Nakumbuka nipo jo'berg south Africa na jamaa yangu fulani,,,tuna mipango tuelekee Swaziland,, ikafika muda jamaa njaa imemkamata,,,akaniomba rands 100 ili afanye mipango ya kula,,nikamjulisha kwamba rands 100 ni nyingi sana kwa mlo wake wa mara moja,,kama vipi nimpe rands 30 tu tosha kwa kupata chakula pale KFC,,ni mgahawa fulani south wanauza chakula fresh sn,,, nakumbuka ilikuwa 2010,,
Basi baada ya mzozo wa kama dk 10 ikabidi nimpe jamaa rands 100 ktk pesa zake nilizozishika,,,
Huyo jamaa alikuwa hajuwi kingereza hata cha kuuliza saa ngapi?
KFC ,,,tukapanga foleni ya kununuwa chakula,,,basi kwa ujuaji wa jamaa nikasema leo nakuwa mtazamaji kuangalia atakacho kiagiza,,basi jamaa akawa mbele yangu Mimi nikawa namfuata yeye ktk foleni,,,
Mara muhudumu wa KFC akaita NEXT PLZ...jamaa akasogea hadi pale kwenye desk la kuagiza chakula,,
Jamaa hakutaka mambo mengi zaidi ya kuonyesha moja ya picha zile za ukutani zizokuwa zimebandikwa ,,
Jamaa akasema THIS ONE..
aisee!!!baada ya kama dk 10 jamaa alipewa fuko zima la rambo limejaa mikate 10 pcs vipande vya kuku 20 pcs na coca cola chupa kama 4 hivi,,kumbe jamaa alipoint ile jumbo size ambayo ndy order ya family ,ambayo ndy size ya mwisho na kubwa Sana hata watu 2 hawamalizi,,,,,jamaa alitozwa rands 100 yote pale pale ilikiwisha,,
Kivumbi ni jamaa baada ya kuona anapewa lile fuko kubwa la Rambo,,
Jamaa alipokea lile fuko la chakula kwa mshangao mkubwa,,, ikabidi anitoe kwenye foleni,,jamaa akaanza kunibembeleze mm nisinunuwe tena chakula changu,,tule wote kile alichonunuwa yeye maana hatokimaliza ,,ili nimchangie pesa kuliko kununuwa chakula kingine ,,basi tulikula chakula kile siku 2,,,aisee!!!
Basi jamaa wakati anatoka pale kwnye foleni na fuko lake wa south wote wanamshangaa,,na mm nacheka sn,,,
Kwakifupi jamaa alitoka nishai hatari,,mwishowe aibu nimeona mm,,,
Ujuwaji haupendezi ,,kama hujuwi Kama kimya..