamika " Hawa watu Wana shida gani lakini, Mzee na wewe ulijichanganya Sana, sijawahi kukutana na familia sio waelewa kiasi hiki" hapo nikamkata jicho Sasa, nikawa namshangaa huyu nae mbona kama anataka kunigeuka tena, hatujashuka pale tukaanza Sasa kushauriana tushuke au twende tu Sasa
Ba mdogo nae Sasa akaniianzishia swaga Sasa pale " mwanangu pambana Sana utafute pesa, umaskini Hauna aibu, Hawa wazee ndo washaona fursa hapa ya kupata chochote kitu, unadhani wangekua na maisha Yao wangehangaika nini na mambo kama haya"
Nawaza pale naona Kuna ukweli ndani yake, tukashuka pale salimiana na wale wazee maana wao wapo nje hapo, wameweka sura za u serious balaa, hapo nawaza Sasa nani kawaita tena Hawa....
Sidhani kama Kuna siku ilikua ya aibu kama Ile, hua sitaki hata kukumbuka, wazee wale wakatukaribisha nyumbani Kwa mama mkwe sebleni hapo tupo, sisi tunawasikilizia tu hatujasoma mchezo.... Kufika ndani Kuna Mzee kaanzisha mazungumzo " karibuni naona mmekuja"
Sasa hapo sielewi, mama mkwe simuoni, nikawaza ameamua huu msala atupeleke kwa wazee tena au, mbona sisi tulikua tumewafata wao na yule mama mwenye nyumba? Tunaangalia na ba mdogo hapo wote code hazisomi.... Hatujaa sawa mara Kuna kijana akaingia akamgeukia ba mdogo akamuambia "mnaitwa huku"
Hapo nimetulia Sasa nawaza hapa nini kinaendelea, ba mdogo kashanyanyuka yeye na wale wazee haziivi kabisa katoka na yule kijana mimi nimebaki hapo, wale wazee wakaanza na mimi Sasa, mara "kijana skia, hakuna kitu kizuri kama kumalizana na wazee, Hawa kina mama wanapenda Sana kuchukulia mambo kiwepesi kesho keshokutwa yatakukuta mambo mazito usijue wapi pa kukimbilia"
Hapo naona kama mbona vitisho tena Hawa, sijakaa sawa ba mdogo kaja kuniita kaniambia "Mzee samahani mara moja" natoka nje ikabidi tutoke kabisa Sasa nje ya nyumba, ba mdogo hapo kashachukia, ananiambia kina mama kule wanatusubiri, huyu mama analalamika Hawa wamekuja kufanya nini na nani kawaruhusu waingie kwake, mi nikawa nishausoma mchezo Sasa, ba mdogo anasema twende tumalizane na Hawa kina mama tukimaliza sisi tuondoke hao wazee wa nini Sasa
Mimi Sasa hapo nawaza mbona aibu sasa hizi, familia gani hawana aibu kiasi hiki, sehemu Moja vikao viwili mbona hiki kitu tofauti na kuona sijawahi hata kukiskia mahali, Sasa Kuna Hali Fulani tu nilikua nimechoka, tangia hili sakata lianze mama mkwe nae Sasa sijui ndo nini akawa ni mtu anashinda amelala kule Kwa yule mama mwenye nyumba, G nae hapa alishaondoka, nikawa namuwazia mwanangu hapo, japo alikua na mdada wa kazi ila nikawa najua Kuna changamoto tu anapitia, hapo nataka hili jambo liishe tu maisha mengine yaanze
Ba mdogo namuambia sasa Hawa wazee tofauti na pesa hakuna wanachotaka, Kwanini tusiangalie namna tumalize hili swala pande zote tulitoka hapa hili swala liwe limeisha kabisa, ba mdogo nae hataki Sasa, akawa anasema " Hawa si unakumbuka mahesabu waliyotupigia, Hawa hata mkikaa kikao mwezi hamuwezi kuelewana"
Tukabishana pale, tumerudi ndani ba mdogo hapo karudi Kwa kina mama mi nikaenda Kwa wale wazee, nafika ikabidi Sasa niwaambie tu ukweli, kua hatuwezi kukaa vikao viwili kuhusu jambo Moja, Kwanini wasiongee na mama mkwe kule kwanza au sisi tuwape muda hili swala wajue wanalimalizaje, wazee nao wanalalamika tu kua huyo mama ni mbishi hataki kuelewa, basi nikawatega pale Kwa kua mama ndo mzazi acha tu tukaongee nae tuskie anasemaje, na wao Sasa Hilo swala hawataki, tumekaa kidogo ba mdogo huyu hapa ananiambia " Mzee hebu njoo basi huku, twende na muda tushachelewa" Kuna mzee Sasa na ye kachukia hapo ananiuliza " hivi kijana huyu umemtoa wapi, mbona Hana adabu kabisa" ikabidi niwatulize pale, aibu naona mimi sijawahi kukutana na upumbavu kama Ile, basi nikatoka kufika kule mama mkwe Kwa mara ya kwanza Sasa ndo tunaongea kuanzia ule msala, ananiambia " hao we achana nao watakusumbua tu, labda kama una pesa za kuchezea" basi nikamwambia maongezi yasiwe mengi maana hata naona amani hakuna hapa, nikaenda kwenye gari nikatoa kiasi tulichokua tumejipanga nikawakabidhi pale nikaacha na ba mdogo wanahesabiana
Hapo nataka nikitoka hapo nisiskie kelele tena kuhusu haya mambo, nikawarudia wale wazee Sasa, tukaongea Sana nikawaambia mama tumeshamalizana nae Salama Cha msingi wao kama wazee watuombee tu sisi watoto wao baraka maisha yaendelee, wapi bana..... Wazee wao wanawaza pesa tu, wakaanza kujiongelesha pale kua tofauti na yote Kuna faini ya ukoo lazima ilipwe, tambiko halikufanywa hivihivi, hapo washaanza kua wapole maana nishawaambia Kila kitu nishalipa kule, wakauliza kiasi nikawaambia mama so yupo tutawaacha myajadili.... Basi wakataka ngombe watatu Kwa ajili ya ukoo sikutaka kubishana Sana nikawaambia Nina uwezo wa wawili, wakaongea pale wakakibaliana, wazee wahuni Hawa hawalazi damu yaani walimtuma mmoja wao nikaenda kumtolea laki6 Kila ngombe laki 3, wakavuta mkwanja pale wakaondoka zao hata Kwa mama kule hawakupita....
Narudi huku sikuona hata haja ya kuwaambia tumemaliza vipi maana ingekua lawama tu, tumeongea pale badae tukaaga tunataka kuondoka yule mama mwenye nyumba akawa anatuambia "muende Sasa mjipange mje mmchukue mwali, huyo ashakua wa kwenu"