Ushawahi kusafiri kwenye basi umekaa na mtu yeye kila anachokiona njian yeye anakula tu,

Ushawahi kusafiri kwenye basi umekaa na mtu yeye kila anachokiona njian yeye anakula tu,

Bakalalwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2024
Posts
748
Reaction score
1,217
20250218_124152.jpg
Ilikuwaje? 😄
 
Mwache ale as long as hakubugdhi, binafsi sio mpenda kula njiani na zile kuku zao za juzi.

Bora safari za usiku, hamnaga kero za watu wa namna hiyo ila mchana unakuta mtu kafunga msosi toka kwake na bado njiani anakula hovyo.
 
Siku niko na dogo toka mkoani Arusha nampeleka kijijini Mbeya ilikua tabu.
Kuanzia ubungo ye anatafuna kila anachokiona, teremshia mimaji , chai, Coca-Cola twende.
Kufika ruvu tu kuitafuta moro alikoma.
Mpaka tufike msamvu hadi analia.
Toka pale katia adabu
 
Kuna siku nilipanda basi kwenye siti yangu ikabaki nafasi moja, kuna bidada mmoja mwenye shep matata nilitegemea aje akae yeye badala yake akasukumwa na mbwiga mmoja akawahi siti , yani nilitamani nimnase kibao yule fala basi tu.
 
kuna safari nilisafiri kwenda Ddm kutoka Dar, nilikuwa nimepata siri ya dirishani, akaja dada mmoja mwenye watoto watatu, basi akaanza kuagiza vitumbua lete, karanga lete, mayai lete, juisi lete, sasa vikavurugana kule ndani, alinitapikia nilimmaindi, gari zima walimuwashia moto
 
Wanadamu tumeumbwa tofauti na kila mmoja ana hulka na utashi wake.... ili kuweka msawazo kwenye jamii tunapaswa kuvumiliana.......

Kama jambo lake halikuathiri moja kwa moja wewe basi yapaswa kumvumilia tu
Kuna jambo linaweza kuathiri assume umekaa siti moja na mtu anatafuna kama nguruwe nlanlanlanla nla ,nakulamba mavidole kama jinga🤔
 
Back
Top Bottom