Ushawahi kujifanya mjuaji ukaja kuumbuka?

Hiyo siikumbuki..Niwekee hapa basi nicheke na mimi[emoji23]
Nakumbuka ile ya Baiskeli tu.
Hata siujui mie niliona hyo story kwenye uzi flani uliotaka watu wataje comment zilizowahi kuwavunja mbavu.

Nakumbuka Saint Anne ndiye aliscreen shot comment ya jamaa na ni kweli nilicheka.
 
'Kuna channel ilikuwa inapatikana kwenye Cable ikifika usiku inaonesha movie za ngono ,na ile mikanda ilikuwa inafichwa geto'.

Hio ni Channel E ya South Africa.
 
Hata siujui mie niliona hyo story kwenye uzi flani uliotaka watu wataje comment zilizowahi kuwavunja mbavu.

Nakumbuka Saint Anne ndiye aliscreen shot comment ya jamaa na ni kweli nilicheka.
Huo uzi naukumbuka.. Ila comment siikumbuki.. ngoja niutafute. Ahsante.
 
hahahaha hii ni kubwa kuliko
 
hahahahahahaha we jamaa ni fala sana
 
Zamani sana mid 90s huko. Bi mkubwa alikuwa ananituma kununua mafuta ya taa 5lts kwenye kidumu kwa matumizi ya home. Basi mzeebaba nikawa nanunua 4.5lts ile hela ya nusu lita nachikichia. Basi bana siku ya siku nmepewa hela nikapitia kwanza sehemu nikamega ile hela yangu kama kawaida kabla sijaenda kununua mafuta. Nmeshatafuna vyangu sasa niende kununua mafuta Hamadiii kumefungwa zurura sana nikaenda hadi magomeni hakuna mafuta ya taa kumbe kulikuwa na shortage kidogo. macho yalinitoka nikawa nawaza kichapo tu kwa bi mkubwa ni mkoloni hatari.
Sitahadithia kilichotokea nilivyorudi home
 
Huyo dogo ni mim hapa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Umenikumbusha nilipokua shule nilikua nikitaka hela ya kufanyia mambo yangu narudi nyumbani natunga TRIP namwambia maza shule tuna TRIP ya kwenda bagamoyo,basi maza anakuuliza sh.ngapi unamtajia "anakupa" imetoka hiyo.

sasa kuna siku nimetunga trip yangu,nikarudi home nikamwambia mama J3 ya tarehe 21 tuna trip kwenda mbuga za wanyama,basi akauliza n sh ngapi,kama kawaida nikataja "nikapewa hela"

kufika ijumaaa ya wiki hii ambayo J3 ijayo ndio ile trip niliyotunga tunaenda,tukatangaziwa kuwa J3 ijayo kuna "kikao cha wazazi" kudadeki,shule niliyosoma huwa vikao vya wazazi taarifa wanapigiwa simu kabisa maana zamani ilikua wazazi wanalalamika hatufikishi barua tunazopewa,kwahyo wakakubaliana Simu zitumike na barua tupewe kwahyo hamna namna mwanafunzi hatofikisha barua,maana usipofikisha barua "mzazi atajua maana kashapewa taarifa kuptia simu.

Basi bwana Ijumaa tulivyotangaziwa vile nikawa nawaza hata nirudi home niseme trip imehairishwa ila sasa nkisema hivyo hela ntarudsha hela gani wakati nishaifanyia mambo yangu.

Nikarudi nyumbani na barua yangu nimenyong'onyea sina nguvu nawaza na kuwazua,ile nafika tu mama ananipokea ananiuliza barua niliyopewa shule,nikatoa nikampa kisha nikaenda chumbani kwangu.

Jumamosi ikafika siku ikaenda haraka haraka mara kuangalia hv tyr usiku ushafka,siku imeisha,jpli ikafka nayo ile siku nilihisi haina masaa 24 nilihisi ina masaa 10 tu maana giza liliingia haraka,usiku wa kuamkia J3 nikawaza na kuwazuaa nafanyaje mimi kesho ntaenda umbuka shule jamani.

Nikapata idea ya kuumwa,mama angu huwa hawezagi fanya chochote kama kaona naumwa basi nikalala hadi asubuhi dada kaja niamsha nikajitia natetemeka sijiwezi,mama akaenda ambiwa akasema hebu amka jikaze twende shule nikakuombee ruhusa nikupeleke hospital (kichwa ikawa inagonga alarm tu) nikaona leo naenda kufa mimi.

nilichofanya baada ya kunywa chai kushiba nikajidumbukiza kidole koooni Nikatoa chenchiiii,ila maza bado kakazana "usijali mwanangu tunaenda shule tukitoka tu nakupeleka hospital" nikaona huyu maza vipi huyu.

tulipokua tunaelekea kwenye gari "nikajidondosha" nikaigiza Nimezimia,pale ndio maza kidogo safari ya shule ikakatika nikabebwa juu juu ingizwa kwenye gari hadi hospital...Daktari kufika sijui kanipima nini et nikiwa nimelala vile vile akasema huyu mbona mzima kabisa hana shida,atakua tu kachoka "akaniamsha" ikabdi tu niamke ntafanyaje sasa.

eti mama angu alivyo na kiherehere akanibeba hadi shule kuwahi kikao "asee". Ila Jamani wapendwa ktk bwana napenda tu niishie hapa kwenye hii story yangu ila fahamuni "janja zangu zote ziligundulika" ile siku nilichokipata n mimi tu na wanafunzi washule ile wanajua "nilikoma" mbona.
 
Hahahaha hahahaha
 
'Kuna channel ilikuwa inapatikana kwenye Cable ikifika usiku inaonesha movie za ngono ,na ile mikanda ilikuwa inafichwa geto'.

Hio ni Channel E ya South Africa.
Sawa sawa, ilikuwa mida flani hv ya hatari
 

Mkuu nimecheka sana, ila hii sio chai kweli hii?
 
Hahah hii umetisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…