Ushawahi kujifanya mjuaji ukaja kuumbuka?

Tulikua tunaenda Dodoma na coaster tulipofika maeneo ya mbezi kuna dogo akamwambia konda tukifika morogoro naomba uniambie konda kama poa tukafika Kibaha dogo akauliza Moro bado ? Konda akasema bado ,tukafika chalinze dogo akauliza tena ,konda akawa mbogo mixa maneno ya shombo dogo kausha tukifika moro nitakwambia
Basi safari ikasonga baada ya masaa mwili dogo akauliza tena moro bado ? hapo tunaitafuta Gairo konda akasema dah! Moro tushapita dogo , kidume nikageuka mbogo na magwanda yangu ya JKT nikamwambia dereva geuza gari turudi Moro abiria wakamaindi kinoma sema wakiangalia konda kazingua wakiniangalia pia mimi ni mwanausalama halafu mwili jumba niko na wenzangu wawili nimewazid ranks kwashingo upande suka kageuza gari mpaka moro.
Nikamwambia dogo moro ndio hapa ,dogo akasema asante bro akafungua begi lake akatoa chupa ya chai na mkate akaanza kugonga konda akamwambia shuka bas dogo akasema anaenda dom ila mama yake alimwambia akifika moro ndio anywe chai lunch atakula dom, unaambia gari zima macho yenye Jazba, hasira,husda,gubu, nongwa,dharau na uchungu yakaelekezwa kwangu hapo ndio ikabidi nizuge naenda kuchimba dawa nikakimbia nikawatext makamanda mizigo yangu nitaikuta kambini
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Mimi maza angu hakua mama wa kuchapa,alikua n mama wa adhabu Nakumbuka zamani alishatukataza kuangalia TV bila yeye kutoa ruhusa,siku hiyo tumezoea mama akirudi si atarudi na Gari atapga Honi tukiskia tutazima tv tutakausha kimya.

huo ndio mtindo wetu tukiskia tu honi piiiii,unakimbia getini kufungua huku nyuma usharudisha kila kitu eneo lake,unasambaza madaftari mezani kuonyesha kwamba ulikua unajisomea,si unajua zileee..

Basi bwana! hiyo siku bi mkubwa gari sijui kaacha wapi "anajua mwenyewe" kaingia kupitia geti la nyuma "anafunguo zake" huku kumbuka tulishakatazwa angalia TV bila ruhusa,basi ghafla bin vuu Mama huyu hapa sebleni,Pale sebule yote inakua ndogo,moment kama hizo huwa naombaga MUNGU aje hata MGENI,ila ndio hivyo haji cha mgeni wala nini

Basi bana baada ya kudakwa tuliulizwa tu swali 1,Nilisema nini? "tukajibu" akatuambia nyie si mnapenda sana TV sasa subirini,Akatoka akaenda chumbani kwake kisha akarudi akaenda Chumba chake cha maombi,Maza angu n maza wa prayer kwa sana "ana chumba chake special hicho" basi akaenda akafungua kisha akachukua TV ya chumbani kwake akaipeleka kwenye ile chumba yake ya maombi.

Alipomaliza akaja seblen ambapo alituacha,akatuuliza tulikua tunaangalia nn? tukamdanganya "tukamtajia limkanda la Yesu" akasema uchukueni nifateni,Tukauchukua ule mkanda tukamfata hadi kwenye chumba chake,akatuingiza akasema sasa ingien mkae humu ndani muangalie huo mkanda mpk mchoke,Tukaingizwa Tukafungiwa.

Kile chumba ni master,Dada wa kazi akaambiwa awe anapika chakula kingi,basi tukiletewa asubuhi msosi mle ndani tunakaa humo ndani mpk usiku muda wakutoka kwenda kulala,Usiku ukfka tunaletewa chakula tule tukmaliza usiku kbsa saa 4 tunafunguliwa tukalale chumbani,asubuhi ikifka tunarudi jela yetu,Ile adhabu ilidumu mwezi mzima wa LIKIZO huwezi amini likizo nazionaga fupi,ila hamna likizo nliona ndefu kama hii tuliiyofungiwa chumba kimoja tunaangalia mkanda wa yesu.

