S3 episode 15
tukapiga hesabu sasa pale na ba mdogo, Hawa mbona wanatuchanganya, tufanye kipi Sasa, karatu zetu tulishazitupa Kwa wale wazee wao ndo wamalize Kila kitu,huku tena tunaitwa Kwa mama mkwe, tushike kipi, hapo ba mdogo nikamwambia ni Bora nikamsize kwanza mama mkwe maana hata hivo yeye ndo kama atakua na maamuzi ya mwisho, kumalizana na wale wazee bila kufika muafaka na huyu mama Bado itakua kazi Bure tu hakuna la maana tutakua tumefanya...... Hapo namwambia ba mdogo acha niende tu mwenyewe maana tushawakwaza Hawa tukisema tena ndo tunaenda wote wakati mtu kashatuweka wazi kua usije tutazidi kuleta misuguano tu, ba mdogo nae Sasa " Hawa wakijua uko mwenyewe watakusumbua Sana, ndo maana mimi npo huko wajue una mtu nyuma Yako, hakuna Cha kwenda mwenyewe kwanza hatujui wao kule wameandaa safu gani"
Sasa hapo nawaza hata tukienda huko ndo kukutana na kina Rachel hapo Kuna kikao kweli au itakua ugomvi tu na kutiana aibu, G hapo Sasa nasiliana nae na ye Sasa ni kujidekeza tu anajifanya kama yeye ndo ana mawazo kuliko mimi, hapo namtuliza tu mambo yatakaa sawa, nikamwambia mama kaniita anataka nikaongee nae, akawa kama hana amani kabisa akaniambia kua makini tu kaka maana mama nae akishakutana na Rachel huwezi Jua wamepanga wakuitie nini
Kesho imefika tumejiandaa ba mdogo kashajitundika zake suti mimi hapo nimevaa casual tu, ndo tunajiandaa kwenda, Sasa bana wale wazee sijui walikua wanatuona vipi bana, labda walishajadiliana kua tumeyavuruga hivo bila wao hatuna namna tena, au kwasababu hizo pesa za tambiko tulitoa bila hata ku bargain kitu wakaona Hawa tushawashika, imagine hapo wametupigia mahesabu ambayo Kwa akili timamu ni kama hayatekelezeki mtu huwezi kulipa pesa zote hizo, alafu hatujakaa hata siku hio siku tukiwa tunajiandaa wakampigia Simu ba mdogo kua badae wanataka jibu hizo pesa zinawakilishwa lini, ba mdogo anawaambia subiri tujipange jamaa wanamuambia mahesabu tuliyopiga hayana mjadala tunataka mpaka badae mue mmetupa jibu lini hizo pesa zitawakilishwa.....
Hapo ba mdogo amekata Simu namuuliza hivi Hawa watu hata kama ni kupeleka hizo pesa tunapeleka Kwa utaratibu upi Sasa? Tunawapelekea wao? Au mama? Au vipi? Na baada ya hapo nini kinafuata Sasa? Ikabidi awapigie tena, "hizo pesa tukishapanga tarehe sehemu ya kuwasilisha ni kule Kwa mama au?" Ba mdogo anauliza, yule Mzee akaanza kujiuma uma pale Kuna Mzee mwingine nadhani alimpokonya Simu watakua labda walikua wameweka loud speaker.... Huyu Mzee Sasa hapindishi maneno 'hivi nyie kikao mmekaa na sisi, sa ivi mnauliza maswali gani Sasa, hii kesi imeshafika ngazi ya ukoo Kila kitu kinafanyika huku"
Ba mdogo akawaambia ntawarudia, wakasisitiza mpaka badae mue mshasema lini mnakuja..... Tukabaki tunashangaa Hawa mbona Wana haraka hivi....... Ba mdogo nae Sasa anaanza kunipa mbinu za kivita, ananiambia hizo pesa wanazotaja hata taahira hawezi kuzitoa, Hawa ngoja tukiona wanatuletea upumbavu we Kaa kimya endelea kuwasiliana na mwenzako(G) wao waache tuone Sasa watatufanya nini, maana naona washatuona wajinga....
Ikafika muda tumeenda, tukapokelewa pale na kijana mmoja ila tukaelekezwa Kuna nyumba nyingine kubwa ndo tuingie sio upande ule wa wapangaji( Kwa kina Rachel).... Kufika ndani tunamkuta mama mkwe Sasa ametandikiwa mkeka sebleni pale amejilaza yupo na wamama wawili, mmoja sijawahi kumuona na mwingine mtu mzima nishawahi kumuona kama mara 2 japokua hatujawahi kuongea.....
