Mnazareth
JF-Expert Member
- Dec 4, 2017
- 3,474
- 7,404
Hii story nimeshahadithiwa na wengi huku mtaani.Mkuu nimecheka sana, ila hii sio chai kweli hii?
Ni chai bila shaka
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii story nimeshahadithiwa na wengi huku mtaani.Mkuu nimecheka sana, ila hii sio chai kweli hii?
ChaiTulikua tunaenda Dodoma na coaster tulipofika maeneo ya mbezi kuna dogo akamwambia konda tukifika morogoro naomba uniambie konda kama poa tukafika Kibaha dogo akauliza Moro bado ? Konda akasema bado ,tukafika chalinze dogo akauliza tena ,konda akawa mbogo mixa maneno ya shombo dogo kausha tukifika moro nitakwambia
Basi safari ikasonga baada ya masaa mwili dogo akauliza tena moro bado ? hapo tunaitafuta Gairo konda akasema dah! Moro tushapita dogo , kidume nikageuka mbogo na magwanda yangu ya JKT nikamwambia dereva geuza gari turudi Moro abiria wakamaindi kinoma sema wakiangalia konda kazingua wakiniangalia pia mimi ni mwanausalama halafu mwili jumba niko na wenzangu wawili nimewazid ranks kwashingo upande suka kageuza gari mpaka moro.
Nikamwambia dogo moro ndio hapa ,dogo akasema asante bro akafungua begi lake akatoa chupa ya chai na mkate akaanza kugonga konda akamwambia shuka bas dogo akasema anaenda dom ila mama yake alimwambia akifika moro ndio anywe chai lunch atakula dom, unaambia gari zima macho yenye Jazba, hasira,husda,gubu, nongwa,dharau na uchungu yakaelekezwa kwangu hapo ndio ikabidi nizuge naenda kuchimba dawa nikakimbia nikawatext makamanda mizigo yangu nitaikuta kambini
Ni chai mimi niliisikia siku nyingi sana kwa bwakila kama sikoseiMkuu nimecheka sana, ila hii sio chai kweli hii?
chaiWakati fulani huko sekondari wakati tunafanya mitihani ya muhula kila tukitoka kwenye paper tunaulizana swali fulani umejibu vipi mimi ndio nakuwa kimbelembele kusema swali lile jibu lake ni hivi na vile,baada ya kumaliza mitihani na yalipotoka majibu mimi nikawa nimedisco wale wenzangu niliokuwa najadiliana nao kila tunapotoka kwenye peper wakatusua.Hapo ndipo nikajiona tumbili
Hapo sawa mamdogo.Ni chai mimi niliisikia siku nyingi sana kwa bwakila kama sikosei
Haha noma!Hii story nimeshahadithiwa na wengi huku mtaani.
Ni chai bila shaka
Niliwahi kujifanya mjumbe miaka ya 90, aiseeeh kilichonipata ni siri yangu.Habari zenu wanaJF. Kama kichwa cha habari kisemavyo hapo juu, katika harakati za hapa na pale katika maisha inaweza kutokea situation fulani tuu ukajikuta unajua kitu na kukifanya mbele za watu hatimae unaumbuka hapo ndo unakuja ule msemo usemao "utajua ujui".