Tangu hapo sijawahi kwenda tofaut na maagizo ya mazaaa,yule mama ana ma adhabu ya JKT Halafu mshua wangu alivyogo boya na yeye hata haingiliagi kesi ambazo mazaa anaishughulikia,mi ananiboaga kweli yani,badala hata antetee et akirud kazini jioni anakuja kwenye ile chumba unamskia anasema "hi my sons" ananiboaga basi tu.

Hahaaa nimechekaa sanaa
 
Binafsi ninakumbuka miaka ile simu za mkononi zimeingia kabla hazijaenea sana wakati huo kila simu ya mkononi ikiitwa 'mobitel' nilitoka zangu Dar nikiwa naelekea Kigoma kikazi, nikawa nimepitia kwa ndugu yangu flani pale Kahama.

Huyu ndugu yangu alikuwa akimiliki simu hiyo, nilimuomba nipige Kigoma kujulisha juu ya safari yangu yeye akaniambia haina "dola" (wakati huo vocha ilikuwa ikiitwa dola) tulikwenda dukani tukanunua hiyo dola akataka aingize namba za hiyo dola Ila kwa vile simu nilikuwa nimeishika mimi, nilitaka niziingize hizo namba mwenyewe ili asinione mimi ni mshamba (si unajua aliyetokea Dar?) Yeye hakuwa na makuu akanipatia ile 'dola'. Ifahamike kuwa sikuwa nimewahi kufanya kazi hiyo ya kuingiza vocha tokea kuzaliwa kwangu ila nilikuwa nawaona watu wakiingiza namba flani zilizoko kwenye hicho kikadi.

Ndipo nillipoanza kuingiza namba kabla hata sijaikwangua hiyo kadi huku nikiamini niko sahihi. Kumbe zile namba nilizokuwa naziingiza ni zile serial number za vocha. Niliporudia kama mara mbili bila mafanikio ndipo yule ndugu yangu akanistukia akanielekeza kwa kuniambia kuwa ninapaswa kukwangua kwanza ile "dola" kisha ndio niziingize hizo namba. Duu kwa kweli nilipatwa na aibu ya mwaka!
 
Habari zenu wanaJF. Kama kichwa cha habari kisemavyo hapo juu, katika harakati za hapa na pale katika maisha inaweza kutokea situation fulani tuu ukajikuta unajua kitu na kukifanya mbele za watu hatimae unaumbuka hapo ndo unakuja ule msemo usemao "utajua ujui".

