Ushawahi kujifanya mjuaji ukaja kuumbuka?

Ushawahi kujifanya mjuaji ukaja kuumbuka?

Nakumbuka ilikuwa kanisani mchungaji katika kutoa neno akaita mtu mbele aje afanye reference katika Bible kwa kuwa mi nlikuwa mbele kidogo chap nikaruka hadi mbele hiyo sehemu ya kusoma nlishaipata tangu mda basi nikasoma baada ya kumaliza kile kipengele ghafla mchungaji akaniambia funua Yoshua sura ya 7 mstari wa 3. Hapo ndo shida nilihangaika pale mbele mara nifunue agano jipya mara agano la kale nikavurugwa kabisa alafu kulikuwa na vile vicheko vya chini kwa chini. Nikamwangalia tu mchungaji nikampa microphone nikarudi kukaa. Haikuisha hata dk 15 nilisepa zangu niliumbuka sana aisee
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mchungaji alikuwa na makusudi sana aisee
 
Tulikua tunaenda Dodoma na coaster tulipofika maeneo ya mbezi kuna dogo akamwambia konda tukifika morogoro naomba uniambie konda kama poa tukafika Kibaha dogo akauliza Moro bado ? Konda akasema bado ,tukafika chalinze dogo akauliza tena ,konda akawa mbogo mixa maneno ya shombo dogo kausha tukifika moro nitakwambia
Basi safari ikasonga baada ya masaa mwili dogo akauliza tena moro bado ? hapo tunaitafuta Gairo konda akasema dah! Moro tushapita dogo , kidume nikageuka mbogo na magwanda yangu ya JKT nikamwambia dereva geuza gari turudi Moro abiria wakamaindi kinoma sema wakiangalia konda kazingua wakiniangalia pia mimi ni mwanausalama halafu mwili jumba niko na wenzangu wawili nimewazid ranks kwashingo upande suka kageuza gari mpaka moro.
Nikamwambia dogo moro ndio hapa ,dogo akasema asante bro akafungua begi lake akatoa chupa ya chai na mkate akaanza kugonga konda akamwambia shuka bas dogo akasema anaenda dom ila mama yake alimwambia akifika moro ndio anywe chai lunch atakula dom, unaambia gari zima macho yenye Jazba, hasira,husda,gubu, nongwa,dharau na uchungu yakaelekezwa kwangu hapo ndio ikabidi nizuge naenda kuchimba dawa nikakimbia nikawatext makamanda mizigo yangu nitaikuta kambini
Aiseee!
 
Dada alipika wali home nikaukosoa vibaya mno kwa maneno mbofu mbofu tukiwa mezani nkawa nakula huku naongea tu wali m'baya m'baya,,nkawa naelekeza hiki kingefanyika hivi,kingefanyika vile Muda huo mimi tu ndio

natawala maongezi watu wengine mezani wote kimya,nilipomaliza mama akasema kesho CONTROLA upike wali kisha wewe dada utamsaidia kupika mboga,Kimoyo moyo nikasema ngojea mtajua kuwa mimi ndio mpishi konki

mama alivyotoa maagizo nikaitkia kisha nikasema kesho ntapika mimi,dada akaambiwa akimaliza kupika asigse kitu kingine chochote,basi kidume kesho ikafika nilichokipika Ki ukweli ilibidi nisingizie naumwa tumbo ghafla maana balaa lake nilijua lingekua kubwa

lakini pamoja na kusingizia naumwa,janja yangu mama aliishtukia alisema niitwe kisha nikalazimishwa kula ule wali wengine wote wakanunuliwa kiepe kuku,mimi niliambiwa ule wali wangu uishe Nikiula wiki sawa,nikiula mwezi sawa

ila ole wangu nitupe kile chakula,(bi kubwa angu n mkoloni sana) ki ukweli nilikula ule wali/uji sijui wiki nzima ile mpaka nikamaliza chakula chote,tangia Hapo sijawahi kosoa chakula chochote hata kama n kibaya vipi kapika mama ntilie

