T 1990 ELY
JF-Expert Member
- Sep 7, 2014
- 12,674
- 29,643
realMamyMsimuliaji uko Vizuri sana tunaenjoy sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
realMamyMsimuliaji uko Vizuri sana tunaenjoy sana
Kazi kweli kweliS3 epi 14
Akili ikanituma hapa nisipanic wala nini, nikatoka nje Sasa, ba mdogo nae Sasa yupo nyuma yangu, nafika nawauliza " vipi tena mbona huku Kuna nini?" Sijakaa sawa Rachel huyo kashanirukia, kanishika akaanza kupiga kelele Sasa " we mwanaume umalaya wako ulishindwa kufanyia kwingine, najuta Sana hata kujujua... Mama anakufa Kwa sababu yako mshenzi wewe"
Sasa katika kitu sipendi ni kushikwa na mwanamke ile kama kibabe, Mila zetu zinakataza kabisa kuanzia tukiwa wadogo baba akikuona umekabwa na mwanamke alafu unashangaa tu lazima badae upigwe bakora, kwetu ilikua marufuku kabisa mwanamke kukukaba, likaja wazo Sasa hapo nIshapata hasira nawaza huyu nimpige kichwa au, ila nawaza kuna shangazi kule, ba mdogo ye ataelewa tu, sijui ba mdogo ni kama alishtuka akaingilia kati haraka, Sasa kelele zile shangazi nae huyu na G washatoka nje.....
Sasa sijui ni hasira au nini, Rachel anaropoka tu " kumbe huyu Malaya wako umekuja kumficha huku(yaani utasema sio mdogo wake)..... Shangazi nae hapo kaanza nyie kwani Kuna nini huku, nikaona Sasa hapa nipo kwangu Hawa wasijaribu kunletea ujinga hapa, kama kuharibu nishaharibu Sana Sina Cha kupoteza tena, Kuna jicho nikamkatia Rachel, uzuri ananijua Kuna siku nilishampiga kama mbwa mwizi, nikamwambia sitaki kelele kwangu, alafu nikamwambia haya mambo wewe hayakuhusu ukitaka kunitafuta nitafute tuongee mambo ya mtoto tu tofauti na hapo acha kuingilia mambo ambayo yamekuzidi uwezo
Tukalumbana pale, shangazi anawabembeleza Kina Rachel waondoke anawaambia ntakuja huko nyumbani tuongee, haikupita muda wakaondoka zao, tunarudi ndani G huyo mpaka chumbani, nafika nakuta analia anasema mimi Bora nijiue tu, hapo nikaona hapa ni kwenda ki askari tu, nikamwambia na we toa ujinga wako hapa, kwanza Simu ipo wapi? Ndo ananiambia hata sijui kuanzia Ile siku mama anachukua, basi nilikua na visimu vidogo ndani nikatoa kimoja na kuna laini nilikua natumia kwenye modem nikamtolea nikampa, Sasa huyu Binti nae alivyo mjinga nae anaanza kunilaumu, eti kwanini nilituma watu kwao bila kumuambia, nikawa namshangaa tu pale maana ye ndo alikua ananitisha kumuambia mama yake
Basi tukarudi sebleni ongea Sana na shangazi pale wakaaga wanaondoka, unajua familia zetu za kibantu lazima hapo utoe posho tu utasingizia hata nauli huwezi kumuacha mtu hivi hivi, tena huyu naona kabisa nimepata mtetezi, G nae nikampa balance kidogo tukaagana wao wakaenda
Ba mdogo nae huku kashaanza kuingiza miss(kuogopa).... Ananiambia Mzee tuwe makini haya mambo mbona kama ni magumu Sana, namwambia Mzee tulia mambo yatakaa sawa tu, siku hazigandi ikafika siku wale wazee wakafanya tambiko lao huko sisi tulitoa sababu kama mia hivi si mimi Wala ba mdogo alijaribu kusogeza pua huko....
Mimi huku G naongea nae tu vizuri, Rachel nae Kila siku atatumia Simu mpya kunitukana nikawa nishamzoea, Sasa wale wazee wakaja kutuita na ba mdogo, ba mdogo akaniambia mwanangu tusiwe mafala Hawa tukutane neutral ground tu( tukatae kwenda kwao) maana huwezi kujua wamejipangaje.... Akawashawishi pale tukutane sehemu nyingine badae wakagoma hapo wanasema hatuna heshima tunawaita mnaanza na kutupangia sehemu ya kukutana
Basi bana Kwa tahadhari Sana tukaja kwenda sehemu waliyotuita, hio siku haikua hata kikao aisee ni kama walikua wanatupa taarifa tu ya walichoamua wao, Sasa hapo nakutana na mahari kwanza Kwa ajili ya mtoto(D), faini ya kumpa ujauzito G, faini ya kuwapa ujauzito mtu na dada yake, faini ya kutokuja kwenye tambiko, faini ya kimila sijui inaitwaje nimesahau jina lake la kilugha, mwisho kabisa mahari ya G..... Ukipiga mahesabu Sasa ndo tukachoka, unajenga ki nyumba kabisa..... Na zote zinatolewa Kwa pamoja hakuna Cha installments Wala nini
Sasa ba mdogo akawauliza vipi mama wa huyu Binti (G) mmemshirikisha na karidhia na haya mnayotuambia? Hapo Kuna kizee kikapanic " sisi ndo Kila kitu, mnatakiwa kufanya Kila kitu tutachosema sisi, hiki kikao mpo na wazee zake wewe unauliza maswali kuhusu mwanamke tena"