Mimi binafsi miaka ya nyuma kidogo nilienda water park fulani hivi kurefresh kuogelea kwenye swimming pools kufika pale nikakuta kuna swimming pools za wakubwa zenye kina kirefu na za wadogo zenye kina kifupi. Sasa sikutaka hata kujiuliza kwanini kule kwenye kina kifupi ndio kuna watu wengi kuliko ile pool nyingine yenye kina kirefu nikaona potelea pote washamba tuu. Kwakweli sikuwa nimewahi kwenda before ndo ilikuwa ni mara ya kwanza ndipo kidume nikajikuta mjuaji kwamba ndio best diver sikutaka kwenda kwenye kina kifupi nikajichanganya kwenye swimming pool yenye kina kirefu na kulikuwa na alert kabisa pale ila mimi nikajiona much know. Basi nikaingia kwenye swimming pool taratibu nikiwa nimejiegemeza pembezoni kabisa huku ukutani nikicheki watu wawili watatu mule wakicheza michezo yao. Sasa sijui ni kitu gani kikanitekenya nikaona ngoja nisogee pale katikati nikajipush kutoka pale pembezoni yaani kama nilitumia nguvu ya ule ukuta kuswim hata pale kati sikufika vizuri nikaanza kuhisi kama navutwa ndani ya maji nikaanza kuvuta picha kwa wale wataalam wanavyo ogelea huwa kuna namna wana piga miguu ndani ya maji wanaelea basi na mimi nikaanza kufanya vile nikawa narudi juu kidogo nikiacha kupiga miguu nazama tena pale kwenye angle ya swimming napaona ila kupafikia ndio ilikuwa shughuli kwangu nilipiga sana miguu nikatumia utaalamu wote niliouona kwenye TV vile wanaogeleaga lakini wapi kupiga kelele za kuomba msaada napo nilikuwa naona aibu. Mwisho wa siku baada ya kutapatapa sana na ukizingatia kwenye angle palikuwa sio mbali basi nikachoka nikajiachia tuu nikawa nazama ndo kama nilikuwa naiona dunia inazunguka nikiwa ndani ya maji huku nikiwa nakunywa vikombe heavy vya maji taratibu kabisa. Wakati naelekea kufumba macho kuiaga dunia kwa mbali nikaona malaika ananipa mkono na mimi nikaona nimpe mkono japo kwa kujikongoja sana huku nikijisemea moyoni Bwana ametoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe, nikampa mkono. Mara ghafla nikaona nimeibuliwa kwa nguvu kutoka ndani ya maji kumbe alikuwa ni jamaa tuu nahisi alikuwa ananichora tuu tangu mda ule natapatapa. Basi akanivuta akanishikisha ile angle aisee niliing'ang'ania kwa nguvu zangu zote huku nikiwa nakohoa nikapanda hadi juu nje ya swimming pool kwa speed ya mwanga nikakaa pembeni nikiwa siamini yaliyo nitokea pale dakika chache zilizo pita huku kwa mbali nikisikia vicheko vya watu ni dhahiri kabisa mimi ndiye niliyekuwa nachekwa maana kwa wakati huo akili haikuwepo kabisa pale.
Nikanyanyuka nikatafuta nguo zangu zilipo nikavaa nikapiga msosi pale fasta nikaondoka zangu home bila hata kugeuka nyuma. Yaani hapo ndio nilijua sijui.

Vipi na nyinyi wadau ni kitu gani ulijifanya mjuaji ukaumbuka hebu tiririkeni hapo hata kama sio wewe lakini ulimshuhudia mtu mwingine,

karibuni.
[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Daah! Nimeshindwa kusoma parefu sana[emoji2297]
 
Zamani sana mid 90s huko. Bi mkubwa alikuwa ananituma kununua mafuta ya taa 5lts kwenye kidumu kwa matumizi ya home. Basi mzeebaba nikawa nanunua 4.5lts ile hela ya nusu lita nachikichia. Basi bana siku ya siku nmepewa hela nikapitia kwanza sehemu nikamega ile hela yangu kama kawaida kabla sijaenda kununua mafuta. Nmeshatafuna vyangu sasa niende kununua mafuta Hamadiii kumefungwa zurura sana nikaenda hadi magomeni hakuna mafuta ya taa kumbe kulikuwa na shortage kidogo. macho yalinitoka nikawa nawaza kichapo tu kwa bi mkubwa ni mkoloni hatari.
Sitahadithia kilichotokea nilivyorudi home
hahah
hapo ndio unajikuta unalala na pesa ya mama na akikuuliza unamwambia nimeambiwa niwahi kesho asubuh nikachukue
 
Binafsi ninakumbuka miaka ile simu za mkononi zimeingia kabla hazijaenea sana wakati huo kila simu ya mkononi ikiitwa 'mobitel' nilitoka zangu Dar nikiwa naelekea Kigoma kikazi, nikawa nimepitia kwa ndugu yangu flani pale Kahama.

