Ushawahi kujifanya mjuaji ukaja kuumbuka?

He heh vp jamaa yenu hamkumuachia msala?
 
Nakumbuka nipo jo'berg south Africa na jamaa yangu fulani,,,tuna mipango tuelekee Swaziland,, ikafika muda jamaa njaa imemkamata,,,akaniomba rands 100 ili afanye mipango ya kula,,nikamjulisha kwamba rands 100 ni nyingi sana kwa mlo wake wa mara moja,,kama vipi nimpe rands 30 tu tosha kwa kupata chakula pale KFC,,ni mgahawa fulani south wanauza chakula fresh sn,,, nakumbuka ilikuwa 2010,,
Basi baada ya mzozo wa kama dk 10 ikabidi nimpe jamaa rands 100 ktk pesa zake nilizozishika,,,
Huyo jamaa alikuwa hajuwi kingereza hata cha kuuliza saa ngapi?
KFC ,,,tukapanga foleni ya kununuwa chakula,,,basi kwa ujuaji wa jamaa nikasema leo nakuwa mtazamaji kuangalia atakacho kiagiza,,basi jamaa akawa mbele yangu Mimi nikawa namfuata yeye ktk foleni,,,
Mara muhudumu wa KFC akaita NEXT PLZ...jamaa akasogea hadi pale kwenye desk la kuagiza chakula,,
Jamaa hakutaka mambo mengi zaidi ya kuonyesha moja ya picha zile za ukutani zizokuwa zimebandikwa ,,
Jamaa akasema THIS ONE..
aisee!!!baada ya kama dk 10 jamaa alipewa fuko zima la rambo limejaa mikate 10 pcs vipande vya kuku 20 pcs na coca cola chupa kama 4 hivi,,kumbe jamaa alipoint ile jumbo size ambayo ndy order ya family ,ambayo ndy size ya mwisho na kubwa Sana hata watu 2 hawamalizi,,,,,jamaa alitozwa rands 100 yote pale pale ilikiwisha,,
Kivumbi ni jamaa baada ya kuona anapewa lile fuko kubwa la Rambo,,
Jamaa alipokea lile fuko la chakula kwa mshangao mkubwa,,, ikabidi anitoe kwenye foleni,,jamaa akaanza kunibembeleze mm nisinunuwe tena chakula changu,,tule wote kile alichonunuwa yeye maana hatokimaliza ,,ili nimchangie pesa kuliko kununuwa chakula kingine ,,basi tulikula chakula kile siku 2,,,aisee!!!
Basi jamaa wakati anatoka pale kwnye foleni na fuko lake wa south wote wanamshangaa,,na mm nacheka sn,,,
Kwakifupi jamaa alitoka nishai hatari,,mwishowe aibu nimeona mm,,,
Ujuwaji haupendezi ,,kama hujuwi Kama kimya..
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]huyu maza lazma ashawahi kuwa mjeda.N vigumu sana raia wa kawaida kuzijua adhabu kama hz plus ile ya kukulisha wali week nzma
 
Mkuu sijaona Kabisa hapa ujuaji wa Mwanetu!!
 
Hii imefanana na zangu mbili ya King fish na chicken marsala [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Nilipigiwa simu nkafunge dish mahali. Huyo mtu akaniambia ni karibu na nyumba za usalama wa taifa. Kwa kiherere sijauliza vuzuri nkachukua toyo vuub mpaka nyumba za usalama wa taifa. Du nilikutana na vichalii fulani wakaniuhoji hoji nkashindwa kuwapa majibu ya kutosha. Nilipigishwa zoezi mpaka nkashindwa kusimama nkisimama miguu haina nguvu.

Mbaya zaidi waliponiruhusu nkawatukana nkawaambia tutakutana mtaani du wakanirudisha nilipigishwa kwata hadi nkaomba msamaha nkawambia nyie ni rafiki zangu. Nakumbuka nlipotoka getini nilitembea na matako hadi kwenye toyo miguu haina kazi. Wachana na hawa watu wanaotwa wasijulikana wasikie tu
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] nimecheka sana aisee. Umetupiga fix lkn
 
Hahahahahahaha
 
chai ya muarobaini
 
Mmhahahaah hahahaha unajua kusimulia tukioo nmecheka kinoma


Pole sana mwamba.
 
Chezea wajeda huhuhuhuh, afu huwa hawan undugu kabisa, poleeeeh San.
 
Tunywe hivi hivi au kuna maandazi yanakuja?
 
Hapo tatizo lilikuwa pesa aliyokuwa nayo mkononi au uchaguzi wa chakula
Tatizo ni pesa na uchaguzi wa chakula, mfano angekuwa na rands 30 hata Kama angeonyesha apewe ile big size isingetosha,,,
Wangempa kulingana na pesa yake,,maana unatoa pesa na halafu unasubiri oder yako..
 
mimi niliendaga msikiti mmoja kupata ibada ya swala....sasa kufika mahali pa kuchukulia udhu...nikakuta mabomba flani hivi yaani yamekaa kama unazungusha ili maji yatoke,mimi bila kuuliza /kuangalia wenzangu nikaanza kuzungusha....maji hayatoki nikakomaa kuzungusha lakini wapi hadi akaja jamaa akabinya maji yakatoka...nilijiona mshamba kama wa chato.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…