Mimi maza angu hakua mama wa kuchapa,alikua n mama wa adhabu Nakumbuka zamani alishatukataza kuangalia TV bila yeye kutoa ruhusa,siku hiyo tumezoea mama akirudi si atarudi na Gari atapga Honi tukiskia tutazima tv tutakausha kimya.
huo ndio mtindo wetu tukiskia tu honi piiiii,unakimbia getini kufungua huku nyuma usharudisha kila kitu eneo lake,unasambaza madaftari mezani kuonyesha kwamba ulikua unajisomea,si unajua zileee..
Basi bwana! hiyo siku bi mkubwa gari sijui kaacha wapi "anajua mwenyewe" kaingia kupitia geti la nyuma "anafunguo zake" huku kumbuka tulishakatazwa angalia TV bila ruhusa,basi ghafla bin vuu Mama huyu hapa sebleni,Pale sebule yote inakua ndogo,moment kama hizo huwa naombaga MUNGU aje hata MGENI,ila ndio hivyo haji cha mgeni wala nini
Basi bana baada ya kudakwa tuliulizwa tu swali 1,Nilisema nini? "tukajibu" akatuambia nyie si mnapenda sana TV sasa subirini,Akatoka akaenda chumbani kwake kisha akarudi akaenda Chumba chake cha maombi,Maza angu n maza wa prayer kwa sana "ana chumba chake special hicho" basi akaenda akafungua kisha akachukua TV ya chumbani kwake akaipeleka kwenye ile chumba yake ya maombi.
Alipomaliza akaja seblen ambapo alituacha,akatuuliza tulikua tunaangalia nn? tukamdanganya "tukamtajia limkanda la Yesu" akasema uchukueni nifateni,Tukauchukua ule mkanda tukamfata hadi kwenye chumba chake,akatuingiza akasema sasa ingien mkae humu ndani muangalie huo mkanda mpk mchoke,Tukaingizwa Tukafungiwa.
Kile chumba ni master,Dada wa kazi akaambiwa awe anapika chakula kingi,basi tukiletewa asubuhi msosi mle ndani tunakaa humo ndani mpk usiku muda wakutoka kwenda kulala,Usiku ukfka tunaletewa chakula tule tukmaliza usiku kbsa saa 4 tunafunguliwa tukalale chumbani,asubuhi ikifka tunarudi jela yetu,Ile adhabu ilidumu mwezi mzima wa LIKIZO huwezi amini likizo nazionaga fupi,ila hamna likizo nliona ndefu kama hii tuliiyofungiwa chumba kimoja tunaangalia mkanda wa yesu.
Tangu hapo sijawahi kwenda tofaut na maagizo ya mazaaa,yule mama ana ma adhabu ya JKT Halafu mshua wangu alivyogo boya na yeye hata haingiliagi kesi ambazo mazaa anaishughulikia,mi ananiboaga kweli yani,badala hata antetee et akirud kazini jioni anakuja kwenye ile chumba unamskia anasema "hi my sons" ananiboaga basi tu.