Huyu ndugu yangu alikuwa akimiliki simu hiyo, nilimuomba nipige Kigoma kujulisha juu ya safari yangu yeye akaniambia haina "dola" (wakati huo vocha ilikuwa ikiitwa dola) tulikwenda dukani tukanunua hiyo dola akataka aingize namba za hiyo dola Ila kwa vile simu nilikuwa nimeishika mimi, nilitaka niziingize hizo namba mwenyewe ili asinione mimi ni mshamba (si unajua aliyetokea Dar?) Yeye hakuwa na makuu akanipatia ile 'dola'. Ifahamike kuwa sikuwa nimewahi kufanya kazi hiyo ya kuingiza vocha tokea kuzaliwa kwangu ila nilikuwa nawaona watu wakiingiza namba flani zilizoko kwenye hicho kikadi.

Ndipo nillipoanza kuingiza namba kabla hata sijaikwangua hiyo kadi huku nikiamini niko sahihi. Kumbe zile namba nilizokuwa naziingiza ni zile serial number za vocha. Niliporudia kama mara mbili bila mafanikio ndipo yule ndugu yangu akanistukia akanielekeza kwa kuniambia kuwa ninapaswa kukwangua kwanza ile "dola" kisha ndio niziingize hizo namba. Duu kwa kweli nilipatwa na aibu ya mwaka!
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Nikiwa form one Siku moja nilimuomba braza flan pikpik niendeshe nilifanya kama utani tu nikajua ataninyima ila cha ajabu aliniliuliza unaweza kuendesha pikpik? Nikaangalia kulia na kushoto nikaona mademu wananiangalia wanasubiri nijibu, nikaona nikisema sijui nitaaibika nikasema ndiyo naweza jamaa akanipa ufunguo hii hapa..

Kwakua nilikua najua kuendesha baiskel sikuwa na hofu ya control ila hofu yangu ilikua ni kwenye kuondoka ila nikavuta kumbukumbu nikapata idea nikakumbuka siku moja nilimskia braza wangu alikua na pikpik anamfundisha rafk yake kuendesha huku akimwambia vuta mafuta huku unaachia clutch taratibu, bas na mm nikashik clutch nikaweka gia huku navuta mafuta, ile naachia clutch tu chuma ikapaa tairi ya mbele ikatua nikayumba ila sikudondoka lakin niliskia kelele huko nyuma huk moyo unadunda nikaivutia mafuta chuma ikakolea.

Kufika mbele nikakumbua kusimama sijui nitafanyaje ili pikpik isimame nigeuke? Nikakumbuka kuna uwanja flan wa waz wa mpira uko mbele bas nikaenda nikaigeuzia pale bila kusimama, nikawa narud naivutia mafuta kinoma yan chuma iko kibati balaa, nikikumbuka kuna madem wananisubiri wanione bas mzee ndo namwaga moto kinoma, Sasa kimbembe ikawa nimefika pale nilipowaacha wale mademu na jamaa mwenye pikpik dah nikashika cluctch nikaona pikpik ndo inazid kukimbia, Wenge likazid nikaona hapa Sasa sina ujanja sijui kusimamisha baiki na nipo kibati ilibid nielekezee pikpik kwenye nguzo ya umeme, niliipiga ile nguzo nikaona giza nikaskia maskio yanalia ziiiii ile nimepata uwezo w kuona ile pikpik ilikua haifai imepasuka hapo mbele karibu kila kitu

Msala mkubwa sana uliamka nyumban,,, mwsho wa siku wale madem walikuwa wakiniona wananicheka ilikua bonge la aibu
 