Mimi binafsi miaka ya nyuma kidogo nilienda water park fulani hivi kurefresh kuogelea kwenye swimming pools kufika pale nikakuta kuna swimming pools za wakubwa zenye kina kirefu na za wadogo zenye kina kifupi. Sasa sikutaka hata kujiuliza kwanini kule kwenye kina kifupi ndio kuna watu wengi kuliko ile pool nyingine yenye kina kirefu nikaona potelea pote washamba tuu. Kwakweli sikuwa nimewahi kwenda before ndo ilikuwa ni mara ya kwanza ndipo kidume nikajikuta mjuaji kwamba ndio best diver sikutaka kwenda kwenye kina kifupi nikajichanganya kwenye swimming pool yenye kina kirefu na kulikuwa na alert kabisa pale ila mimi nikajiona much know. Basi nikaingia kwenye swimming pool taratibu nikiwa nimejiegemeza pembezoni kabisa huku ukutani nikicheki watu wawili watatu mule wakicheza michezo yao. Sasa sijui ni kitu gani kikanitekenya nikaona ngoja nisogee pale katikati nikajipush kutoka pale pembezoni yaani kama nilitumia nguvu ya ule ukuta kuswim hata pale kati sikufika vizuri nikaanza kuhisi kama navutwa ndani ya maji nikaanza kuvuta picha kwa wale wataalam wanavyo ogelea huwa kuna namna wana piga miguu ndani ya maji wanaelea basi na mimi nikaanza kufanya vile nikawa narudi juu kidogo nikiacha kupiga miguu nazama tena pale kwenye angle ya swimming napaona ila kupafikia ndio ilikuwa shughuli kwangu nilipiga sana miguu nikatumia utaalamu wote niliouona kwenye TV vile wanaogeleaga lakini wapi kupiga kelele za kuomba msaada napo nilikuwa naona aibu. Mwisho wa siku baada ya kutapatapa sana na ukizingatia kwenye angle palikuwa sio mbali basi nikachoka nikajiachia tuu nikawa nazama ndo kama nilikuwa naiona dunia inazunguka nikiwa ndani ya maji huku nikiwa nakunywa vikombe heavy vya maji taratibu kabisa. Wakati naelekea kufumba macho kuiaga dunia kwa mbali nikaona malaika ananipa mkono na mimi nikaona nimpe mkono japo kwa kujikongoja sana huku nikijisemea moyoni Bwana ametoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe, nikampa mkono. Mara ghafla nikaona nimeibuliwa kwa nguvu kutoka ndani ya maji kumbe alikuwa ni jamaa tuu nahisi alikuwa ananichora tuu tangu mda ule natapatapa. Basi akanivuta akanishikisha ile angle aisee niliing'ang'ania kwa nguvu zangu zote huku nikiwa nakohoa nikapanda hadi juu nje ya swimming pool kwa speed ya mwanga nikakaa pembeni nikiwa siamini yaliyo nitokea pale dakika chache zilizo pita huku kwa mbali nikisikia vicheko vya watu ni dhahiri kabisa mimi ndiye niliyekuwa nachekwa maana kwa wakati huo akili haikuwepo kabisa pale.
Nikanyanyuka nikatafuta nguo zangu zilipo nikavaa nikapiga msosi pale fasta nikaondoka zangu home bila hata kugeuka nyuma. Yaani hapo ndio nilijua sijui.
Vipi na nyinyi wadau ni kitu gani ulijifanya mjuaji ukaumbuka hebu tiririkeni hapo hata kama sio wewe lakini ulimshuhudia mtu mwingine,
karibuni.
True story mkuu ila imekaa kichaichai 😂Mkuu nimecheka sana, ila hii sio chai kweli hii?
Wewe dogo chenga sana ulisababisha kamanda akaonekana sungusunguHuyo dogo ni mim hapa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hii stori nimeishawahi kuisikia humu ila umeiedit kidogo...Tulikua tunaenda Dodoma na coaster tulipofika maeneo ya mbezi kuna dogo akamwambia konda tukifika morogoro naomba uniambie konda kama poa tukafika Kibaha dogo akauliza Moro bado ? Konda akasema bado ,tukafika chalinze dogo akauliza tena ,konda akawa mbogo mixa maneno ya shombo dogo kausha tukifika moro nitakwambia
Basi safari ikasonga baada ya masaa mwili dogo akauliza tena moro bado ? hapo tunaitafuta Gairo konda akasema dah! Moro tushapita dogo , kidume nikageuka mbogo na magwanda yangu ya JKT nikamwambia dereva geuza gari turudi Moro abiria wakamaindi kinoma sema wakiangalia konda kazingua wakiniangalia pia mimi ni mwanausalama halafu mwili jumba niko na wenzangu wawili nimewazid ranks kwashingo upande suka kageuza gari mpaka moro.