nikiona kitu kibaya namezea kimya kimya ila sikosoi mtu na kupitia ile adhabu nilijikuta nampenda yule dada angu kiasi kwamba ikawa nikirudi mahali,nikimkuta jikoni naenda kupka nae.
😂 😂 😂 😂
Umenichekesha sana mdogo wangu, hiyo tabia na My Mom alikuwa nayo, niliwahi pika ubwabwa mbichi nililishwa mpaka nikawa nalia, nikapika ugali mbichi nikalishwa mpaka mdada tuliyekuwa tunaishi naye, akanitetea kwa Mama ndiyo nikaumwaga, nikapika uji una mabonge nilinyweshwa chupa nzima mpaka nikahisi kutapika..!
Namshukuru sana yule mwanamke lakini, maana akili ilinikaa hasa.!!

Kuhusu kuumbuka, siku hiyo nimefika kwa bamdogo ugenini, wakawa wanataka kupika mboga halafu ni tembele, basi nikajitia sogeeni tu mie ndiyo nitapika, nafanya utani pale na mbwembwe kibao wanakaukia kucheeeeka.!
Basii nikawasha zangu jiko la gesi, bwaaana bwaaana.!! Ule mjiko kumbe unazingua bwana haupunguzi moto, yaani sikutoa tembele nilitoa 'rojo la tembele' na imagine limeshika chini,

Niliona aibu, nikawa mpole na ile 'ki-ere-ere' yote ikaniisha, nilishindwa hata kutazama watu usoni, nikajiuliza aliyenituma niseme nitapika hapa ugenini kwa watu ni nani.???
 
Wapi kashata yakheeeeeeeee
 
Mwana kuli find Mwana kuli get😂😂
 
Nilipokuwa la saba A,mwalimu wa maarifa ya jamii aliomba mtu ajitolee kuandika Notice kidogo kwenye ubao.Kwa kimbelembele changu nikainua kidole juu,nafikiri ili nionekane nimekolea kinidhamu.
Aisee niliandika ubao wote ukajaa,Mwalimu alinisifia sana Mwandiko mzuri.Kuna maeneo yalikuwa yana michoro napanda kwenye kiti.Mkono ulichoka,miguu ikaanza kutetemeka,aisee nikaanza kuhema juu jui na kipindi hicho nilikuwa mfupi,nainua shingo juu,napeleka mkono huko nifikie mwisho wa ubao.Mwalimu alifurahi sana akasema nifute mwanzo nijaze tena atanipa daftari nikaandikie home.
Nilikoma kujikomba,siku ile ubao ulifutwa mara mbili.Nilirudi nyumbani hooi,sikuweza kuandika mkono unatetemeka ubao ulikuwa mkubwa sana.Kuanzia siku hiyo mpaka namaliza mwalimu alinifanya ndondocha lake la kuandika ubaoni.
Haha binti phoneix we are together [emoji3]
 
Nimeingia kwenye daladala ilikuwa kituoni inasubiri abiria nakuta wameachia mziki mnene hadi kero.

Basi nikawafokea nyie vipi mbona makelele watu tumechoka bana hebu punguzeni sauti konda akaja juu Nami nikaja juu mara kumi yake wakazima mziki.

Gari limejaa likaondoka konda ameanza kukusanya nauli kujisachi nimesahau wallet.

Nimejisachi kila mifuko yote minne ya suruali na miwili ya shirt mara kumi kumi hamna kitu. Konda akaniwashia moto upya siwezi kujitetea wala kumuambia chochote bahati nzuri akapatikana msamaria akanilipia ila konda alinisema safari nzima.
 