ninambuka kitambo nilienda kumtembelea mjomba wangu moro town, kipindi hicho mimi ni mdau sana wa pool table sasa baada ya kufika kuna eneo jirani na hpo tulipokuwa tunakaa kulikuwa na bar na mda wote watu wanagonga kete tuh. nilipokuwa nacheza nao nilikuwa nawabuluza kinoma hadi ikafikia misifa ikazidi nikawa najiita komando
kumbe jamaa wananichora tu hlf kuna mapoti kibao mule na mimi nilizidisha masihara nikikufunga najisia mimi ni komando nimeshindikana kambini uwezi kushindana na mimi, kumbe baadhi ya wajeda wakawa wanaambiana wawe makini pale coz wapo na komandoo kipindi icho mimi sijui chochote.
basi bhn za mwizi 40 siku hiyo sina hili wala lile nipo na stick mkononi nacheza na jamaa hku naleta mbwembwe ghafla nashangaa nimeshikwa begani nikaambiwa samahani braza tunakuomba mara moja...
kilichofata hpo ni maswali yaani swali juu ya swali mala upo kikosi gan, mala intek gani mimi nimetoa macho tuh kumbe jamaa ni makomando na walikuwa wananimaindi ninavyojipa vyeo pale
na kilichonipata siku ile kilinipa ticket ya kuondoka baada kutoka hospital wiki moja mbele, hadi Leo moro napitaga tuh sijawahi patamani coz sio sehemu salama tena kwenye maisha yang.
 
Nikiwa form one Siku moja nilimuomba braza flan pikpik niendeshe nilifanya kama utani tu nikajua ataninyima ila cha ajabu aliniliuliza unaweza kuendesha pikpik? Nikaangalia kulia na kushoto nikaona mademu wananiangalia wanasubiri nijibu, nikaona nikisema sijui nitaaibika nikasema ndiyo naweza jamaa akanipa ufunguo hii hapa..

Kwakua nilikua najua kuendesha baiskel sikuwa na hofu ya control ila hofu yangu ilikua ni kwenye kuondoka ila nikavuta kumbukumbu nikapata idea nikakumbuka siku moja nilimskia braza wangu alikua na pikpik anamfundisha rafk yake kuendesha huku akimwambia vuta mafuta huku unaachia clutch taratibu, bas na mm nikashik clutch nikaweka gia huku navuta mafuta, ile naachia clutch tu chuma ikapaa tairi ya mbele ikatua nikayumba ila sikudondoka lakin niliskia kelele huko nyuma huk moyo unadunda nikaivutia mafuta chuma ikakolea.

Kufika mbele nikakumbua kusimama sijui nitafanyaje ili pikpik isimame nigeuke? Nikakumbuka kuna uwanja flan wa waz wa mpira uko mbele bas nikaenda nikaigeuzia pale bila kusimama, nikawa narud naivutia mafuta kinoma yan chuma iko kibati balaa, nikikumbuka kuna madem wananisubiri wanione bas mzee ndo namwaga moto kinoma, Sasa kimbembe ikawa nimefika pale nilipowaacha wale mademu na jamaa mwenye pikpik dah nikashika cluctch nikaona pikpik ndo inazid kukimbia, Wenge likazid nikaona hapa Sasa sina ujanja sijui kusimamisha baiki na nipo kibati ilibid nielekezee pikpik kwenye nguzo ya umeme, niliipiga ile nguzo nikaona giza nikaskia maskio yanalia ziiiii ile nimepata uwezo w kuona ile pikpik ilikua haifai imepasuka hapo mbele karibu kila kitu

Msala mkubwa sana uliamka nyumban,,, mwsho wa siku wale madem walikuwa wakiniona wananicheka ilikua bonge la aibu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Tulikua tunaenda Dodoma na coaster tulipofika maeneo ya mbezi kuna dogo akamwambia konda tukifika morogoro naomba uniambie konda kama poa tukafika Kibaha dogo akauliza Moro bado ? Konda akasema bado ,tukafika chalinze dogo akauliza tena ,konda akawa mbogo mixa maneno ya shombo dogo kausha tukifika moro nitakwambia
Basi safari ikasonga baada ya masaa mwili dogo akauliza tena moro bado ? hapo tunaitafuta Gairo konda akasema dah! Moro tushapita dogo , kidume nikageuka mbogo na magwanda yangu ya JKT nikamwambia dereva geuza gari turudi Moro abiria wakamaindi kinoma sema wakiangalia konda kazingua wakiniangalia pia mimi ni mwanausalama halafu mwili jumba niko na wenzangu wawili nimewazid ranks kwashingo upande suka kageuza gari mpaka moro.
Nikamwambia dogo moro ndio hapa ,dogo akasema asante bro akafungua begi lake akatoa chupa ya chai na mkate akaanza kugonga konda akamwambia shuka bas dogo akasema anaenda dom ila mama yake alimwambia akifika moro ndio anywe chai lunch atakula dom, unaambia gari zima macho yenye Jazba, hasira,husda,gubu, nongwa,dharau na uchungu yakaelekezwa kwangu hapo ndio ikabidi nizuge naenda kuchimba dawa nikakimbia nikawatext makamanda mizigo yangu nitaikuta kambini
Hizi ni hadithi za vichekesho za dogo anaitwa KIZIBO..
 