Nikamwambia dogo moro ndio hapa ,dogo akasema asante bro akafungua begi lake akatoa chupa ya chai na mkate akaanza kugonga konda akamwambia shuka bas dogo akasema anaenda dom ila mama yake alimwambia akifika moro ndio anywe chai lunch atakula dom, unaambia gari zima macho yenye Jazba, hasira,husda,gubu, nongwa,dharau na uchungu yakaelekezwa kwangu hapo ndio ikabidi nizuge naenda kuchimba dawa nikakimbia nikawatext makamanda mizigo yangu nitaikuta kambini
Basi sawachai
Kuna jamaa alibeba deki mpk shuleWale madogo ambao mlikua mnaangalia porn kwny zile deki za VHS na mara paaaaaap umeme unakatika na haujarudi mpk asubuhi haujarudi mbona siwaoni aisee?
Itakua yule dogo ndio amekuhadithia mkuu yuko humu piaHii stori nimeishawahi kuisikia humu ila umeiedit kidogo...
Itakua uliisikia kwa yule dogo yuko humu nasikia batmanwafezHii stori nimeishawahi kuisikia humu ila umeiedit kidogo...
Dah umenikumbusha nilikuwa redio flani Kuna jamaa namfaham kitambo Sana nikamuona mazingira hayo bwana we ziakanza salamu maraa pap kaongea ngeli nikasema alaaa usinidharaulishe na mi nikakirwanga af pembeni kulikuwa Kuna watu wakubwa tu na elimu zao.Mimi hapo zamani nilijifanyaga usalama wa taifa kumbe wale naowatambia ndio wazee wenyewe dahh walikuwa wanacheka kweli ila mwishoe nilijua Ila walinionya kwa usalama wangu nisipende kufanya nilivyofanya ile bar ndio ilikuwa mwisho wng kwenda.
Nyingine kuna mshkaji wng mmoja kitambo iko niliwahi kusoma nae kitambo iko academy flan sas tulipotezana kwa muda siku tumeonana alikuwa na wana mabishoo km wawili iyo siku bana nilikuwa gari ya mshkj wng nilivyokutana na mwamba siunajua mambo ya kuvimba tena nikaanza kupiga ngeli na mshkj yes no nyng wale wadau pemben wametulia tuu Wana smile kwa mbali nishapiga mkorogo broken za kutosha ili niwatambie wana apo tupo kweny ndinga. Bana Bana wale wadau wawili si wakaanza kuongea unaijua American English ya ma black yenye slain ya kihuni kumbe wajuba hawajui ata kiswali ni wabongo waliozaliwa USA bongo ndio first time yani. Mzee baba nilijiskia nishai kinoma mzee baba. Sema wao walichukulia poa tuu ila mm nilijishtukia sanaa
Kanisaniii...
Watumishi ilitokea wamepungua wawili, basi Father Akaomba yeyote anayejua Kutumikia apite mbele akavae joho, mzee mzima nikapanda madhabahuni nikaingia room nikavaa Joho..
Kwa kufupisha...
Nilichanganya madesa kuanzia kwenye uvaaji, kushika vifaa hasa cheteso,
Nikiangalia waumini wanaziba midomo, nikaona hii ni live nazingua sio kama najishtukia tuu.
Mambo yalivyozidi kua magumu, nikaone isiwe tabuu..
Nilichomokea mlango ule wa nyuma ya Altale, nikavua joho nikasepa misa ikiwa kati...
Niliacha vicheko na taharuki kwa waumini na Wote pale mbele, na ilikua mtu zaidi ya 200..
Pili nilitoka mjini nikaenda kijijini kusalimia, nikajitia najua ngumi tena za movie,
Nikalichokoza jamaa flani hivii...
Kilichonipata ilibidi niingie kwenye karavati, yeye alishindwa sababu ya mwili mkubwa.
🤣🤣🤣🤣🤣Kanisaniii...