Mimi maza angu hakua mama wa kuchapa,alikua n mama wa adhabu Nakumbuka zamani alishatukataza kuangalia TV bila yeye kutoa ruhusa,siku hiyo tumezoea mama akirudi si atarudi na Gari atapga Honi tukiskia tutazima tv tutakausha kimya.

huo ndio mtindo wetu tukiskia tu honi piiiii,unakimbia getini kufungua huku nyuma usharudisha kila kitu eneo lake,unasambaza madaftari mezani kuonyesha kwamba ulikua unajisomea,si unajua zileee..

Basi bwana! hiyo siku bi mkubwa gari sijui kaacha wapi "anajua mwenyewe" kaingia kupitia geti la nyuma "anafunguo zake" huku kumbuka tulishakatazwa angalia TV bila ruhusa,basi ghafla bin vuu Mama huyu hapa sebleni,Pale sebule yote inakua ndogo,moment kama hizo huwa naombaga MUNGU aje hata MGENI,ila ndio hivyo haji cha mgeni wala nini

Basi bana baada ya kudakwa tuliulizwa tu swali 1,Nilisema nini? "tukajibu" akatuambia nyie si mnapenda sana TV sasa subirini,Akatoka akaenda chumbani kwake kisha akarudi akaenda Chumba chake cha maombi,Maza angu n maza wa prayer kwa sana "ana chumba chake special hicho" basi akaenda akafungua kisha akachukua TV ya chumbani kwake akaipeleka kwenye ile chumba yake ya maombi.

Alipomaliza akaja seblen ambapo alituacha,akatuuliza tulikua tunaangalia nn? tukamdanganya "tukamtajia limkanda la Yesu" akasema uchukueni nifateni,Tukauchukua ule mkanda tukamfata hadi kwenye chumba chake,akatuingiza akasema sasa ingien mkae humu ndani muangalie huo mkanda mpk mchoke,Tukaingizwa Tukafungiwa.

Kile chumba ni master,Dada wa kazi akaambiwa awe anapika chakula kingi,basi tukiletewa asubuhi msosi mle ndani tunakaa humo ndani mpk usiku muda wakutoka kwenda kulala,Usiku ukfka tunaletewa chakula tule tukmaliza usiku kbsa saa 4 tunafunguliwa tukalale chumbani,asubuhi ikifka tunarudi jela yetu,Ile adhabu ilidumu mwezi mzima wa LIKIZO huwezi amini likizo nazionaga fupi,ila hamna likizo nliona ndefu kama hii tuliiyofungiwa chumba kimoja tunaangalia mkanda wa yesu.

Tangu hapo sijawahi kwenda tofaut na maagizo ya mazaaa,yule mama ana ma adhabu ya JKT Halafu mshua wangu alivyogo boya na yeye hata haingiliagi kesi ambazo mazaa anaishughulikia,mi ananiboaga kweli yani,badala hata antetee et akirud kazini jioni anakuja kwenye ile chumba unamskia anasema "hi my sons" ananiboaga basi tu.
 
Habari zenu wanaJF. Kama kichwa cha habari kisemavyo hapo juu, katika harakati za hapa na pale katika maisha inaweza kutokea situation fulani tuu ukajikuta unajua kitu na kukifanya mbele za watu hatimae unaumbuka hapo ndo unakuja ule msemo usemao "utajua ujui".