Wewe ulikuwa unambeep mtoa roho kwa kutafuta sifa.
 
Kanisaniii...
Watumishi ilitokea wamepungua wawili, basi Father Akaomba yeyote anayejua Kutumikia apite mbele akavae joho, mzee mzima nikapanda madhabahuni nikaingia room nikavaa Joho..

Kwa kufupisha...
Nilichanganya madesa kuanzia kwenye uvaaji, Joho nimegeuza, kola nayo imegeukia mabegani, cheteso nacho hakishikiki, full ku vibrate.
Nikiangalia waumini wanaziba midomo, nikajiridhisha hii ni live nazingua sio kama najishtukia tuu.

kumcheki best yangu, ndio kainama kwenye benchi kwa kukosa nguvu za kucheka, huyu ndio akanipa go ahead kua mzee, toka sasa Utageuza altale kua futuhi, nikaone isiwe tabuu, nikarudi kinyume nyumee...
Nilichomokea mlango ule wa nyuma ya Altale, nikavua joho nikasepa misa ikiwa kati...

Niliacha vicheko na taharuki kwa waumini na Wote pale mbele, na ilikua mtu zaidi ya 200..
Hahaaaa, hiyo halii ishanitokea aisee nashukuru ilikuwa kigangoni[emoji23][emoji23]
 
Nikiwa form one Siku moja nilimuomba braza flan pikpik niendeshe nilifanya kama utani tu nikajua ataninyima ila cha ajabu aliniliuliza unaweza kuendesha pikpik? Nikaangalia kulia na kushoto nikaona mademu wananiangalia wanasubiri nijibu, nikaona nikisema sijui nitaaibika nikasema ndiyo naweza jamaa akanipa ufunguo hii hapa..

Kwakua nilikua najua kuendesha baiskel sikuwa na hofu ya control ila hofu yangu ilikua ni kwenye kuondoka ila nikavuta kumbukumbu nikapata idea nikakumbuka siku moja nilimskia braza wangu alikua na pikpik anamfundisha rafk yake kuendesha huku akimwambia vuta mafuta huku unaachia clutch taratibu, bas na mm nikashik clutch nikaweka gia huku navuta mafuta, ile naachia clutch tu chuma ikapaa tairi ya mbele ikatua nikayumba ila sikudondoka lakin niliskia kelele huko nyuma huk moyo unadunda nikaivutia mafuta chuma ikakolea.

Kufika mbele nikakumbua kusimama sijui nitafanyaje ili pikpik isimame nigeuke? Nikakumbuka kuna uwanja flan wa waz wa mpira uko mbele bas nikaenda nikaigeuzia pale bila kusimama, nikawa narud naivutia mafuta kinoma yan chuma iko kibati balaa, nikikumbuka kuna madem wananisubiri wanione bas mzee ndo namwaga moto kinoma, Sasa kimbembe ikawa nimefika pale nilipowaacha wale mademu na jamaa mwenye pikpik dah nikashika cluctch nikaona pikpik ndo inazid kukimbia, Wenge likazid nikaona hapa Sasa sina ujanja sijui kusimamisha baiki na nipo kibati ilibid nielekezee pikpik kwenye nguzo ya umeme, niliipiga ile nguzo nikaona giza nikaskia maskio yanalia ziiiii ile nimepata uwezo w kuona ile pikpik ilikua haifai imepasuka hapo mbele karibu kila kitu

Msala mkubwa sana uliamka nyumban,,, mwsho wa siku wale madem walikuwa wakiniona wananicheka ilikua bonge la aibu
Dah nimecheka sana!
 