Tukaomba tukajipange tukapewa muda zisipite siku 21, tukaaga tukaondoka, njiani ba mdogo ananiambia Hawa wajinga hio Hela si unajenga kabisa ka nyumba kazuri wanatuona sisi mafala sio, alafu Hawa kama hawajamshirikisha mama hamna kitu, tutapigwa hela hapa kesi ibaki pale pale tu.... We si umeona wazee wenyewe wajanja wajanja
Basi sisi hao tukapita zetu bar agiza chakula pale gambe kidogo tunapeana faraja tu, mara sms kwenye Simu yangu namba mpya "mimi mama Yako(mama G Sasa) kesho uje nyumbani ila uje mwenyewe huyo baba Yako asije"
Nikamuonyesha ba mdogo Sasa Ile sms, nae anavyojikuta Sasa, akaniambia waache ujinga hao hakuna movie linachezwa bila sterling kesho mguu Kwa mguu tunaenda wote
Uko sawa brooo,,Yaani kuna watu sijui mnakua na maisha gani? Mimi nimejiunga jf 2012 hii thread ni ya pili kuanzisha, mwaka 2014 nilipandisha uzi hapa Kuna ipads na computer nilikua nauza kipindi hiko Niko chuo, sijawahi kuanzisha thread tena mpaka hii hapa, mpaka Sasa nimeanzisha threads mbili tu
Lakini hilo gap la miaka 10 sijawahi kupitisha siku 3 lazima ntaangalia jf nini kinaendelea, kuna msemo wanasema ukiwa mjanja penda Sana kusikiliza kuliko kuongea
Na ndo maana hua napita tu naona members wanasemaje hata bila ya kucomment
Unavyodai mtu hawezi kukumbuka mazungumzo ya Miaka miwili? Mi nimeweka ya Miaka 7 nyuma......
Navyofanya kuquote ni kama relevance tu lakini si Kila neno Lina asilimia 100 kwenye kumbukumbu, Mzee wangu alifariki kitambo ila mpaka Leo naweza kukaa na ndugu tukakumbushana maneno yake, imepita zaidi ya miaka kumi? Kama huwezi kukumbuka maongezi basic ya watu wako wa karibu ya hata miaka iliyopita sijui nakuweka kundi gani,
Kuna story za mwamba UMUGHAKA nimezisoma zote sijawahi hata kucomment, na nimesoma mpaka mwisho, Kuna watu wengi walimponda Sana wanasema anasimulia uongo, ila kuna mahali alinifurahisha akawajibu "Hawa wanaoniponda ndo Kila saa wanachungulia waone nimeishia wapi"
Kuna story za Analyse nilizisoma mpaka mwisho, ila Kuna story nyingi Sana jf nilianza kuzifatilia ikafika mahali sipati vibe nazo kabisa nikaacha njiani, nyingi tu, ila sijawahi kucomment kuponda story ya mtu nikiona haivutii tena nakaa pembeni maisha yanaendelea...... It's that simple,jf hakuna anayemlipa mwenzake Sasa sielewi we unahisi mimi nafaidika vipi, na mimi ni mzito nimepata pm nyingi tu ila nimejibu mbili tu, Moja Kuna kijana tulikua tunaongea nae kuhusu mambo ya kazi, ya pili Kuna mtu tulikua tunataniana tu na hayupo hata hapa Tanzania, kama nasema uongo naruhusu mtu aje aniumbue
Ukiona unakua na mashaka na kitu kwanini usiachane nacho tu? Kuliko kuanza kulalamika???
Hua mnanishangaza sana
Kwenye hii thread nimejifunza uvumilivu😂...hasa kusubiri hizi episodes za patty.....Zitashushwa Tu😀Saa ngap mkuu muendelezo?
Tena Baba mdogo angekuwa wale wazee ambao wanavaa Barakashia lakini sio waislam 🤣🤣🤣Hii stori ningekuwa na studio ningetengeneza movie Tena series Kali maana tayar stori nzuri ipo ya kuanzidhishia
Huyo baba mdogo kanywa pombe confidence imekuwa high mpk katoka nje ya script 😹Umenikumbusha story ya dj ally b anasema akilewa anajionaga mtu flani Mkubwa,
Ndo kama babaake mdogo Patrick alivokuwa anajiona ukweni ila watu wakilewa sijui wanajionaje😂😂
Naunga mkono hoja,mleta mada atafute director,auze stori,au watengeze MovieHii stori ningekuwa na studio ningetengeneza movie Tena series Kali maana tayar stori nzuri ipo ya kuanzidhishia
Ndiko anakoelekea mbona ni suala la muda tu.!!Hahaha na huo ukaribu bamdogo anaweza mtaka mama rachel
🤣🤣KabisaTena Baba mdogo angekuwa wale wazee ambao wanavaa Barakashia lakini sio waislam 🤣🤣🤣
Pole na songa mbele usiangalie nyumaMapenzi!!
Yamenitesa sana
😀😀😀Kumbe Bado ipoKama ile story yako ilikuwa nzuri sana
Mr Khumbu upo??!😀Boss sasa unazingua. Unaandika fupifupi sana halafu unaishia penye utamu. Hebu gonga ndefu halafu usiishie kwenye utamu.
Balaa hiliNdiko anakoelekea mbona ni suala la muda tu.!!
Laiti tungekuwa wengi tunatuma comment fupi tu tena iseme. " asante nimetuma chochote kitu check sms jina la wakalaLaiti kama member mngekuwa na akili kama zangu kusingejaa comment humu..
Na hakuna haja ya kumpressurize mleta story aendelee just simple en life goes on
Naamini kuna members wengi san wanasoma hii story then wako kimya kwa yoyote anayefatilia hii story kimya kimya like hii comment..
Calmness!!