Mimi binafsi miaka ya nyuma kidogo nilienda water park fulani hivi kurefresh kuogelea kwenye swimming pools kufika pale nikakuta kuna swimming pools za wakubwa zenye kina kirefu na za wadogo zenye kina kifupi. Sasa sikutaka hata kujiuliza kwanini kule kwenye kina kifupi ndio kuna watu wengi kuliko ile pool nyingine yenye kina kirefu niakaona potelea pote washamba tuu. Kwakweli sikuwa nimewahi kwenda before ndo ilikuwa ni mara ya kwanza ndipo kidume nikajikuta mjuaji kwamba ndio best diver sikutaka kwenda kwenye kina kifupi kinajichanganya kwenye swimming pool yenye kina kirefu na kulikuwa na alert kabisa pale ila mimi nikajiona much know. Basi nikaingia kwenye swimming pool taratibu nikiwa nimejiegemeza pembezoni kabisa huku ukutani nikicheki watu wawili watatu mule wakicheza michezo yao. Sasa sijui ni kitu gani kikanitekenya nikaona ngoja nisogee pale katikati nikajipush kutoka pale pembezoni yaani kama nilitumia nguvu ya ule ukuta kuswim hata pale kati sikufika vizuri nikaanza kuhisi kama navutwa ndani ya maji nikaanza kuvuta picha kwa wale wataalam wanavyo ogelea huwa kuna namna wana piga miguu ndani ya maji wanaelea basi na mimi nikaanza kufanya vile nikawa narudi juu kidogo nikiacha kupiga miguu nazama tena pale kwenye angle ya swimming napaona ila kupafikia ndio ilikuwa shughuli kwangu nilipiga sana miguu nikatumia utaalamu wote niliouona kwenye TV vile wanaogeleaga lakini wapi kupiga kelele za kuomba msaada napo nilikuwa naona aibu. Mwisho wa siku baada ya kutapatapa sana na ukizingatia kwenye angle palikuwa sio mbali basi nikachoka nikajiachia tuu nikawa nazama ndo kama nilikuwa naiona dunia inazunguka nikiwa ndani ya maji huku nikiwa nakunywa vikombe heavy vya maji taratibu kabisa. Wakati naelekea kufumba macho kuiaga dunia kwa mbali nikaona malaika ananipa mkono na mimi nikaona nimpe mkono japo kwa kujikongoja sana huku nikijisemea moyoni Bwana ametoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe, nikampa mkono. Mara ghafla nikaona nimeibuliwa kwa nguvu kutoka ndani ya maji kumbe alikuwa ni jamaa tuu nahisi alikuwa ananichora tuu tangu mda ule natapatapa. Basi akanivuta akanishikisha ile angle aisee niliing'ang'ania kwa nguvu zangu zote huku nikiwa nakohoa nikapanda hadi juu nje ya swimming pool kwa speed ya mwanga nikakaa pembeni nikiwa siamini yaliyo nitokea pale dakika chache zilizo pita huku kwa mbali nikisikia vicheko vya watu ni dhahiri kabisa mimi ndiye niliyekuwa nachekwa maana kwa wakati huo akili haikuwepo kabisa pale.
Nikanyanyuka nikatafuta nguo zangu zilipo nikavaa nikapiga msosi pale fasta nikaondoka zangu home bila hata kugeuka nyuma. Yaani hapo ndio nilijua sijui.

Vipi na nyinyi wadau ni kitu gani ulijifanya mjuaji ukaumbuka hebu tiririkeni hapo hata kama sio wewe lakini ulimshuhudia mtu mwingine,

karibuni.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mama yangu alikuwa Ni mkali ,yaani ukizingua unachezea bakora Africa mashariki na kati hazijawahi kutokea....![emoji23][emoji23]

Nakumbuka kipindi nipo form four home kilikuwa na deki yenye upande wa VHS na DVD, ujio wa CD za DVD ukawa ule upande wa VHS hautumiki sana...

Sasa si unajua utundu wa ukijana Tena,nikaunganisha waya waya zile ikawa unauwezo wa kurecord kitu kinachooneshwa kwenye tv,dhumuni Ni kurecord nyimbo channel 5 enzi hizo hata cable ikiwa haijalipiwa tuwetunachek,

Basi ile kitu ikawa Ni tabia natafuta mikanda ya zamani naifuta narecord nyimbo zangu,mwanzoni alipiga mkwara baadae akazoea naona hata yeye akawa anapenda tunaangalia familia nzima maana nakumbuka kulikuwa na mazishi ya kiongozi mkubwa duniani aliomba nimrecodie,ila nilikuwa makini kuchagua mikanda,maana kuna mikanda yake alikuwa anaipenda hagusi mtu

katika kurecord pia tulikuwa na mikanda yetu sisi vijana wakiume tulikuwa tunarecord video za ngono,Kuna channel ilikuwa inapatikana kwenye Cable ikifika usiku inaonesha movie za ngono ,na ile mikanda ilikuwa inafichwa geto,