Tulikua tunaenda Dodoma na coaster tulipofika maeneo ya mbezi kuna dogo akamwambia konda tukifika morogoro naomba uniambie konda kama poa tukafika Kibaha dogo akauliza Moro bado ? Konda akasema bado ,tukafika chalinze dogo akauliza tena ,konda akawa mbogo mixa maneno ya shombo dogo kausha tukifika moro nitakwambia
Basi safari ikasonga baada ya masaa mwili dogo akauliza tena moro bado ? hapo tunaitafuta Gairo konda akasema dah! Moro tushapita dogo , kidume nikageuka mbogo na magwanda yangu ya JKT nikamwambia dereva geuza gari turudi Moro abiria wakamaindi kinoma sema wakiangalia konda kazingua wakiniangalia pia mimi ni mwanausalama halafu mwili jumba niko na wenzangu wawili nimewazid ranks kwashingo upande suka kageuza gari mpaka moro.
Nikamwambia dogo moro ndio hapa ,dogo akasema asante bro akafungua begi lake akatoa chupa ya chai na mkate akaanza kugonga konda akamwambia shuka bas dogo akasema anaenda dom ila mama yake alimwambia akifika moro ndio anywe chai lunch atakula dom, unaambia gari zima macho yenye Jazba, hasira,husda,gubu, nongwa,dharau na uchungu yakaelekezwa kwangu hapo ndio ikabidi nizuge naenda kuchimba dawa nikakimbia nikawatext makamanda mizigo yangu nitaikuta kambini
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Wale madogo ambao mlikua mnaangalia porn kwny zile deki za VHS na mara paaaaaap umeme unakatika na haujarudi mpk asubuhi haujarudi mbona siwaoni aisee?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787],nilibeba deki kuipeleka kwa fundi akatoe ule mkanda maana adhabu za mshua zilikua kama Adolf Hitler [emoji1787][emoji1787].
 
Kipindi hiko tumemaliza form 6 tunasubiri matokeo,Likizo ndefu hivyo washikaji kutembeleana ilikuwa kawaida....sasa hiyo siku tuko wawili tunaenda kumcheki jamaa yetu home kwao..Tulifika akatupokea vizuri tuu..sema kuna kazi alikuwa anamalizia ndani kwao hivyo tukabaki sebuleni..Sasa akamuagiza mdogo wake wa kike"wawekee muvi ile waangalie wapoteze muda kidogo mi nakuja mida si mirefu"..Na dogo akasema hii muvi kali sana...mkono wa kutosha...

Tukaoma yes..Akaweka muvi kisha na ye akarudi kuendelea kupika..Ile ameingia jikoni tuu Mzee wao kumbe alikuwepo akatoka kuja sebuleni muvi ndo ilikuwa ndo inaanza...sisi hatuna hili wala lile kumbe muvi inaelezea maisha ya steringi kuwa ni mtu wa bata na mademu...heeeeh ile Mzee anakaa tuu na muvi iko jamaa kamuinamisha demu anampiga paipu halafu na kelele za kutoshaaaaa.mwendo wa sekunde kama 30(ila zilikuwa kama masaa 15).Daaaah rimoti iko mbali na Mzee kakaza tuu anatuangalia Mi nikaona nifuate rimoti nitoe Ile muvi..Mzee akatukazia,acha tuu si ndo mambo mnayoangalia siku hizi...Daaaah nikakomaa nakuitoa asee...

Ndani ya dakika 5 tukaaga kwamba tunaenda asee...mbaya zaidi tunaonekana sisi ndo tumeenda special kw ajili ya yale mambo na mzee alikuwa mbali kujua kuwa si tumewekewa tuu na hatuna hatia..
 
Back
Top Bottom