Dada alipika wali home nikaukosoa vibaya mno kwa maneno mbofu mbofu tukiwa mezani nkawa nakula huku naongea tu wali m'baya m'baya,,nkawa naelekeza hiki kingefanyika hivi,kingefanyika vile Muda huo mimi tu ndio
natawala maongezi watu wengine mezani wote kimya,nilipomaliza mama akasema kesho
CONTROLA upike wali kisha wewe dada utamsaidia kupika mboga,Kimoyo moyo nikasema ngojea mtajua kuwa mimi ndio mpishi konki
mama alivyotoa maagizo nikaitkia kisha nikasema kesho ntapika mimi,dada akaambiwa akimaliza kupika asigse kitu kingine chochote,basi kidume kesho ikafika nilichokipika Ki ukweli ilibidi nisingizie naumwa tumbo ghafla maana balaa lake nilijua lingekua kubwa
lakini pamoja na kusingizia naumwa,janja yangu mama aliishtukia alisema niitwe kisha nikalazimishwa kula ule wali wengine wote wakanunuliwa kiepe kuku,mimi niliambiwa ule wali wangu uishe Nikiula wiki sawa,nikiula mwezi sawa
ila ole wangu nitupe kile chakula,(bi kubwa angu n mkoloni sana) ki ukweli nilikula ule wali/uji sijui wiki nzima ile mpaka nikamaliza chakula chote,tangia Hapo sijawahi kosoa chakula chochote hata kama n kibaya vipi kapika mama ntilie
nikiona kitu kibaya namezea kimya kimya ila sikosoi mtu na kupitia ile adhabu nilijikuta nampenda yule dada angu kiasi kwamba ikawa nikirudi mahali,nikimkuta jikoni naenda kupka nae.