Sasa bwana Kuna siku mama katoka kuwapokea wageni wametoka kijijini,Sasa usiku baada ya kumaliza kula watu wote tupo sebuleni ,baada ya taarifa ya habari ya ITV kuisha Mimi kiherehere changu nikasema ngoja niweke mkanda wa rose mhando umburudishe mama na wale wageni maana mama alikuwa anampenda kweli

Lahaula mkanda unaanza rose mhando kipande Mara kinakuja kipande Cha ngono,kumbe Kuna mtu alirecord pasipo kujua Ni mkanda wa rose mhando...
Kwanza nilianza kuona Giza sebule nzima,nilikimbia kwenye tv hata sielewi nifanye nn,nilijikuta nimechomoa waya Hadi ukutani...

Bahati nzuri sisi watoto wakiume tulikuwa tunalala nje Basi nilivyotoka sikurudi Tena nyumbani nilisingizia nipo kambini najisomea kwa ajili ya kuanza na mitihani mpk nilivyomaliza form four.....
 
Dada alipika wali home nikaukosoa vibaya mno kwa maneno mbofu mbofu tukiwa mezani nkawa nakula huku naongea tu wali m'baya m'baya,,nkawa naelekeza hiki kingefanyika hivi,kingefanyika vile Muda huo mimi tu ndio

natawala maongezi watu wengine mezani wote kimya,nilipomaliza mama akasema kesho CONTROLA upike wali kisha wewe dada utamsaidia kupika mboga,Kimoyo moyo nikasema ngojea mtajua kuwa mimi ndio mpishi konki

mama alivyotoa maagizo nikaitkia kisha nikasema kesho ntapika mimi,dada akaambiwa akimaliza kupika asigse kitu kingine chochote,basi kidume kesho ikafika nilichokipika Ki ukweli ilibidi nisingizie naumwa tumbo ghafla maana balaa lake nilijua lingekua kubwa

lakini pamoja na kusingizia naumwa,janja yangu mama aliishtukia alisema niitwe kisha nikalazimishwa kula ule wali wengine wote wakanunuliwa kiepe kuku,mimi niliambiwa ule wali wangu uishe Nikiula wiki sawa,nikiula mwezi sawa

ila ole wangu nitupe kile chakula,(bi kubwa angu n mkoloni sana) ki ukweli nilikula ule wali/uji sijui wiki nzima ile mpaka nikamaliza chakula chote,tangia Hapo sijawahi kosoa chakula chochote hata kama n kibaya vipi kapika mama ntilie

nikiona kitu kibaya namezea kimya kimya ila sikosoi mtu na kupitia ile adhabu nilijikuta nampenda yule dada angu kiasi kwamba ikawa nikirudi mahali,nikimkuta jikoni naenda kupka nae.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nakumbuka ilikuwa kanisani mchungaji katika kutoa neno akaita mtu mbele aje afanye reference katika Bible kwa kuwa mi nlikuwa mbele kidogo chap nikaruka hadi mbele hiyo sehemu ya kusoma nlishaipata tangu mda basi nikasoma baada ya kumaliza kile kipengele ghafla mchungaji akaniambia funua Yoshua sura ya 7 mstari wa 3. Hapo ndo shida nilihangaika pale mbele mara nifunue agano jipya mara agano la kale nikavurugwa kabisa alafu kulikuwa na vile vicheko vya chini kwa chini. Nikamwangalia tu mchungaji nikampa microphone nikarudi kukaa. Haikuisha hata dk 15 nilisepa zangu niliumbuka sana aisee
Umezingua ata muislam najua
 
Back
Top Bottom