Ushawahi kujifanya mjuaji ukaja kuumbuka?

Mimi bwana utoto kabla sijawa na mambo mengi kichwani nilikuwa na akili sana

Kila mtihani ukija napata 98%~100%

Sasa nikawa sioni umuhimu wa kwenda shule.Nabeba zangu nguo za nyumbani kwenye begi naenda zangu beach kwa hela ya shule kupunga upepo,huku nakula madafu enzi hizo dafu sh 150/-

Dingi akastukia mchezo baada ya kukutana na mwalimu ambaye anamfahamu basi wakaanza kupiga story,ticha akamwambia mwanao haji shule anakuja siku za mitihani tu anafaulu anapotea au ndo unamfundisha mwenyewe nyumbani???

Mzee akasema hapana ila kesho nitakuja nae mwenyewe basi baba kesho yake akanichukua mguu kwa mguu hadi shule ...

Basi ile paledi asubuhi uwanjani pale wanafunzi wa madarasa yote wapo ndo baba akanishika mkono mnamjua huyu wanafunzi ndiooooooooooo ni nani “ni flaniiiiiiii” basi baba akasema na mchapa mbele yenu sababu haji shule mpk siku za mitihani na nyumbani anaaga anaenda shule.nakumbuka nilikuwa std 5.

Nilikula stick kama 20 hivi watu wote wanacheka mpaka yule ticha ndo akaanza kumpooza dingi.

Tokea siku hiyo sikuwa na amani kabisa pale shule na kwanza shule sikuwahi kuipenda tena hadi namaliza form 6 mimi sikuwa mtu wakupenda shule kabisaaa ni zile akili zangu za kudunduliza zilizosalia ndo zilikuwa zinafanya navuka kila stage bila kukwama.

Nahisi kuna Doa ,dingi aliliweka maishani mwangu.Wazazi tuwe makini na adhabu za kudhalilisha watoto[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Nimekua saivi deep down naogopa sana kulea mtoto hasa kumjenga mtoto kihisia.Nawaogopa sana watoto na hapo hapo nawaheshimu sana watoto ukinikuta naongea na mtoto ni kama mtu mzima mwenzangu jinsi navyomuheshimu nahisi hii nilinyimwa mimi.
 
Chai
 
chai
 
Niliwahi kujifanya mjumbe miaka ya 90, aiseeeh kilichonipata ni siri yangu.
 
Hii stori nimeishawahi kuisikia humu ila umeiedit kidogo...
 
Mimi hapo zamani nilijifanyaga usalama wa taifa kumbe wale naowatambia ndio wazee wenyewe dahh walikuwa wanacheka kweli ila mwishoe nilijua Ila walinionya kwa usalama wangu nisipende kufanya nilivyofanya ile bar ndio ilikuwa mwisho wng kwenda.

Nyingine kuna mshkaji wng mmoja kitambo iko niliwahi kusoma nae kitambo iko academy flan sas tulipotezana kwa muda siku tumeonana alikuwa na wana mabishoo km wawili iyo siku bana nilikuwa gari ya mshkj wng nilivyokutana na mwamba siunajua mambo ya kuvimba tena nikaanza kupiga ngeli na mshkj yes no nyng wale wadau pemben wametulia tuu Wana smile kwa mbali nishapiga mkorogo broken za kutosha ili niwatambie wana apo tupo kweny ndinga. Bana Bana wale wadau wawili si wakaanza kuongea unaijua American English ya ma black yenye slain ya kihuni kumbe wajuba hawajui ata kiswali ni wabongo waliozaliwa USA bongo ndio first time yani. Mzee baba nilijiskia nishai kinoma mzee baba. Sema wao walichukulia poa tuu ila mm nilijishtukia sanaa
 
Dah umenikumbusha nilikuwa redio flani Kuna jamaa namfaham kitambo Sana nikamuona mazingira hayo bwana we ziakanza salamu maraa pap kaongea ngeli nikasema alaaa usinidharaulishe na mi nikakirwanga af pembeni kulikuwa Kuna watu wakubwa tu na elimu zao.

Baada ya mazungumzo mtu pembeni akaniita akanambia mbona mbona umeongea broken Sana vp dah mwanangu Domo lilinishuka macho Kama vile yanataka kudondoka ili nibidi niwe mpole coz alinichambuaa... Ile moments sitaisahau
 
 
Hahaaa nimechekaa sana ww ulizingua pakubwa kugeuza nguo
 
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…