Ushawahi kujifanya mjuaji ukaja kuumbuka?

Naomba kuuliza.
Shimo la samaki linakuwa namna gani?
 
Nilipokuwa la saba A,mwalimu wa maarifa ya jamii aliomba mtu ajitolee kuandika Notice kidogo kwenye ubao.Kwa kimbelembele changu nikainua kidole juu,nafikiri ili nionekane nimekolea kinidhamu.
Aisee niliandika ubao wote ukajaa,Mwalimu alinisifia sana Mwandiko mzuri.Kuna maeneo yalikuwa yana michoro napanda kwenye kiti.Mkono ulichoka,miguu ikaanza kutetemeka,aisee nikaanza kuhema juu jui na kipindi hicho nilikuwa mfupi,nainua shingo juu,napeleka mkono huko nifikie mwisho wa ubao.Mwalimu alifurahi sana akasema nifute mwanzo nijaze tena atanipa daftari nikaandikie home.
Nilikoma kujikomba,siku ile ubao ulifutwa mara mbili.Nilirudi nyumbani hooi,sikuweza kuandika mkono unatetemeka ubao ulikuwa mkubwa sana.Kuanzia siku hiyo mpaka namaliza mwalimu alinifanya ndondocha lake la kuandika ubaoni.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wakati fulani huko sekondari wakati tunafanya mitihani ya muhula kila tukitoka kwenye paper tunaulizana swali fulani umejibu vipi mimi ndio nakuwa kimbelembele kusema swali lile jibu lake ni hivi na vile,baada ya kumaliza mitihani na yalipotoka majibu mimi nikawa nimedisco wale wenzangu niliokuwa najadiliana nao kila tunapotoka kwenye peper wakatusua.Hapo ndipo nikajiona tumbili
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 

Hii sasa kali 😂
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ningeshaa kama nisingekuta comment yako kwenye huu uzi..
Wewe una matukio mno.. Ukianza na kile kisa cha Baiskeli[emoji3][emoji3]
 
Unaweza endesha gari,Nikajibu ndio mbona naendeshaga sana tu home kwakua kila mtu anajua kwetu magari yapo na tunaonekana tuktoka tukiingia wakaona "labda kweli anaweza",wasichojua n kwamba home ukikutwa tu ndani ya gari umekaa

ni utalambwa stick mpk ukiona gari uwe unalia tu mwenyewe,Basi bana baada ya mimi kujibu "naweza" nikaambiwa chukua funguo Nenda hadi sehemu flani kisha rudi,tuone utachukua dk Ngapi,nikaingia ndani ya gari nakumbuka ilikua ni SUZUKI ESCUDO,nikawasha gari vizuri kbsa(hiyo hainishindi) nikaanza ondoka,Bwana weee sikieni tu

Nilienda Gongesha gari kwenye limti flani huko mbelee,ile kesi ikamfkia mshua bwana wee nilidundwa home bado kidogo nife (sijui ka namm ntampgaga mwanangu vile) sema mshua wangu nae anajua kuonea dagaa sana.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hii nimeipenda kulikp
 
Hii chai mkuuu
 
[emoji23]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nakumbuka ilikuwa kanisani mchungaji katika kutoa neno akaita mtu mbele aje afanye reference katika Bible kwa kuwa mi nlikuwa mbele kidogo chap nikaruka hadi mbele hiyo sehemu ya kusoma nlishaipata tangu mda basi nikasoma baada ya kumaliza kile kipengele ghafla mchungaji akaniambia funua Yoshua sura ya 7 mstari wa 3. Hapo ndo shida nilihangaika pale mbele mara nifunue agano jipya mara agano la kale nikavurugwa kabisa alafu kulikuwa na vile vicheko vya chini kwa chini. Nikamwangalia tu mchungaji nikampa microphone nikarudi kukaa. Haikuisha hata dk 15 nilisepa zangu niliumbuka sana aisee
 
Secondary umedisco? ????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…