Tukasalimu pale mama mkwe anaitikia kinyonge ni kama vile anaumwa, tukakaribishwa tumekaa pale, badae yule mama wa makamo Sasa( nikaja kujua ndo mwenye nyumba) ndo akaanzisha maongezi, akaanza mbali kweli jinsi wanavyojuana na mama Rachel, alivyowaona Rachel na G wanakua na historia nyingine ndefu ndefu, Sasa akawa anasema kama makosa ndo yashafanyika, maji yakimwagika hayazoleki, akadai amekaa Sana kamshauri mama Rachel hili jambo aangalie namna ya kulimaliza maana linahusisha watoto wake... Basi pale yule mama akaongea maneno mengi tu Sana tukawa tunamsikiza tu
Badae Sasa akanigeukia, kumbe taarifa zote za sisi kukutana na wale wazee, tulivyopigwa faini la tambiko na Yale mahesabu tulivyopigiwa mama mkwe alikua anazo, lakini hakuambiwa na wale wazee sijui hata nani ndo alimpenyezea, Sasa yule mama ndo akawa ananiambia naskia mmeenda kule mmefanya hivi na hivi akanieleza Kila kitu, Sasa akaanza kuniambia, "mwanangu kua makini utapoteza muda wako Bure na pesa zako alafu matatizo yatabaki pale pale, huyu mama tangu namjua ameishi hapa miaka mingi sana tushakua kama ndugu, amelea watoto wake Kwa shida hakuna hata ndugu ashawahi kusogeza mguu hapa kumpa msaada wote, Leo hii watoto wamekua wakubwa ndo wanajifanya kimbelembele ndo waonekane na wao ni wazee wao"
Yule mama akawa anasisitiza niangalie Namna tu ya kujua tunayamaliza vipi huku upande wa mama mkwe maana wale wazee hawana Mamlaka yoyote Kwa Hawa kina G kwanza mama Yao hataki hata kuwaskia, Sasa katika maongezi ndo tukaja kujua kumbe hata Ile million laki 3 tulioacha Ile siku ya faini ya Rachel ilileta shida maana tuliwapa wale wazee kumbe hapo washajiwekea mgao mkubwa( wazee wa fursa)
Ba mdogo nae ni mtu anapenda kurahisisha Sana mambo, akawa anamwambia yule mama Sasa " tumekuelewa ulivyotuambia, na Kwa jinsi nilivyokuona naamini hili swala limeshaisha, labda tu mama mtoto( mama G Sasa) aseme jambo tujue utaratibu ukoje"
Sasa yule mama mwenye nyumba akadakia " huyu mwacheni kwanza naona hata Hali yake sio nzuri ngoja akae sawa tutatafuta siku tuongee"
Hapo mama mkwe kajilaza tu hajatia neno tangia tufike na mimi hapo nipo kimya tu naona mambo sijui ya kuanza kuomba msamaha hapa ni ujinga tu, tukaendelea kuongea pale badae nikatoka nikaenda upande wa wapangaji namkuta dada wa mtoto yupo nje pale namwambia mlete mtoto nimsalimu, ile anaingia ndani namskia Rachel anamwambia " mwambie huyo mtoto anataka kulala" basi yule dada anakuja kuniambia dada anasema mtoto anataka kulala, nikajua tu huyu anataka Shari mi sikusema kitu nikarudi kule ndani.....
Sasa nafika ndani wale wazee nao kumbe wanampigia ba mdogo akawa kama ananionyesha Simu lakini akawa hawapokelei, nao wanazidi kupiga tu mpaka nikawa nawaza huenda Hawa wazee nao wameweka mitego huku wanajua tumekuja huku bila wao, maana walishatuambia tusije huku wao ndo watamaliza mambo yote, au nikawa nawaza huenda Rachel ndo kawaambia maana huyu najua fika hataki suluhu kwenye hili jambo
Badae wakamtumia Sasa ba mdogo sms "nyie si mnajiona wajanja, nadhani mmekosa ukoo wa kuchezea, safari hii lazima tuwafunze adabu" ba mdogo akawa kanipasia Simu nisome, Sasa naye hakujali hata tupo ugenini akajikuta karopoka " Sasa na mimi wananijumlisha tena?"